Shirika la Viwango Tanzania (TBS) yapania kuongeza thamani ya ubora wa viwango vya korosho na bidhaa zitokanazo na korosho wilayani Nachingwea

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS) YAPANIA KUONGEZA THAMANI YA UBORA WA VIWANGO VYA KOROSHO NA BIDHAA ZITOKANAZO NA KOROSHO WILAYANI NACHINGWEA

Na Mwandishi wetu Nachingwea

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) leo Tarehe 16 Septemba, 2021 wanatoa mafunzo kwa Wajasiriamali na Wasindikaji na wafungashaji wa korosho na bidhaa za korosho.

Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Rasmi na Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Nachingwea Bi. Lilian Mwaipungwa kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea.

Bi. Lilian ameipongeza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa maandalizi mazuri ya mafunzo na kuamua kutoa mafunzo hayo wilayani Nachingwea

"Natambua mafunzo haya yatakuwa ni nyenzo muhimu kwa Wajasiriamali hawa wapatao 40 wanakwenda kufanikisha malengo ya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa Kati kupitia Uwekezaji katika Viwanda na hivyo kuuza bidhaa zitokanazo na korosho nje ya Nchi na kuliongezea taifa fedha za kigeni" - Bi. Lilian Mwaipungwa

Hata hivyo Meneja wa utafiti na Mafunzo Kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mwal. Hamisi Sudi Mwanasala amemuhakikishia Mkuu wa Wilaya kuwa TBS imepania kuhakikisha bidhaa zitokanazo na korosho zinazalishwa kwa kuzigatia ubora wa Viwango vinavyokubarika katika soko la nje kwa kuwapatia mafunzo ya kutosha Wajasiriamali hawa kutoka Tandahimba.

Meneja wa kanda ya Kusini kutoka TBS Bi. Amina Yasini amesema Mafunzo watakao patiwa Wajasiriamali hao kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Taasisi zingine za serikali kama SIDO, mafunzo hayo yatajikita katika maeneo yafuatayo;

1) Kanuni za kilimo bora

2) Viwango na matakwa ya Viwango vya korosho

3) TeKnolojia mbalimbali za usindikaji korosho na bidhaa zake

4) Usajili wa Biashara

5) Kanuni bora za usindikaji

6) Vifungashio na ufungashaji wa bidhaa za korosho

7) Upatikanaji wa korosho ghafi na korosho katanga

8) Utaratibu wa kuthibitisha ubora wa bidhaa na usafirishaji wa bidhaa kwenda nje ya Nchi.

IMG_20210916_120017_303.jpg


IMG_20210916_120017_463.jpg


IMG_20210916_120017_386.jpg


IMG_20210916_120017_503.jpg
 
Back
Top Bottom