Shujaa: Maj Gen Mwita Chacha Marwa "Kambale" Afariki

Philemon Mikael,

..for your information Gen.Ricardo Sanchez ana degree ya Maths. Ge.Petreas ana PhD toka Princenton. Gen.Wesley Clark ni Rhodes scholar. sasa kwanini ktk jeshi letu wenye elimu watengwe kama wakoma?

Unaongelea kuwa wasomi wanatengwa sasa hivi au walitengwa zamani? Kwa nini Sanchezi alipewa nafasi kubwa kwa kuwa na degree ya math wakati Petreas alikuwa na PhD? Mbona aliyemteua Sanchez kwanza hakumteua Petreas that time pamoja na Phd yake?

Ni wanajeshi wangapi kati ya wanajeshi milioni moja na ushee wa marekani wana degree? je wote wenye position kubwa jeshini ni wasomi wa princeton?
 
phillemon mikael,

..nauliza tena: kwanini wenye elimu wanatengwa kama wakoma huko jeshini?

..hivi pale UDSM wakiamua kumteua VC ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi wewe utaunga mkono ilimradi chini yake kuna wataalamu waliobobea?
 
ELEWA KUWA JESHI SIO TAASISI YA KITAALUMA PEKEE...THAT IS A FORCE....SASA HUONI CHUO KIKUU NI TAASISI YA KITAALUMA NA YA WANATAALUMA TU!!!!......
 
mwafrika,

..kwanza ungemrekebisha Phillemon kwa kujaribu kutu-mislead.

..turudi hapa kwa Twalipo,Musuguri, na Kiaro. Nadiriki kusema kwamba hawa elimu yao ilikuwa ya ngumbaru na utaalamu wao wa kijeshi ulikuwa mdogo kulinganisha na Chief of Staffs wao. Sasa ni kigezo gani kilichotumika kuwateua kama siyo upendeleo wa namna fulani?
 
Japo mfano unaotoa hauendani hata kidogo na jeshi (shule ya msingi na UDSM ni mifumo tofauti, na yote ina wakuu wake kwa utaratibu wake), napenda kukusaidia taarifa.

Ibrahim Kaduma na Nicholaus Kuhanga walishawahi kuwa ma-VC pale UDSM na hawakuwa maprofesa wala hawakuwa na PhD. Lakini walikuwa na elimu ya chuo kikuu, na waliwaongoza maprofesa na watu wengine wenye PhD zao. Endelea kutafakari.
 
Phillemon,

..Jeshi ni taasisi ya KITAALAMU kama zilivyo taasisi nyingine.

..ili tujenge jamii yenye maendeleo basi ni lazima tuhakikishe kwamba wale waliobebea ktk taaluma zao wanapewa nafasi kuongoza.
 
Bado hujatoa evidence yoyote katika utendaji wao wa kijeshi!

Katika elimu wote wamekuonyesha hapa kuwa kina musuguri na kiaro walikuwa na elimu ya jeshini. Haya ya kushindanisha nani alisomea wapi ili kufaa kuwa kiongozi wa jeshini yamepitwa na wakati.

Mfano wako wa kuteua mwalimu wa shule kuwa VP wa mlimani hauna kabisa uhusiano wowote na mambo ya jeshi ambayo factors nyingi zinatumika kupandisha mtu kutoka rank moja kwenda nyingine.

Kwa sasa wewe ndio unasubiriwa utoe evidence kuwa kina musuguri utendaji wao ulikuwa mbovu.

So far evidence za Kichuguu kuhusu vita ya Kagera na Philemon kuhusu elimu ya kijeshi zinafit standard ya JF. Za kwako bado ni speculatiion tu kwa hiyo mpira uko upande wako!
 
Japo mfano unaotoa hauendani hata kidogo na jeshi (shule ya msingi na UDSM ni mifumo tofauti, na yote ina wakuu wake kwa utaratibu wake), napenda kukusaidia taarifa.

Ibrahim Kaduma na Nicholaus Kuhanga walishawahi kuwa ma-VC pale UDSM na hawakuwa maprofesa wala hawakuwa na PhD. Lakini walikuwa na elimu ya chuo kikuu, na waliwaongoza maprofesa na watu wengine wenye PhD zao. Endelea kutafakari.

Asante sana Mwalimu Kithuku na Mwalimu Kichuguu. Wakati mwingine inafurahisha kuona walimu mkitoa shule hapa zenye uthibitisho zaidi ya story tu na speculation kama zile tulizosikia kuwa Mwinyi hakujua kiingereza na kuwa Kawawa hakujua kusoma ila walipendelewa tu na Nyerere.
 
Kithuku,

..sasa nakuongezea na Pius Msekwa naye alikuwa VC wa UDSM. Natumai unaelewa madhara ya ma-VC hao.

..Msekwa aligeuza UDSM kuwa tawi la CCM, matokeo yake wataalamu wengi wetu wakaachia ngazi.

..Ibrahim Kaduma "Ibra-Kadu" naye alivuruga kazi pale UDSM kwa kiburi na ujeuri wake. Nicholas Kuhanga naye kazi ilimshinda.

..Kwa kifupi endelea kutafakari uongozi wa Kaduma,Kuhanga,Msekwa vs wa Prof.Pratt, Prof.Chagula,Prof.Mmari.
 
Phillemon,

..Jeshi ni taasisi ya KITAALAMU kama zilivyo taasisi nyingine.

..ili tujenge jamii yenye maendeleo basi ni lazima tuhakikishe kwamba wale waliobebea ktk taaluma zao wanapewa nafasi kuongoza.

Hapa sasa nimeanza kuamini kuwa unabisha tu ili kuendeleza ubishi na wala sio ku-counter argument au kuleta uthibitisho kuwa Kina Marwa na wenzake hawakuwa na elimu yoyote ya kijeshi na wala hawakufanya kazi kubwa jeshini kustahili vyeo vyao kama ulivyoanza mwanzoni.
 
Nimesoma kwa makini hoja kdhaa hapa. Tatizo ziko mahali pasipotakiwa. INGEKUWA NI AGENDA TOFAUTI. Why linked na kifo Cha Marwa? Wheather tukubali tukatae Haya majamaa ni mashujaa kwelikweli. Jeshi si sanaa, jeshi means you put life in line. you kill and be ready to die!. Hivi mnajua historia ya mapambano ya uhuru kusini mwa Africa? kuanzia Msumbiji, Zimbabwe, Angola n.k kisima cha mafunzo kilikuwa wapi? hao walimu walitoka marekani? no kwa hiyo msichanganye mambo ya jeshi na BAs Masters and PhDsssss. kupanda CHEO JESHINI Vilevile unatakiwa uwe jasiri MURA!!! Sio Madegree yako!! kafundishe chuo kikuu basi a aaa aa KWI KWI

RIP MAJOR GEN. MWITA MARWA.
 
Kithuku,

..sasa nakuongezea na Pius Msekwa naye alikuwa VC wa UDSM. Natumai unaelewa madhara ya ma-VC hao.

..Msekwa aligeuza UDSM kuwa tawi la CCM, matokeo yake wataalamu wengi wetu wakaachia ngazi.

..Ibrahim Kaduma "Ibra-Kadu" naye alivuruga kazi pale UDSM kwa kiburi na ujeuri wake. Nicholas Kuhanga naye kazi ilimshinda.

..Kwa kifupi endelea kutafakari uongozi wa Kaduma,Kuhanga,Msekwa vs wa Prof.Pratt, Prof.Chagula,Prof.Mmari.

Hapa sasa kuna upana mkubwa unataka kuleta katika hii thread. Kuna wasomi kibao tu wametumia usomi wao kuharibu nchi ukianzia na PhD mwenyewe mzee Malecela ambaye amekuwa makamu wa CCM kwa miaka nenda rudi, waziri mkuu na mengine mengi tu!
 
Nimesoma kwa makini hoja kdhaa hapa. Tatizo ziko mahali pasipotakiwa. INGEKUWA NI AGENDA TOFAUTI. Why linked na kifo Cha Marwa? Wheather tukubali tukatae Haya majamaa ni mashujaa kwelikweli. Jeshi si sanaa, jeshi means you put life in line. you kill and be ready to die!. Hivi mnajua historia ya mapambano ya uhuru kusini mwa Africa? kuanzia Msumbiji, Zimbabwe, Angola n.k kisima cha mafunzo kilikuwa wapi? hao walimu walitoka marekani? no kwa hiyo msichanganye mambo ya jeshi na BAs Masters and PhDsssss. kupanda CHEO JESHINI Vilevile unatakiwa uwe jasiri MURA!!! Sio Madegree yako!! kafundishe chuo kikuu basi a aaa aa KWI KWI

RIP MAJOR GEN. MWITA MARWA.

Maarifa,

kuna watu wako kwenye mission ya kuandika upya historia ya nchi ili kulaumu kila baya linaloendelea sasa hivi kwenye serikali ya awamu ya kwanza.

Kila nafasi wanayopata wanaitumia kufit context yao na sasa wanazidi kuchemsha na kuumbuliwa!
 
wewe hata kama umekulia baracks ..utakuwa ni mtoto mdogo sana na sana sana utakuwa ukisikiliza majungu yaliyotokana na frustration za baba yako ao whoever jioni akirudi kazini....maana hizo unazoongea zote ni hear saying na yalikuwa ni mastori ya kawaida miaka ya 80...kama zile stori nyingine za kawawa hajui wala hasikii kingereza ....

but ukija kwenye reality,.....hawa kiaro,na musuguri walikuwa ni infatria tactician by proffession ...so definatelly walikuwa na washauri wa fani nyingine kama ndege,logistics,communication,navy ets....hawaongozi peke yao...kuna aliyesema tumekuwa na historia ya ma chief of staff wasomi zaidi...HILO NI KWELI...

kuwa hawajui kusoma hilo nakataa hawa wote wameanzia chini ,...na wote wametrain SUNDHURST.....

Kiaro na Msuguri hawajuhi kusoma wala kuandika. Washauri unaosema wewe ndio watendaji wa kazi za kila siku. Hao wazee walikuwa wanaogopa kwenda likizo kwa kuogopa nafasi zao kuchukuliwa.
 
Mwafrika,

..Kiwelu amepata mafunzo ya officer cadet Sandhurst. sasa niambie Kiaro na Musuguri wamepata mafunzo yao wapi kama siyo kwa promotions za Africanization!!

..Kiwelu alikuwa chief of staff wa Twalipo. Ina maana alikuwa senior kwa Musuguri na Kiaro.

..Kiwelu aliongoza mapambano ya kumuondoa Amini ktk ardhi ya Tanzania. Baada ya hapo akarudi ngome kwenye planning na logistics. Hiyo inaonyesha jinsi gani wataalamu wa aina yake wako flexible na well rounded.

..Kabla na baada ya vita vya Kagera, Kiwelu alikuwa senior kwa Musuguri, lakini akapitwa kwenye promotion ya kuwa CDF.

..Kiwelu tena kama Major General alikuwa senior kwa Kiaro, lakini Kiaro akawa promoted to General na Kiwelu to Lt.Gen, and Kiwelu was made to serve under Kiaro kama Chief of Staff.

..Maj-Gen.Herman Lupogo ni graduate wa Makerere. Pia aliwahi kuwa CO wa Monduli. Wasomi hao ndiyo wameweka standards pale mpaka tunaheshimika kimataifa. Makamanda wote wa Monduli walikuwa wasomi na waliopata mafunzo ktk vyuo vinavyoeleweka vya kijeshi.

Sielewi vizuri lengo la post hii, ila nataka kufahamisha kuwa Kiaro na Musuguri walipanda cheo kimoja baada ya kingine kuanzia private mpaka walipofikia. Mwaka 1972, tulipigina kidogo na Amin pale Mutukula, na alieyongoza mapigano yale alikuwa Colonel (wakati huo) Musuguri. Mpaka mwaka wa 1985 wakati bado najaua mambo ya jeshi letu, vyeo vya maofisa wote wa jeshi vilikuwa vinatolewa kwa ridhaa ya rais ambaye ndiye amiri jeshi mkuu. Hata hivyo utoaji wa vyeo vya kuanzia junior na senior officers, yaani 2nd. Lt. had Lt. Col. ilikuwa ni lazima recommendation itolewe na Ngome, halafu Rais anabariki. Baada ya hapo, vyeo vya juu (superior officers, yaani wenye alama nyekundu kwenye collar) kuanzia colonel na kuendelea vilikuwa vinatolewa na rais kwa kushauriana na CDF pamoja na Chief of Staff tu; na superior officers waliokuwa wakipandishwa vyeyo kwa njia hii ilikuwa ni kuanzia Colonel na Brigadier tu. Vyeo vyote vilivyokuwa vinatolewa kukiwa na baraka za jeshi vilikuwa vinathamini sana uwezo wa mtu kijeshi, ingawa katika miaka ya themanini siasa zilianza kuharibu kidogo utaratibu huu ambapo makada wa Chama (kama akina Nsa Kaisi) walipewa vyeo vya ukanali from nowhere. Zaidi ya kuvurugwa kidogo na hizo siasa, ni lazima tukubali kuwa watu waliopanda ngazi baada ya ngazi hadi kuwa mabrigadier walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuongoza jeshi. Musuguri, Marwa, na Kiaro ni baadhi ya maofisa waliopanda namna hiyo.

Juu ya Brigadier, yaani Major General, Luteni Gen na General ni vyeo vilivyokuwa vinatolewa na rais tu kwa kushauriana na mashushushu wake, na wala havikuwa na mkono wa mtu yeyote jeshini; ni kama vyeo vya kuteuliwa. Mara nyingi inasemekena kuwa utoaji wa vyeo hivyo ulifuata popularity jeshini (hii ilikuwa ni muhimu sana ili kuridhisha wapiganaji), loyality (katika miaka hiyo ambapo majeshi yalikuwa yanaweza kuangusha utawala wa kiraia). Hakukuwa na formula yoyote juu ya utoaji wa vyeo hivyo. Generel Twalipo alipandishwa cheo na Nyerere kutoka Luteni Kanali hadi kuwa Major General (akiruka vyeo vya Kanali na Brigadier) kwa vile alitoa siri ya mapinduzi yaliyokuwa yamepikwa na sarakikya, kwa hiyo alikuwa ni Loyal kwa Nyerere.

Kuna wasomi wengi sana ambao hawakupata kuteuliwa kushika vyeo vya juu sana kutokana na ubovu wa muundo wa jeshi letu wakati huo. Brigadier ilikuwa ni lazima awe Brigade commander, kwa hiyo ilikuwa lazima awe na Brigade yake. Wasomi na wataalam wengi wa kijeshi wakawa wanaishia kwenye Ukanali ambacho ndicho kilikuwa cheo cha juu kutolewa chini ya recommendation ya Ngome na hakikuwa na ulazima wa kuwa batallion Commander. Hii ilikuwa ni unfortunate sana, kwa mfano unakuta kuwa kwa vile Colonel Lupogo ndiye alikuwa mtaalam mkuu wa kupanga vita, position yake ile ilikuwa ni ya muhimu sana kwa jeshi zima kuliko kumfanya awe Brigade commander wa brigade moja; kwa hiyo akaendelea kubaki kama Kanali na mkuu wa mipango ya kivita.
 
Historia Haidanganyi and you cant force it. itakugeuka one day. Binadamu si Mungu. Ndiyo juLius baada ya uhuru hakung'ang'nia madaraka. he let it go! na alisema anatakiwa mtu wa kufikiri kulingana na wakati wa sasa. So tuna wakati wa kutengeneza mambo vema badala ya kukaa na kuandika historia ya kuangalia mchawi wa 1961. aaaaa. I dont buy that.
 
Mwafrika,

..aliyeleta habari ya Kaduma na Kuhanga ni Kithuku. Uteuzi wao ulizingatia siasa kuliko taaluma na matokeo yake yanajulikana. lets stick kwenye mada.
 
Kiaro na Msuguri hawajuhi kusoma wala kuandika. Washauri unaosema wewe ndio watendaji wa kazi za kila siku. Hao wazee walikuwa wanaogopa kwenda likizo kwa kuogopa nafasi zao kuchukuliwa.

Naona hii sasa ni chini hata ya kiwango cha kawaida cha ubishi wa watoto wa shule za awali. Kyaro na Musuguri hawakujua kusoma?
 
Mwafrika,

..aliyeleta habari ya Kaduma na Kuhanga ni Kithuku. Uteuzi wao ulizingatia siasa kuliko taaluma na matokeo yake yanajulikana. lets stick kwenye mada.

Hii bado haijakutoa kwenye hook ya kujibu swali nakuleta evidence kuwa Kyaro, Msuguri na wenzake hawakuwa na elimu yoyote na pia utendaji wao haukustahili kabisa kupanda ranks hadi kufikia walikokuwa.

Bado unasubiriwa hapo!
 
ELEWA KUWA JESHI SIO TAASISI YA KITAALUMA PEKEE...THAT IS A FORCE....SASA HUONI CHUO KIKUU NI TAASISI YA KITAALUMA NA YA WANATAALUMA TU!!!!......

Jeshi sio taasisi ya kitaaluma na vile vile Ikulu sio ofisi ya kitaaluma. Lakini wanaoajiriwa na kupewa ngazi za juu ni lazima wajue kusoma na kuandika.
 
Back
Top Bottom