Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC) latoa ufafanuzi kuhusu taarifa za kutofanya kazi kwa Saa 24

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,992
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai kuwa Mawakala wa meli (shipping agents) hawafanyi kazi kwa muda wa Saa 24 katika siku saba (7) za wiki, Shirika la Uwaka wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa ufafanuzi.

TASAC imesema kuwa Wadau wa Sekta ya Usafiri majini kupitia Kamati ya Maboresho ya Bandari (PIC) wamekuwa wakitoa hoja na ushauri kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo suala la utoaji huduma za kibandari kwa utaratibu wa saa 24 katika siku 7 za wiki (24/7).

Katika kufanyia kazi hoja na ushauri wa wadau kupitia PIC kuhusu utaratibu wa Wadau wa huduma za kibandari kufanya kazi kwa saa 24 katika siku 7 za wiki, TASAC iliratibu kikao cha Wadau tarehe 12 Agosti, 2021 ili kukusanya maoni na kufanya maamuzi kadhaa

(i) Kuendelea na utaratibu wa wadau wa huduma za kibandari kufanya kazi kwa saa 24 katika siku 7 katika kuhudumia meli na shehena bandarini na katika bandari kavu, pamoja na kazi za bandari za kutoa vibali vinavyotakiwa ili shehena bandarini ihudumiwe;

(ii) Huduma za kiofisi zitolewazo na watoa huduma wengine wasio bandari au bandari kavu, kutolewa kama ifuatavyo;

a) Jumatatu – Ijumaa: saa 2.00 asubuhi – saa 3.00 usiku;
b) Jumamosi: saa 2.00 asubuhi – saa 11.00 jioni; na
c) Jumapili na Sikukuu za Kitaifa: saa 3.00 asubuhi – saa 8.00 alasiri;

Ufafanuzi wa Masaa 24-FINAL_page-0001.jpg

Pia Soma >> Kwanini Mawakala wa Meli (Shipping Line) hawafanyi kazi masaa 24 kama zamani?
 
Ufafanuzi mzuri na pia inaonyesha ule ujumbe uliwafikia ndo mpango mzima yaani.
 
Tunapenda mambo ya uwajibikaji kama hivi, siyo mnajifungia ndani tu.
 
Back
Top Bottom