Sielewi vizuri lengo la post hii, ila nataka kufahamisha kuwa Kiaro na Musuguri walipanda cheo kimoja baada ya kingine kuanzia private mpaka walipofikia. Mwaka 1972, tulipigina kidogo na Amin pale Mutukula, na alieyongoza mapigano yale alikuwa Colonel (wakati huo) Musuguri. Mpaka mwaka wa 1985 wakati bado najaua mambo ya jeshi letu, vyeo vya maofisa wote wa jeshi vilikuwa vinatolewa kwa ridhaa ya rais ambaye ndiye amiri jeshi mkuu. Hata hivyo utoaji wa vyeo vya kuanzia junior na senior officers, yaani 2nd. Lt. had Lt. Col. ilikuwa ni lazima recommendation itolewe na Ngome, halafu Rais anabariki. Baada ya hapo, vyeo vya juu (superior officers, yaani wenye alama nyekundu kwenye collar) kuanzia colonel na kuendelea vilikuwa vinatolewa na rais kwa kushauriana na CDF pamoja na Chief of Staff tu; na superior officers waliokuwa wakipandishwa vyeyo kwa njia hii ilikuwa ni kuanzia Colonel na Brigadier tu. Vyeo vyote vilivyokuwa vinatolewa kukiwa na baraka za jeshi vilikuwa vinathamini sana uwezo wa mtu kijeshi, ingawa katika miaka ya themanini siasa zilianza kuharibu kidogo utaratibu huu ambapo makada wa Chama (kama akina Nsa Kaisi) walipewa vyeo vya ukanali from nowhere. Zaidi ya kuvurugwa kidogo na hizo siasa, ni lazima tukubali kuwa watu waliopanda ngazi baada ya ngazi hadi kuwa mabrigadier walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuongoza jeshi. Musuguri, Marwa, na Kiaro ni baadhi ya maofisa waliopanda namna hiyo.
Juu ya Brigadier, yaani Major General, Luteni Gen na General ni vyeo vilivyokuwa vinatolewa na rais tu kwa kushauriana na mashushushu wake, na wala havikuwa na mkono wa mtu yeyote jeshini; ni kama vyeo vya kuteuliwa. Mara nyingi inasemekena kuwa utoaji wa vyeo hivyo ulifuata popularity jeshini (hii ilikuwa ni muhimu sana ili kuridhisha wapiganaji), royality (katika miaka hiyo ambapo majeshi yalikuwa yanaweza kuangusha utawala wa kiraia). Hakukuwa na formula yoyote juu ya utoaji wa vyeo hivyo. Generel Twalipo alipandishwa cheo na Nyerere kutoka Luteni Kanali hadi kuwa Major General (akiruka vyeo vya Kanali na Brigadier) kwa vile alitoa siri ya mapinduzi yaliyokuwa yamepikwa na sarakikya, kwa hiyo alikuwa ni Royal kwa Nyerere.
Kuna wasomi wengi sana ambao hawakupata kuteuliwa kushika vyeo vya juu sana kutokana na ubovu wa muundo wa jeshi letu wakati huo. Brigadier ilikuwa ni lazima awe Brigade commander, kwa hiyo ilikuwa lazima awe na Brigade yake. Wasomi na wataalam wengi wa kijeshi wakawa wanaishia kwenye Ukanali ambacho ndicho kilikuwa cheo cha juu kutolewa chini ya recommendation ya Ngome na hakikuwa na ulazima wa kuwa batallion Commander. Hii ilikuwa ni unfortunate sana, kwa mfano unakuta kuwa kwa vile Colonel Lupogo ndiye alikuwa mtaalam mkuu wa kupanga vita, position yake ile ilikuwa ni ya muhimu sana kwa jeshi zima kuliko kumfanya awe Brigade commander wa brigade moja; kwa hiyo akaendelea kubaki kama Kanali na mkuu wa mipango ya kivita.
Thanks Kichuguu,
Hizi evidence ndio wenzangu wanakosa zaidi ya kuleta story za mtaani. Appointment za ngazi ya juu kabisa ya jeshi sehemu nyingi hata Marekani huwa ni ridhaa ya rais ambayo mara nyingi haijali elimu ya Havard au WestPoint!