Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeagiza majengo ya baa, kantini, mihagawa, maduka makubwa, hoteli na maduka ya vipodozi visajiliwe na walipe tozo

Hii nchi bwana. Ndio maana kila siku wafanyabiashara wanalalamika "utitiri" wa kodi na tozo
 
Kupata Kibali hawawezi kutoa bure hata siku moja.

Mlolongo uliokataliwa TFDA unarudishwa kwa mgongo wa nyuma hii nchi ina laana hii.

Wangeunda upya TFDA iwe inashughulikia kila kitu, ubora wa bidhaa na vinywaji na udhibiti wa bidhaa za kutoka nje.

TBS ivunjwe.

Kisha ili kuondoa usumbufu kwa raia kuzunguka kutafuta vibali na kujisajili iundwe tovuti wa ajili ya wafanya biashara kuitumia popote pale walipo.

Kwa kuwa tayari BRELA na TRA wapo zile kanzi data zinakuwa zinawasiliana mtu anapotaka vibali ili kufanya uhakiki.

Mtu akimaliza kila kitu mtandaoni ndo aenda kule ofisi za TFDA kuhakiki na kukabidhiwa vibali original.

Hayo yatakuwa ni mapinduzi ya kimaendeleo pia si tu kufukuzana na akina nanihii.
 
Hakika masuala ya kuwa na vibali lukuki ni kuongeza urasimu tu badala ya kuboresha utoaji huduma.
BRELA kwenye masuala ya biashara ingekuwa kila kitu kinafanyika hapo huko mamlaka zingine zibakize suala la ukaguzi tu badala ya kuanza kukimbizana na watoa huduma.

Hawakuwa na sababu za kuondoa TFDA kwenye suala la dawa na chakula na kuipa TBS ambayo tayari ilishaelemewa na mzigo siku nyingi sana.
 
Back
Top Bottom