Albedo,Mtanzania Mbona Ukada unakufanya unakuwa Kipofu hivi
CDM wameshawahi kuwatuhum u CCM kwamba walipitisha Magari yao bila kodi TRA wakawataka CDM wapeleke USHAHIDI. Lakini TRA baada ya kusikia Nape anasema Slaa halipi kodi TRA wakaanzisha Uchunguzi. Mkuu Mtanzania Wananchi wanaona na kupima Usanii wote huu na naamini una mwisho wake.
TRA ni wezi tu na ndio maana wameamua kupambana na CDM
Albedo,
Nijuavyo mimi CCM walilipa kodi ya magari hayo na kutoa ushahidi. Kama una ushahidi tofauti basi ni vizuri kuumwaga hapa JF.
Hata kama CCM hawakulipa basi nao wanafanya makosa hayo hayo.
Hili si suala la kisiasa na tukilijadili kisiasa tunakosea mno. Kama CCM wameishingia bango CHADEMA basi ndio muda muafaka kwa CHADEMA nao kuja na ushahidi kuonyesha CCM wana kwepa kodi.
Pia ni vizuri kama mtu unataka kuleta mabadiliko basi uwe whiter than white. Itakuwa ni makosa makubwa sana kwa CHADEMA kufikiri wanaweza kutumia njia zile zile chafu za CCM kwasababu CCM nao wanafanya. Watu hupenda kubaki kwenye status quo unless mabadiliko yataleta mambo mazuri zaidi.
Yaani haiingii akilini chama cha siasa kushindwa kulipa kodi lionekane jambo la kawaida. Nitaelewa kama wametumia accounting principles kukwepa kulipa kodi kwa kutumia sheria zilizopo kama yanavyofanya makampuni mengi makubwa. Lakini kushindwa kabisa kulipa hata kodi za ajira za wafanyakazi kwa kweli hapo ni dalili kwamba sisi sote ni wababaishaji tu na siasa zetu za kudanganyana. Hilo halijalishi ni CCM au CHADEMA.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeitoza faini ya sh. milioni 100 CHADEMA, baada ya kubainika inakwepa kodi tangu ilipoanzishwa mwaka 1992. TRA pia imeanza kukata kodi mshahara wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa na watumishi wengine wa CHADEMA.
"Ijapokuwa tangu ilipoanzishwa ilikuwa hailipi kodi, katika uchunguzi tulipata taarifa za kuanzia mwaka 2000 hadi sasa zinazoonyesha hailipi kodi,'' kilisema chanzo hicho.
Mkuu Albedo,Mkuu Mtanzania Heshima
Siungi mkono suala la mtu au Chama chochote chochote kukwepa Kulipa Kodi, nonachopingana ni taasisi ya Serilkali Kutumika Kisiasa. Kubali kataa hata Mtoto Mdogo ambaye hajaenda shule anaweza kabisa kuchambua na kuona kwamba TRA wametumika Kisiasa. Haiwezekani CDM wawe hawali[pi kodi toka Mwaka 1992 halafu leo hii Baada ya kumsikia Nape anasema Dr. Slaa halipi kodi na wenyewe "Wakasema watachunguza" Mbona CDM walivyosema kwamba CCM hailipi kodi TRA hawakuidaka hiyo ishu na kuahidi kuanza Uchunguzi.
Mkuu TRA wameamua kupambana na CDM kwa niaba ya CCM.
Hebu Cheki Hii Statement
Halafu Cheki na hii
Yaani hata Mtoto aliyesoma Shule ya Kata na akafeli anatambua wazi kwamba hii Taarifa imeandaliwa Lumumba
Mtanzania, Ebu nielemishe kidogo. Umesema Chadema wanategemea ruzuku na hivyo wanatakiwa kulipa kodi.. Huu mchezo unakwenda vipi fedha inatoka kwa serikali (fungu la Kodi) kisha inatakiwa kulipiwa kodi.. Ni kodi gani hiyo?..
Pili, Katika sehemu yoyote ya ajira mwajiliwa na mwajiriwa wote hujitegemea inapofika swala la kutolipa kodi, unless Chadema walitakiwa kukusanya kodi ya mtu (Dr.Slaa) kwa niaba ya TRA. Sasa kama Dr.Slaa hakulipa kodi kwa miaka kadhaa ni jukumu la TRA kuyamaliza na Dr.Slaa sio kukihusisha wala kukihukumu chama ktk makosa ambayo yamefanywa na mwajiliwa. Na ndio maana Bungeni wabunge woote huwakilisha orodha ya mali zao kwa malengo sio tu kufahamu mali zao bali kikubwa zaidi ni kutazama viongozi wamelipa kodi za kumiliki mali hizo na wapo ktk maadili mazuri ya uongozi bora. Itachekesha sana tunapokazania ulipaji kodi wakati asilimia kubwa ya wabunge wenyewe watunga sheria hawalipi kodi hivyo kukiuka miiko yao sheria waloitunga wao..
Sasa leo naposoma haya ya TRA na kuonyesha kwamba Dr.Slaa alipokuwa Mbunge hakuwahi kulipa kodi... Hii inanipa mshtuko zaidi kwa serikali yetu kutoweza kukusanya miaka mitano iliyopita na wala sii jukumu tena la Dr.Slaa bali serikali inayozembea kukusanya kodi zake. Vitu kama hivi huwezi kuvikuta nchi za huku, Yaani Taasisi ya serikali iloshindwa kukusanya kodi toka kwa watunga sheria lakini wepesi wa kukumbuka kutoza adhabu baada ya kuadhiriwa... Huyo mkulu wa TRA angekuwa hana kazi kutokana na scandal ya Dr.Slaa, lakini kwa - Miafrika Ndivyo Tulivyo ndio kwanza anapewa sifa!
Mkuu Mkandara,
Kwanza, nimeongelea ruzuku kama njia mojawapo ya mapato ya vyama vya siasa. Wana mapato yao mengine. Pia wana wafanyakazi ambao wameajiriwa na wanatakiwa kulipa kodi.
Hiyo kodi ya wafanyakazi ndio haijawahi kupelekwa TRA. Sasa kama wewe unafaidika na ruzuku ambayo inatokana na kodi ya Watanzania, ningetegemea uwe wa kwanza kuelewa umuhimu wa kulipa kodi.
Pili, suala la mtu aliyeajiriwa, kodi yake hulipwa na mwajiri wake. Kwenye suala la Dr. Slaa ni kosa la CHADEMA kwamba hawajalipa kodi yake. Ingelikuwa amejiajiri hapo ndipo yeye mwenyewe angetakiwa kuhakikisha kodi yake inalipwa TRA. Lakini ukisema chama cha siasa hakilipi kodi, huwezi kuwaondoa viongozi wake wakuu katika lawama.
Tatu, Suala la viongozi kuwakilisha mali zao tume ya maadili, halina uhusiano na kodi au TRA. Hilo ni kwa lengo la kujua kama wamezipata hizo mali kihalali au la.
Nne, sijaona mahali popote wakisema Dr. Slaa alipokuwa mbunge hakuwahi kulipa kodi. Kodi ya mbunge inakusanywa na ofisi ya bunge au wizara ya fedha (sina uhakika nani analipa mishahara ya wabunge) na ndio wao wanaiwakilisha serikalini. Ambao hawajawahi kulipa kodi ni wafanyakazi wa CHADEMA. Dr. Slaa alikuwa hajalipa hiki kipindi cha hapa mwishoni ambacho mshahara wake sasa unalipwa na CHADEMA.
Hakutaja chanzo kwa sababu chanzo cha hii habari ni kutoka gazeti la uhuru, gazeti ambalo thamani yake ni
chini ya toilet na linaendeshwa kwa ruzuku asilimia 90% kwani hakuna mtu mwenye busara anayesoma gazeti la uhuru.
Upi ni mpuuzi zaidi? chama kilichoko Ikulu lakini hakikusanyi kodi ya kuendesha serikali yake au chama kinachotaka kwenda lkulu lakini hakilipi kodi??chama kinachotaka kwenda ikulu hakilipi kodi? halafu wanataka wapewe dhamana waongoze taifa hili! wapuuzi!!!
Nyie watu mbona ni waajabu hivi. Kisa chadema wameambiwa walipe kodi imekuwa nongwa. ingeambiwa cuf, tlp au ccm ungeona jinsi TRA inavyosifiwa. lakini chadema no, ni kupinga kila kitu. Narudia kusema nyinyi ni watu wa ajabu sijapata kuona kwenye hii dunia.
chadema lipeni kodi. pia TRA nendeni kaangalieni maeneo mengine yanayosemwasemwa kuwa na loophole za ukwepaji wa kodi kama mlivyoziba hii ya chadema.
eeeh, siasa bwana??!!
hivi kwenye vyama vingine hali ikoje? katika vyama takriban 18 vilivyosajiliwa ni chadema tu ndio walikuwa "wakorofi" kwenye masualal ya kodi? hata hivyo wawe makini kama haya madai ni ya kweli na ya haki kwani harakati zao zina gharama sana na hii ni mojawapo
wanaotakiwa kulipa kodi hii inayoongelewa (PAYEE) ni wafanyakazi wala si chama au taasisi! Hapo ndo tunapopotoshana....Anayelipa kodi ni mwajiliwa na si mwajili. Sasa mbona wanaituhumu chadema wakati wao(CHADEMA) ni waajili tu?
Monday, 08 August 2011
NA HAMIS SHIMYE, Gazeti la Uhuru
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeitoza faini ya sh. milioni 100 CHADEMA, baada ya kubainika inakwepa kodi tangu ilipoanzishwa mwaka 1992. TRA pia imeanza kukata kodi mshahara wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa na watumishi wengine wa CHADEMA.
Habari za kuaminika kutoka ndani TRA zilisema ulipaji faini unaanza mara moja, baada ya uchunguzi kukamilika na kuonyesha chama hicho hakilipi kodi.
"Tumemaliza uchunguzi na kubaini CHADEMA hailipi kodi ya mishahara ya kila mwezi ya watumishi wake tangu ilipoanzishwa,'' kilisema chanzo chetu cha habari.
Imeelezwa kuwa, CHADEMA imekiuka sheria na kanuni za ulipaji kodi, zinazotaka mtu, kampuni au taasisi yoyote kulipa kodi TRA.
"Ijapokuwa tangu ilipoanzishwa ilikuwa hailipi kodi, katika uchunguzi tulipata taarifa za kuanzia mwaka 2000 hadi sasa zinazoonyesha hailipi kodi,'' kilisema chanzo hicho.
Kutokana na hilo, chama hicho kinapaswa kulipa faini ya sh. milioni 100 na kimeamriwa kulipa kodi ya mishahara ya watumishi wake kuanzia mwezi uliopita.
Chanzo hicho kilisema CHADEMA imeiandika barua TRA ikidai wanacholipana ni posho na si mishahara.
Hata hivyo, sheria ya kodi inaeleza kiwango chochote cha posho kinachozidi kima cha chini cha mshahara kinapaswa kukatwa kodi.
Watendaji ambao TRA imeanza kuwakata kodi ni Dk. Slaa, ambaye analipwa mshahara wa zaidi ya milioni 7.4, fedha ambazo ni nyingi kuliko mshahara wa mbunge.
Mshahara huo unatokana na mapendekezo ya Azimio la Kamati Kuu ya chama hicho iliyokutana Januari 29 na 30, mwaka huu, mjini Dar es Salaam, ambapo mshahara huo umegawanya katika sehemu sita.
Sehemu hizo ni posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi, ambapo mshahara wa mwezi ni sh. 2,300,000.
Fedha za mafuta ni sh. sh. 1,387,000 kwa wastani wa lita 750 kwa mwezi, huku fedha za majukumu zikiwa sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. milioni moja.
Posho kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa mshahara kama huo.
Last Updated ( Monday, 08 August 2011 19:34 )
CHADEMA yakiri kukwepa kodi
Tuesday, 09 August 2011 20:09
NA SULEIMAN JONGO
KATIBU Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibroad Slaa, amekiri kuwa chama chake kimetozwa faini na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Hatua hiyo imetokana na chama hicho kudaiwa kukwepa kulipa kodi za mishahara na posho za watumishi wake kwa miaka kadhaa. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, jana, Dk. Slaa alisema TRA imeitoza CHADEMA faini ya sh. milioni 94. "Ni kweli tumepigwa faini na TRA kulipa sh. milioni 94, kwa kutolipa mishahara ya watumishi wetu.
Tutalifikisha hilo katika vikao vya juu na tutalipa tu," alisema Dk. Slaa.
Alisema kuwa tayari wamepokea barua kutoka TRA inayowataka kulipa sh. milioni 94, kama adhabu ya kutolipa kodi za watumishi wake. Hata hivyo, katika hali ya kushangaza Dk. Slaa alisema kuwa CHADEMA haijalipa kodi tangu kuanzishwa mwaka 1992, haijalipa kodi za watumishi wake kwa kutofahamu.
Pia, alisema kuwa walikuwa hawafahamu mabadiliko ya Sheria za Kodi, ambayo huko nyuma mishahara ya watumishi inayotokana na fedha za ruzuku ya serikali.
Wakati huo huo, CHADEMA kimeshauri kutazamwa upya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) baada ya kukosa mwelekeo katika kutimiza majuku yake.
Dk. Slaa alisema mkanganyiko katika mambo mbalimbali yanayotokea kwenye sekta ya nishati na maji yanatokana na ulegevu wa EWURA na kutotimiza majuku yake ipasavyo.
Alisema lengo la kuanzishwa EWURA ni kusimamia na kuratibu huduma mbalimbali zinzohusiana na maji na nishati ya mafuta na gesi, jambo ambalo linafanya kuwepo na haja ya kuitazama upya EWURA.
Kwa mara ya kwanza habari za CHADEMA kukwepa kodi ziliibuliwa na gazeti hili, ambapo baada ya TRA kufanya uchunguzi wake ilibaini ni kweli na sasa itavuna mamilioni ya shilingi kama adhabu, ambazo zitasaidia kutoa huduma kwa jamii.
wewe ni chapati kwelikweli tena ya kuchoma.Hata nyinyi chadema wezi tu,haijalishi kama wengine wamelipa au la,kwani chadema nyinyi nani bwana,nyie mnataka mkondo wa usfisadi uje uchagani tena,baada ya kikwete kuhamisha mtandao wenu,hata nyie ni mafisadi na wengine ni majambazi
mheshimiwa mtoa hoja, unajua mshahara wa mbunge????kwanza source ya habari ni uhuru of all news papers?du umeishiwa! let them do what they want ili wadhoofishe mkombozi wa watanzania!tushasema, chadema ikibidi tutawachangia sisi wananchi ili kukamilisha ndoto za watanzania ambao wameteseka ndani ya nchi yao nzuri cha ajabu hata somalia wana nafuu ambao wanategemea mchanga wa kutengeneza vioo!
Hawa TRA ile consultancy fee ya Idd Simba (Milion 285) kutoka Simon group wamechukua kodi? Vipi CCM,CUF, TLP wamewadai ngapi????????