shombeshombe,chotara nini tofauti?

ummu kulthum

JF-Expert Member
Feb 6, 2012
2,785
1,317
jamani wapedwa kuna utata umejitokeza chit-chat kuhusu utofauti wa hayo maneno hapo juu.naomba ufanunuzi please!
 
kumbe siko peke yangu watu ishiri walioview hakuna hata aliyepapasa ka jibu,kiswahili ki gumu jamani
 
Ngoja nijaribu, kimsingi maneno hayo hayana tofauti ni kama ni moja ni mbadala wa lingine, maana kwa kiingereza yote yanafasiriwa kama Mixes breed au Half caste! lakini hili Shombe limedadavuliwa zaidi kwa kuonesha ni mchanganyiko wa damu hasa ya mwarabu na watu wa jamii nyingine, wakati Chotara ni " coloured" na haijalishi amechanganya vipi damu! nawasilisha
 
kilebwe asante kwa kunipa mwaga hafifu ngoja tuwasubiri na wengeni.............
 
Last edited by a moderator:
ummu kulthum kwa Mujimu wa Kamusi ya TUKI

shombe nm ma- [a-/wa-] halfcaste person, mulatto, mixed blood, coloured.


chotara
nm [a-/wa-]

1. chotara = half caste, mulatto.

2. chotara = mixed breed, crossbreed (of seeds or animals):


  • Kuzaa watoto chotara = miscegenation;
  • Mbwa chotara = mongrel/mutt;
  • chotara wa Kiberiberi na Kiarabu = Moor.

miscegenation n uchotara, usuriama; kuzaa watoto chotara.

.
 
jamani wapedwa kuna utata umejitokeza chit-chat kuhusu utofauti wa hayo maneno hapo juu.naomba ufanunuzi please![/QUOTE]
Kwa mtazamo wangu ni vyema kwanza kujua maana ya Chotara na shombeshombe
Chotara naamini na mchanganyiko wa damu au asili ya mataifa mawili tofauti kwa level ya mabara na mchanganyiko wa asili ya mabala tofauti
kwa maana hiyo naamini hata mchanganyiko wa makabila mawili unazalisha Chotara
Shombeshombe ni mchanyiko wa wabantu na watu wenyeasili ya uarabu huo ni mtazamo wangu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
:spy::spy:
 
Back
Top Bottom