Hawa wanao mtetea babu (a.k.a Kinjeketile Ngwale) wa Rolly, wana sera kama za serikali ya Marekani...! Walipotaka kuivamia Iraq, walidai kuwa Sadam alishiriki kuanguza Twin Tower, hii sababu haikukubalika, mara wakadai kuwa Sadam Hussein ana siraha za maangamizi, walipozikosa wakaja na msemo mwingine kuwa wanamuondoa dikteta, walipoona kuwa bado jamaa anaungwa mkono wakaja na msemo mwingine kuwa wanapeleka demokrasia ya kweli kwa Wairaq...! Matokeo yake wao ndio wameiangamiza nchi ya watu...! Sawa na hao wanao mtetea huyu babu, kila kukicha wana kuja sera na mpya...!
Watu sasa wanaonekana wakifa wengi tunasikia jinsi wanavyo mtetea...! Oooh babu hazuii kifo, ndio tunajuwa kuwa hakuna mtu mwenye uwezo wa kuzuiya vifo... ndio hata hao mitume tunao waamini kwenye dini zetu, ziwe za jadi au hizi ambazo tuna ziita za kimapokeo, hawakuwa na uwezo wa kuzuiya watu wasife... Lakini kama vifo vinatokana na uzembe na ujinga wa makusudi kwa kuacha kula dawa zenye kukuongezea uhai, mnataka tuwaeleweje? Sasa tunasikia tena kuwa watu wasiache kula dawa zao, japokuwa wamepata kunywa dawa za Kinjeketile Ngwale wa karne hii ya ishirini na mbili... Kulikoni tena?
Hao waliokwisha kunywa dawa mpaka leo hatusikii wakisema kuwa wamekwenda kupima... Wanaogopa kitu gani...!? Utawasikia wakijisifia kuwa wamepona kwa kujiangalia kwenye kioo...! Na hali maradhi yanawatafuna ndani kwa ndani...! Mwisho hao watetezi watakuja na utetezi mpya kuwa wale wote ambao hawakupona hawana imani ndio maana dawa ya babu Kinjeketile haikufanyakazi...! Hivi hao waathirika waliozidiwa baada ya kuto endelea na dawa zao za mahospitalini, watajisikiaje watakapo simangwa kwa kushutumiwa kuwa hawakupona kwa kuwa hawana imani...! Je hamuoni ni kuwadhidishia maradhi zaidi?
Hivi anayetakiwa kuwa na imani hapa ni nani mgonjwa au babu kinje...! Yeye si ndiye aliye dai kuwa kaoteshwa na mungu na dawa yake inaponyesha maradhi yote...!? Hivi Mwenyezi Mungu anapoleta Neema huwa anachaguwa wa kumpa? Au huwa anawapa hata wale wasio muamini?
Hivi ni kweli uwezi kupona mpaka huwe na imani ...!? Inaingia akilini kweli? Mbona tunasoma kwenye maandiko ya biblia kuwa kuna watu waliponywa na wala hawakuwa na hiyo imani...! Na wengine walifufuliwa...! Je wale walioponywa na kufufuliwa na Nabii Elisha...! Walikuwa na imani? tena wengine walifufuka kwa kugusa mifupa ya manabii tu.
Jamani tuwache kushabikia vitu ambavyo haviwezekani kwenye karne hii... karne ambayo mwenyezi Mungu ametujaalia utaalam wa kutengeneza madawa ya kutibu maradhi mbali mbali...! Kinacho wafanya watu wasitumie hiyo miujiza ya kunywa dawa mahospitalini ni kitu gani kama si ulimbukeni na kutafuta njia za mkato ni nini...!? Kwani hizo dawa za mahospitalini hazina baraka za Mwenyezi Mungu!? Hivi tunamwambia nini Mwenyezi Mungu siku ya hukumu... Na hali ametupa akili na tunashindwa kuitumia... Hivi ni neema gani zaidi ya kutumia akili zako na kutambua kuwa hapo Lolly hakuna uponyaji zaidi ya kuwapumbaza watu kwa kivuli cha imani!?
Mara nyingi ni vigumu sana kushindana na wajinga, watakushinda tu...! Watakusumbua na hoja zao za kijinga na kukushusha mpaka ufikie level yao...!
Kisha watajiona kuwa wao ni mahodari na kuanza kujisifia na hali wanaona kuwa ujinga wao umepelekea maangamizi ya ndugu, marafiki na jamaa zao wenyewe...! Ukiwauliza haya mambo yamekuwaje... Hawakosi hoja hata siku moja...! Utawasikia wakisema "Aaah wale, wale wamekosa imani ndio maana hawakupona, unatakiwa umkili bwana kwanza..." Jamani hivi hakuna viongozi wa dini ambao wamefariki kwa maradhi ya kutibika, lakini wakafariki? Je hawakuwa na imani!? Msije sema kuwa hatukuwaonya na kuwatahadharisha na hatari iliyoko mbele yenu...! Sisi tunawapenda zaidi ya hao ambao wanao wapeleka kwenye mdomo wa mauti, uko mnakoenda hakuna uponyaji, bali kuna mauwaji...!