Shivji: Tanganyika Siijui, Siihitaji

Shivji: Tanganyika Siijui, Siihitaji

Character X

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
331
Reaction score
382
Kwakuwa Nilisha sema na kuandika Mawazo yangu juu ya Muundo Wa Muungano wetu Mara kadha na hasa kuhusu dhana ya utanganyika.

ninaomba kuweka Hapa Sehemu Kati ya yale aliyo ya sema Prof. Idea Shivji wakati wa kongamano la vijana hivi majuzi. Msisitizo Zaidi Hasa kwenye Suala la UTANGANYIKA!!

Nanukuu,

"Juu ya hilo la Utanganyika, ningependa kuongeza maneno machache hasa kwa faida ya vijana wetu. Nimeshangaa kidogo kwamba hata mzee na mwanazuoni mwenzangu Prof. Mpangala ametumia msamiati wa ‘Utaifa wa Tanganyika’ bila kudadisi kihistoria ‘Utaifa wa Tanganyika’.

Kwa muhtasari tu, kabla ya vita vya kwanza, hatukuwa na Tanganyika. Tulikuwa na ‘German East Africa’ ambayo eneo lake lilijumuisha Burundi, Rwanda na eneo hilo la ‘Tanganyika’ chini ya himaya ya ubeberu wa Wajerumani. Baada ya Ujerumani kushindwa katika vita, Rwanda na Burundi ziligawiwa kwa Ubelgiji na Tanganyika kwa Uingereza. Waingereza ndipo wakaunda neno hili ‘Tanganyika’ na iliitwa ‘Tanganyika Territory’, yaani, bustani ya wakoloni, siyo taifa.Mababu zetu waliopigania uhuru walijikita kwenye dhana ya Utaifa wa Kiafrika, kama alivyoeleza vizuri tu Profesa Mpangala. Vyama vya wananchi, kutoka TAA (Tanganyika African Association) mpaka TANU (Tanganyika African National Union), viliweka msisitizo kwenye ‘African’, Uafrika wao. Iliwabidi kuweka neno Tanganyika kwa sababu tu ndilo lililokuwa eneo la utawala wa wakoloni.Tulipopata uhuru mnamo Desemba 1961, hatukuwa taifa kwa sababu mkuu wa nchi bado alikuwa Malkia. Mwezi wa Novemba 1962 ndipo tukawa Jamhuri ya Tanganyika wakati Mwalimu alipochaguliwa kuwa Rais. Na Mwalimu tangu mwanzo alisistiza kwamba sisi hatukuwa taifa bali mkusanyiko wa makabila na lilikuwa jukumu la serikali huru kujenga utaifa (nation-building).

Lakini Mwalimu hakupata muda wa kutosha kujenga utaifa wa Tanganyika kwa sababu mwezi Aprili 1964, yaani baada ya miezi 14 tu, tukaungana na Zanzibar kuwa Tanzania. Na kwa takriban nusu karne tumekuwa tunajenga Utaifa wa Tanzania.

Sasa hii dhana ya Utaifa wa Tanganyika, au Utanganyika, unatoka wapi? Na mantiki na historia yake ni ipi?Ningependa kujua hapa tulipo ni vijana wangapi kati yenu mlizaliwa kama Watanganyika. Nyoosheni mikono juu. Nyinyi wote mlizaliwa mkiwa Watanzania, utaifa wenu ni Utanzania; utambulisho wenu ni Utanzania; mnajitambua kama Watanzania na mnatambuliwa na wengine kama Watanzania.Ukweli ni kwamba mking’ang’ania Utanganyika wenu, ambao wala hamjui kama mtakuwa mnavunja taifa, mtakuwa mnatumikia maslahi na matakwa ya mabeberu na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka. Na Utanganyika wenu hautadumu kwa sababu mtaanza kudai sasa Jamhuri ya Makonde na Jamhuri ya Sukuma! Mtakuwa vipande vipande. Hivi siyo vitisho; kuna mifano hai mbele yetu. Somalia imesambaratika, Libya pia, Sudan, Afrika ya Kati, na nchi nyingine nje ya Afrika – Afghanistan, Pakistan, Syria, Iraq bila kutaja nchi za Ulaya"

- Prof. Issa Shivji 2014.

Comrades, maneno haya ya mwanazuoni huyu nikama ameyasikia kutoka kwangu ama kuyasoma katika kuta zangu katika mitandao mbali mbali,. Sijilinganishi naye., hapana hata kidogo. Ila ninachosema nikwamba mtu yeyote mwenye nia njema na fikira tulivu anaweza kung'amua nia hasa ya wale wanaotupandikiza hisia za utanganyika na uzanzibari. Walafi wamadaraka!!

Nilisha sema na ninasema tena hapa Tanganyika Siijui, na wala Siihitaji.!!

Comrades ninashukuru sana.
 
Shivji sio???? Jina lake halipo ktk kamusi ya majina ya kitanganyika anaongea nini sasa!?
 
mtanganyika pekee ndio anaweza ijua Tanganyika. Si yeyote mwingine mwenye double identity!
 
Suala la msingi sio historia, bali tueleze muugano wa nchi 2 serikali 2 ni wa aina gani? usitumie nguvu wala vitisho tunataka kitu kinachoingia masikioni hata mjinga akaelewa!
Hivi kumbe Mwenyezi akiamua kuondoa ufahamu hata usome kiasi gani hauelrewi?
 
Nimeuliza hapa, ni yupi Kati yetu anaeweza kujifisia akisema yeye ni mtanganyika zaidi kuliko alivyokuwa Mwalimu Nyerere??! Ni nani?
 
Ninakumbuka ya Amil Jamal. Hawa wenzetu wana uraia pacha. Jamal alikuwa Waziri wakati wa Nyerere na pia Mbunge wa Morogoro. Baada ya kufariki amezikwa Canada kama sijakosea! Hivyo hivyo kwa huyu Bwana unaweza kukuta naye ni raia wa Canada! Kila kitu kinawezekana katika nchi hii.
 
Kama tuwamoja kwanini mkerewe aishi kwa masharti Zanzibar na mzanzibari aishi na aruhusiwe kumiliki ardhi huku bara? Shivji atujibu hili pia
 
To me, nadhani hoja haijajitosheleza. Tanzania ni muungano wa Zanzibar na Tanganyika whichi means kuna Tanganyika na Zanzibar zilizounganishwa.
Labda atoe darasa juu ya muungano kwanza tujue Tanganyika ilisimama vipi katika muungano.
 
hizo ni porojo ambazo hazistahili kutolewa na mssomi wa kiwango cha uprofesa, kwa upeo huu hata mimi sina phd namzidi kwambali huyo msomi uchwara.

kwa nchi zilizoendelea pro, shivji inabidi avuliwe "phd na uprofesa" wake kwani ameyakana maandiko yake yaliyo mpa hizo academic status

sisi watu wa kawaida tunategemea drs na professors ni problem solvers huku tz ni problem creators,

point siyo jina la Tanganyika, ni jinsi gani tulalijenga taifa moja regadless ya mfumo wa serikali ngapi, wengine wameuguza vichwa wametoa pendekezo la serikali tatu na wametoa sabau za msingi

tulitegemea drs na professors waende mbali zaidi watupe solution hapa tulipokwama, ili huko mbeleni yasiwepo malalamiko, unapoona drs na professors nao wanalia lia utaashangaa sana,

majigambo meee...ngi, toeni solution, mbona sisi kwenye taaluma zetu tunatoa solution ya matatizo,

kipimo sahihi cha drs na professors wetu kwa sasa kingelikuwa ni kutoa solution ya muungano,
kulilia serikali mbili na kuiponda tanganyika bila kutuambia ni jinsi gani tutaondoka hapa tulio ni upumbavu,
kwa jinsi nilivvyo wadharau hawa madr na maprof wa nguine, naanza kuamini kwamba tulikuwa sahiihi zama zile tukiwa shule kwamba, hawa jamaa zetu degree zao ni laini mno, maneno murefu vitendo hakuna,
 
Prof.Shivji anapotosha,
Tanganyika iliungana na Zanzibar ikatokea Tanzania.
Baada ya miaka kadha, Wazanzibar hawataki kujitambulisha kama Watanzania bali ni Wazanzibari.Sisi wa Tanganyika tunapata wapi uhalali wa kujiita Watanzania wakati partner katika muungano anajitoa?
Mh.Pinda aliwahi kutamka Bungeni Tanzania Visiwani,Wazanzibari wakaja juu,leo Sisi Watanganyika tunawezaje kuwa Watanzania kama mwenza katika muungano anajitoa?
 
Hivi Wadau Naomba Kuuliza, Si Wengine Elimu Zenu Za Kayumba Hizi! Sijui Tunapotoshwa, Kwa Vile Waalimu Wenyewe Mhhhhh!! Hivi Ule Mkutano Wa Berlin 1880 -1884 Ulikuwa Na Lengo Gani?? Coz Sijaelewa Kwa Neno Tanganyika, Lilianza Wkt Wa Uingereza Au Ujerumani??
 
Inaelekea Shivji anafahamu sana historia ya Tanganyinka lakini hajadadavua vizuri jina hili TANGA-NYIKA lilitoka wapi? ni kitu gani kiliitwa (Tanga nyika) sawa ilikuwa Bustani ya wakoloni ndo tusijue neno asili yake ni wapi? je ni maneno mawili kama nilivyoyaandika au ni neno moja? akimaliza kutuambia Tanga Nyika atuambie na Zanzibari nalo lilitoka wapi( maana kule kuna Unguja na Pemba)
 
Kifupi Twaita Tanganyika Yetu!! Wenyewe Tanganyika HALISI.!! Sio Mtanganyika Wa Kuungaunga!!!
 
Naanza kupata sababu kwa nini Rev. Mtikila anawaita 'MA---------'
 
Ninakumbuka ya Amil Jamal. Hawa wenzetu wana uraia pacha. Jamal alikuwa Waziri wakati wa Nyerere na pia Mbunge wa Morogoro. Baada ya kufariki amezikwa Canada kama sijakosea! Hivyo hivyo kwa huyu Bwana unaweza kukuta naye ni raia wa Canada! Kila kitu kinawezekana katika nchi hii.

Kwa hiyo Balali kuzikwa Marekani ndio tuseme alikuwa na ngozi ya ki-"Shivji?" Nilishasema huu utanganyika hautaishia kuwabagua tu Wazanzibari, bali tutaanza kubaguana wenyewe kwa wenyewe! Mungu atuepushie mbali na huu msukule wa Utanganyika!
 
Nimeuliza hapa, ni yupi Kati yetu anaeweza kujifisia akisema yeye ni mtanganyika zaidi kuliko alivyokuwa Mwalimu Nyerere??! Ni nani?

Ili twende sawa pia tueleze nani ni Mtanzania zaidi ya Nyerere??, kisha tuambie ilipatikanaje hiyo tanzania halafu tufafanulie ikiwa zanzibar ni nchi kama mabadiliko ya katiba yao ya mwaka 2010 yanavyosema yanatoa tafsiri gani kwa ustawi wa hiyo tanzania
 
Ok ok if that is the case, tuwe na serikali moja na sio mbili......!!!!!
 
Back
Top Bottom