Nimekuwa nikifuatilia mijadala mingi inayoendelea nchini kuhusu Utanganyika na Uzanzibar kiasi kwamba sasa mijadala hiyo imeingia kwenye Muungano wenyewe!
Madai ya mwanzo kabisa ilikuwa kutaka muundo wa Muungano wetu uwe wa Shirikisho (Federal Union) Serikali 3, badala ya huu uliopo wa NCHI moja (Unitary State) Serikali2 na walijenga hoja zao kwa kufuata mfumo wa Shirikisho iilihali huo sio mfumo wetu. Inawezekana hawakujua kwamba Muungano wetu wa mwaka 1964 haukuwa wa Shirikisho kama walivyo aminishwa.
Hata hivyo, binafsi nimekuwa nikipingana na mawazo yao nikiamini kwa dhati kabisa hsamira yao haikuwa njema, mwisho wa siku patakuwa hakuna Muungano kwa sababu madai ya Serikali 3 ni lugha ya kistaarabu au kiungwana iliyotumiwa Kuficha dhamira yao ya kweli. Na sasa hivi wamechoka kujificha nyuma ya pazia la Muungano.
Namshukuru Mwenyezi Mungu, kuwasikia sasa hivi wakifunguka wazi kanisa kwa madaha wakidai kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haukuwa Halali toka uliposainiwa mwaka 1964.
Tena baadhi viongozi wanasema wazi wazi kuwa Muungano ule Baraza la Malinduzi walilazimishwa kuukubali lakini haukupata ridhaa yao. Sijui hawa pia walikuwa katika Baraza lile Mpinduzi la kwanza lenhe wajumbe 29 ama nao walihadithiwa.
Kifupi, Haya ni matusi mazito sana kwa Taifa letu nanhasa katika jamii ambayo tumeishi zaidi ya miaka 60 tukiamini sisi wote ni Watanzania.
Kumbe nyuma ya pazia, kuna wale wanaodai Serikali 3 ndio wao wasoutambua Muungano.
Ukisikia Wazanzibar wanadai NCHI yao na Watanganyika wanadai NCHI yao. Muungano haramu hauwezi kuunda Serikali ya Shirikisho kwenye Muungano Haramu.
Kama hutuutambui Muungano, tunawezaje kuunda Serikali zozote ndani ya Muungano usotambuliwa? Kama hutuutambui Muungano wetu wala hauna ridhaa yetu, tunataka Serikali 3 za kitu gani?
Namshukuru Mungu wachawi wameanza kutua juu ya paa mchana kweupe. Na kibaya zaidi zile sifa za KiongoI tumtakae, alizosema Mwalimu mwaka 1995 kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Chama chake zimebakia kuwa hadithi nyingine ndani ya Kitabu.
Tuliombee taifa letu, aidha maneno ya Mwalimu yametimia, tunasubiri Utabiri wa Sheikh Yahya Hussein.
Masalaam