Unafikiri hayajui yote hayo Mkuu?Basi tu kaamua kujifanya punguani lakini hilo wala halihitaji kwenda shule kujua faida watakazopata wanamtwara endapo madai yao yatasikilizwa.
Mkuu suala sio kujifanya punguani kinachonisikitisha ni kuona fujo, kuharibu mali za watu wasio na hatia na umwagaji damu bila hao wanaofanya hizo fujo kujua kuwa wanatumiwa kwa faida ya watu wachache. Tanzania karibia kila mkoa una rasilimali ambazo zikutumiwa ipasavyo bila kuwanufaisha wachache ni manufaa kwa wakazi wa mikoa hiyo na watanzania kwa ujumla wake lakini kinachofanyika sasa wanaonufaika ni wachache wenye madaraka, mafisadi na tena wasio na uchungu na nchi. mfano Geita kuna dhahabu lakini angalia geita leo. Shinyanga tangu niko mdogo nasikia almasi Mwadui angalia shinyanga ilivyo, Arusha Tanzanite, na mikoa mingi mingineyo je ni kweli sisi hohehae tunanufaika nazo wakati ziko kwenye mikoa yetu? Geita nasikia sina uhakika kuwa mkataba ni miaka miamoja? baada ya hapo geita ikoje serikali haina hata hisa kwenye huo mgodi, na SHERIA ZETU NI DHAIFU ZA KULINDANA ZIMETUNGWA NA MUHIMILI AMBAO NI BUNGE. ndio manaana mtu akiboronga hapa anahamishiwa pale badala ya kuwajibishwa? tufanyeje "KATIBA MPYA"
Nini kifanyike basi tuanzishe fujo kwenye kila mkoa wenye rasilimali kwa kuchoma nyumba za watu, kuua, kuharibu barabara, kuvunja madaraja, kung'oa reli ili tupate haki zetu, kazi za wabunge wetu ni kutushawishi kufanya fujo ili wao waonekane ndio wabunge wazuri wanaotetea maslahi yetu (kujipaka mafuta kwa mgongo wa chupa) wakitudandanya ndio haki itapatikana na dunia ijue tunaonewa au kazi zao ni kuwatetea kwa nguvu zote ili ile rasilimali itunufaishe wanachi. na akishindwa tumwajibishe yeye tuliyemchagua? Maana shida hii sio Mtwara tu ni Tanzania nzima ila watu leo masikio yao yako mtwara kesho masikio yatakuwa wapi? Kahama? Mwadui, Mara, Geita, Arusha, Kilimanjaro, Serengeti, ngorongoro au wapi maana kote kuna wahanga ambao ni watanzania masikini wanaoteseka kwa mengi? maana kila mkoa unarasilimali Mungu kweli alitubaliriki lakini ndio tunaongoza kwa umasikini.
Tufanye nini basi kama na Wabunge tuliowaamini wako kiitikadi zaidi kila mmoja anataka umaarufu lakini kiukweli wako kimasilahi yao zaidi dawa ni kuwawajibisha wabunge na mawaziri ambao ni serikali kwa kusaini mikataba mibovu na kutokujali wananchi tusikubali sisi ndio tuwe chambo cha wao kupandia ngazi kwa kutochochoea tufanye fujo mimi nafikiri kila sekta iamke lakini sio kwa uvunjifu wa amani? hata kama ni mwenyekiti wa kijiji wananchi wamwajibishe pale anapoenda kinyume maana kawekwa kusimamia wananchi kwa nini agawe ardhi ya kijiji kwa matakwa yake.
Nionavyo matatizo ni makubwa zaidi lakini tutayatatua kwa jinsi wanavyofanya wanamtwara? fujo, kuua, kuchoma nyumba za watu, kuvunja madaraja? wewe unaonaje hapo? hasara ni kwa nani unapovunja daraja? kwa yule aliyevaa suti huku anapigwa na kiyoyozi au wewe unayeenda kuvunja hilo daraja? Maana wakati wewe unapoenda kuvunja yeye kapanda ungo na kuruka? Kwa nini yeye asiende nasi tukavunja hilo daraja tukiwa wote bega kwa bega tujue kweli anastahili kuwa kiongozi wetu maana yu pamoja nasi kwa shida na raha.