Shocking Truth Kutoka Loliondo

Muhimbili national hospital wagonjwa wengi wanakufa nenda Mwananyamala hali ni hiyohiyo bila kusahau Temeke hospital
lakini hakuna anayehoji dawa na tiiba zinazotelewa na hospitali hizo kama zinafaa au la.Siri ya kufa anaye Mungu si mwanadamu napendekeza tumwache babu afanye kazi yake kwa binadamu anayependa na kuamini tiba yake.
 
Babu alichokifanya ni kama kilichowahi simuliwa na Abunuasi:…
"Jamaa(Abunuwasi) aliwaambia watu kuwa kwake kuna malaika waje kumuona kwa hela ila aliye na dhambi hatamuona …watu wakamiminika kwa wingi sana ikawa kila anayetoka ndani anasema nimemuona nimemuona nimemuona ili asionekane ana dhambi…"
Sasa hadith hii babu aliisoma na akaielewa akanza kuwafanyia watanzania na ndio maana kila aliyekuwa anakunywa alijifanya kutoa ushuhuda kuwa amepona amepona amepona, na kwa sababu hiyo walilazimika kuacha dawa zao kumbe ile danganya toto matokeo yake ni hayo na bado tutasikia mengi, ipo siku tutaambiwa wote waliokunywa watakufa in a short period, hapo ndio babu atakamatwa.
 
 


Next time try your level best to be objective and rational! After all who told you that babu anatoa dawa ya kuzui kifo.
 

Akigeuza kibao kuwa wote waliokuja kunywa dawa watakufa kwani kama wangekuwa na imani wangemwamini Mungu katika neno lake kuwa kwakupigwa kwake 'Yesu tumepona' so yeye kama mchungaji aliambiwa kudhihirisha kuwa Yesu ndiyo njia kweli na uzima kwa matendo na ameoteshwa sasa hao wote walioenda ndiyo wapinga kristo na lazima wafe amasivyo wakate shauri na kuokoka; utaona kizaazaa kitakachotokea hapo!

Our God is a loving and abundant in grace, He is gentle and meek. Hatumii desperation ya watu kuonyesha nguvu zake mara zote hutoa majibu yanayo kidhi haja ya moyo. Akikupa divine visitation anaponya mwili roho na nafsi yako kiasi kwamba kunakuwa hakuna swali bali majibu yanajidhihirisha yenyewe. Ndiyo maana anatoa adhabu kubwa kwa wale wote wanaotumia jina lake vibaya kama ambavyo dola inavyoweza mwajibisha tapeli anayetumia madaraka ambayo hana katika kusaidia watu. Mfano kutoa cheti cha kugushi hata kama nia ilikuwa kumsaidia mhusika kupata kazi ama nafasi ya kuendelea kusoma; dola haitaona huruma eti kwasababu huyo alikuwa na dhamira njema.

Ole kwa Babu kama amegushi madaraka na kutoa kitu ambacho dola ya mbinguni haijakibariki maana hukumu yake wala si mpaka afe bali itakuwa hapa hapa duniani. Anaheri kama anafanya hilo bila yeye kujitambua maana Mungu pia ni mwenye rehema na hurehemu maelfu kwa maelfu. Bado nasisitiza huo uponyaji wa babu si kwa jina la Yesu lakini hii haimaanishi kuwa si kwa jina la Mungu wa huyo Babu!
 
Hii hadhithi yako mbona waitowa kila siku? Umeishiwa au hujui kutunga nyingine? Ndiyo huwa anaitumia mchungaji Kakobe au Kulola?

Jitahidi basi ulete nyingine maana hii tumeshaisikia sana hapa JF kutoka kwako. Poor you!!!
 

Usamehewe kwa hili maana hujui ulitendalo.
 
Hii hadhithi yako mbona waitowa kila siku? Umeishiwa au hujui kutunga nyingine? Ndiyo huwa anaitumia mchungaji Kakobe au Kulola?

Jitahidi basi ulete nyingine maana hii tumeshaisikia sana hapa JF kutoka kwako. Poor you!!!

Du! msg imekugonga mpaka umejihisi kama kila siku naipost?!!! ama kweli hii msg kiboko.Its my 1st T, pole sana kama nawewe ulitoa ushuhuda kuwa " Nimepona! Nimepona! Nimepona! ukiongea kwa mshangao, sasa hivo ndiyo utakavyokuwa ukijishangaa kidogo kidogo mpaka ujisifu ujinga kwa kuamini nguvu za giza.
 
Huyu babu ni mganga wa kienyeji kama waganga wengine ila tu kinachombeba sana ni kuwa askofu mstaafu,hiki ndicho kinawaingiza wengi mkenge.
Shemeji yangu mama yake mzazi amekufa mara tu baada ya kutoka Loli na mwingine mkazi wa manzese mkunguni kafia kwenye gari akitikea Loli kwa babu.Sasa kama mgonjwa huponywa kwa imani yake kwa nini mpaka Loli kwa nini asijifungie chumbani usiku na kumuomba Mungu amponye maradhi yanayomsumbua kwani kwa Mungu hakuna linaloshindikana.
Na kama babu anaponya kwa imani YESU aliponyesha watu kwa neno na hakuwahi kuchemsha dawa akawapa wagonjwa Iweje mchungaji awape watu mizizi kisha aseme anaponya kwa imani.Hana tofauti na DR NDODI.
 
Mwanzoni ilianza kwa mbwembwe nyingi kwamba [B]"yeyote atakaye fika kwa babu hatakufa." [/B]Remember?
Fool me once, shame on you. Fool me twice, shame on me ! Wise Quotes

Jesus is Lord

Hapo pekundu hapo!!
Kuna atakayekwepa mauti jamani? Upuuzi ulioje na ujinga ulioje kuamini kuwa ukinywa kikombe hutakufa!!
KILA NAFSI ITAONJA UMAUTI....
AMA KWELI NABII HOSEA ALIVYOSEMA " WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA" hakukosea hata kidogo.

Wajinga na waliokosa maarifa tu ndio wanaoweza kuamini kuwa ukinywa dawa hii hutakufa.
 
Kwanini Babu tu kila siku...mbona hampingi vikombe vingine vinavyoibuka mikoa mbalimbali.....Tupeni basi na ushuhuda wa waumini mliowaponya nyie waasi wa Babu. Najua hamna na ndio maana hata waumini wenu wameamua kutimkia Loliondo kwa Babu kugonga kikombe.
 
Si useme tu kuwa ni wewe ulyepga kikombe heshma ya ndoa ikarud.. Hongera kwa kupona..... RIP wote walio2tangulia.
 

Du pole sana,mpe pole mzee wako. Vipi kwa sasa unaweza toa ushuhuda gani baada ya kugundua kuwa babu dawa yake anayomsingizia Mungu eti kamuotesha si dawa? Ama kweli watanzania wengi washirikina, ivi kweli Mungu anaweza kukupatia dawa ya Uongo? Halafu cha ajabu babu anasema ni dawa ya kiimani zaidi halafu anatafutia upenyo wa kuchomokea eti watu wakapime hospitalini! hiyo siitakuwa tayari ni kisayansi tayari. kama ni dawa ya kiimani ibaki kuwa ya kiimani na mtu baada ya kuinywa kwa ugonjwa wa kisukari na abakie na imani yake kuwa kapona.Serikali na baadhi ya Makanisa yametia aibu kubwa taifa letu kwa kushabikia Ushirikina wa waziwazi
 
Usamehewe kwa hili maana hujui ulitendalo.

Mama,mie nahisi asiyejua alitendalo ni mtu amabaye mpaka leo anahendekeza nguvu za giza kama wewe, Una macho wala huoni, una masikio wala husikii, na una akili lakini hazifanyi kazi. Media zilimtangaza sana babu na kwa title yake ya uchungaji mpaka makanisa yamejikuta yakipigia debe ushirikina, sasa wote mnaoamini ktk ushirikina mtaaibika mwaka mzima, inabidi mtafute cd nyingine ya kulisafisha kanisa. Takwimu zinaonesha kuwa wengi wa waliokunywa mpaka dakika hii wapo hoi hasa hawa wa sukari na ngoma
 

Jamani faith ya kikombe cha babu? Acheni kutumia maandiko vibaya! "My people are destroyed for lack of knowledge" and this exactly it! Guys Mungu anajali zaidi kuponya roho za watu na wala siyo kuponya mwili. Kama Babu Ambi angekuwa anaponya kwa nguvu za Mungu angewatangazia pia hao wanaoenda kupata uponyaji wapate pia na wokovu maana huo sasa ndiyo uponyaji wa roho ambao Mungu wa Ibrahimu,Isaka na Yakobo anautaka. Haijalishi wewe kufa leo kwa ugonjwa cha msingi na kikubwa kwa Mungu ni roho yako iponywe!

Mungu wa mbinguni aendelea kufunua yote ili watu waijue kweli kupitia kadhia hii ya Loliondo!
 
Niliwaambia hapa mapema ndugu zangu waTanzania. Kwamba hili la Loliondo ni Diable, sikueleweka na ikaonekana kwamba nampiga vita "babu yao watu" sikuchoka nikawaletea tafiti mbalimbali na matumizi ya dawa hiyo lakini ikaonekana bado sijasema la maana!
Nasikitika kufa kwa watanzania wenzetu lakini husema:
NI HERI WAKAFA WAJINGA ELFU MOJA KULIKO MTAALAMU MMOJA! Hivyo basi huu ni MCHUJO!
 
Ww nyerere wacha kusoma magazeti ya shigongo huyu anafanya biashara, watchout. Siku nyingine shuhudia mwenyewe usiambiwe.
 
Sasa jamani, Mungu yupi anakuponya halafu anasema endelea kutumia dawa zako, ukiacha unakufa???????
....wa babu wa loliondo... na wale wa wale mababu na mabibi wengine!!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…