Gaijin Nipo mwalimu..... Tena nipo Jana na leo. Alafu nahisi kama nimekumiso. Fanya kuni ublock huko kwenye PM yako japo kwa dk 5. :biggrin:
he he he he, niliishi gongo la mbagala wakanilipua, nikahamia gongo la mboto nako wakalipua, sembuse hapa mabomu ya maneno?
Naona hoja zimeisha ... hii thread ssio official na mimi sijafanya research yoyote hapo. Umeona unajikanyaga sasa umehamia kwenye validity ya thread badala ya ethic.
Imaginations ... Nani kakataa hizo sample zako? Hata imi mbona nilisema hivi mwanzoni? Soma post za nyuma utaona sehemu niliyopost .
Kama umeangalia vizuri mtoa mada haja taja kituo hila kaleta takwimu! Swala la umuhimu wa usiri katika mapambano haya nalifahamu sana tena sana. Lakini wewe unafikiri tofauti! Sababu mtoa mada haja taja kituo bado amewasitiri! Lab tech ajamwambia mtoa mada peke yake bali baada ya kupima hizo takwimu kuna mahali ana zipeleka na kuna mtu ana mpatia kuziandaa je bado ni kusitiri?
Pengine tusibishane na kupoteza nguvu kwenye hili tujadili datta hizo na mstakabali wa afya zetu pia!
Tusitumie muda mwingi kuhukumu mtu!
Pia na mshukuru mleta uzi ili watu wajue kilichopo duniani.
Breach of rules of confidentiality is not weighed on the balance of probabilities gentlemen, it needs a proof holding truth watertight, beyond reasonable doubt. So the question whether you were there at that particular material day, on the due time, does not suffice a breach! Unless otherwise you have been directly mentioned.
Ni sawa na mahakama kusema kuwa, kila mwaka tunapokea mashauri 300 may be ya wanawake walioolewa kubakwa na waume zao.
Maambukizi huwa hayako evenly distributed kwa nchi nzima
Kuna maeneo yana maambukizi makubwa, mengine kidogo
Niliwahi fanya kazi na mradi wa vijana wa UKIMWI, kuna sehemu zilikuwa zinatisha kabisa, hata wiki inapita bila kuhudumia mwenzi sababu ya hofu, na sehemu zingine maambukizi yalikuwa chini sana.
Sikuwa lab technician, lakini niliweza jua kati ya respondent wetu wapi wamekutwa na VVU, imagine walikuwa vijana kati ya miaka 14 - 26, na frequency kubwa ya umri ilikuwa kwenye group la 15-20.
Hakuna confidentiality kihivyo.
Ni sawa kabisa kusema...
Hizi ni statistics..
na kwa mujibu wa Professional Ethics- Pale ambapo data unatoa taarifa kwa manufaa ya public... inaruhusiwa..
we call it Duty to Public..
Mnaacha kutafakari ukweli wa jambo mnajadili mambo ya validity..Ndio maana watu huwa wanaangamia kwa kukosa maarifa...
Chukua hatua..
Takwimu unazijua wewe?
Huyu kaleta umbea hapa, si takwimu. Big difference.
Ukweli wa mambo unataka kufikiri, hautaki simplification isiyo na tija. Ukitaka simplifications unaweza kukataa kwamba dunia si tufe kwa sababu tu baraza lako liko bapa.
Unaweza kuona vi Lab Technician kufuja dhamana ya kazi ni kuzuri, kumbe matokeo yake ni kukosesha shughuli nzima ya upimaji imani kwa wananchi.
Watu wanapata virusi vya UKIMWI, hawaamini upimaji, hawajijui kama wanao, wanaendelea kuambukizana.
Unachofanya hapa ni justification ambayo ina systemic unintended consequences.
Kiranga, nakubaliana na wewe, hakuna ethics kabisa.
Ni jambo si la kufurahisha lakini ni ukweli.
Huo mfano niliotoa, haikutakiwa kwa watu wa lab kudisclose id na majibu ya wale repondent lakini yalikuwa wazi.
Kuna mtu mmoja anajulikana kidogo huku nakoishi, alishasema yeye kupima VVU nchini labda awe hajitambui, sababu hiyo hiyo ya confidentiality haipo.
Ukimwi Upo sana hata madaktare wakikupima na wakaona hauna wanashangaa imekuwaje hauna? inasikitisha Tulizana tupo wangapi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Tunachotaka ni ku uphold professional ethics.
Hata kama unataka kutoa data za mtaa mmoja tu ufanye yafuatayo.
1. Uwaambie wanaopima kwamba utawa identify kwa mtaa, ili mtu asije kupima halafu data zake zikatumiwa asivyotaka.
2. Due process ya formal verification kuhakiki false positinves, margins of errors, methodology etc inafanywa.
3. Matokeo yanakuwa public, kwenye magazeti, bulletins za mtaa etc, accessible to all.
Then hapo kunakuwa na kitu formal kilicho na consent ya wapimwaji, kinachoelimisha jamii nzima bila favoritism wala kuwa prone to human nature ya Lab Tech anayeweza kuanza kutaja majina akibanwa na ndugu yake. Hapo hata Lab Tech akiulizwa anasema tushachapa figures angalia bulletin fulani.
Hizi habari za Lab Tech kuanza kuongelea mambo ya kazini over dinner ndo mwanzo wa "Na yule mama wa mtaa wapili pale aliyefiwa na mumewe mwaka jana vipi? si walisema TB? Lakini mbona anakonda siku hizi?"
Na binadamu alivyo na nature ya kujifanya mzuri kwa ndugu zake, ukichanganya na sense of power inayokuja na info, kirahisi tu mtu anaingia mkenge "Pale msiguse ndugu zangu".
Tayari usha compromise confidentiality, ukishtuka neno lishatoka.