#COVID19 Shirika la Afya Duniani (WHO) laitaka Tanzania kujiandaa kupokea chanjo ya Corona

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Siku moja baada ya Rais wa Tanzania, John Magufuli kutaka wizara ya afya kutokukimbilia chanjo ya Corona, Shirika la Afya Duniani WHO imeitaka nchi hiyo kujiandaa na chanjo ya Corona kama mataifa mengine duniani.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao, mkuu wa WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshdiso Moeti amesema kuwa Tanzania inatakiwa kutumia mwanya wa upatikanaji wa chanjo kwa faida ya wananchi na kanda ya Afrika Mashariki kwa ujumla.

''Tumeanza kuwasiliana upya na ngazi za juu za uongozi, na tunatoa mchango wetu kama ilivyokua hapo mwanzo, na tunataka kushirikiana na Tanzania, kwa niaba ya watu wa Tanzania, nchi jirani na dunia kwa ujumla. Sehemu ya mawasiliano yetu na Tanzania ni kukumbusha serikali kuwa, hii ni sehemu ya makubaliano ya kanuni za afya za kimataifa ambapo nchi wanachama wamekubali kwa pamoja kuzuia kusambaa kwa magonjwa'' anasema Dkt. Moeti.

WHO inasema kuwa imekua ikitoa mchango na kuwasiliana na serikali ya Tanzania kuanzia mwanzo wa janga hili la Corona. Shirika hilo pia limesisita Tanzania kutoa takwimu za mwenendo wa Corona nchini Tanzania ili iwe rahisi katika kupambana na kuzuia maambukizi mapya.

Naye katibu mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Tedros Ghebreyesus anasema anaunga mkono alichosema @MoetiTshidi, anatoa rai hatua dhabiti za kiafya kukabiliana dhidi ya corona zinapaswa kufuatwa na kujiandaa kupokea chanjo.

Takwimu ni suala la muhimu pia kwa Tanzania kuzitoa, tena baada ya kesi za miongoni mwa wasafiri na wageni katika miezi ya hivi karibuni.

Chanzo: BBC SWAHILI
 
Serikali lazima ikubali kupokea chanjo na kama inakataa lazima kuwa na hoja za msingi sana za kushawishi kuwa sio chanjo bora au ina shida. lakini kuikataa tuu haitawezekana kwa sababu uchumi wetu na kila kitu kinategemea muingiliano wa watu ni lazima chanjo tukubali kwani hili ni jambo jema kwani tuna chanjo nyingi sana tumezikubali na zimeonesha ufanisi mkubwa.

Serikali kukataa chanjo ni kuua watu wasio na hatia.

Tumesaini mikataba mingi ya kimataifa lazima tukubali chanjo hii.

Swala la chanjo ni lazima.
 
Dunia ni Kijiji, vyema tupate hizo chanjo ili kuruhusu watu waendelee na biashara zao hasa za kusafiri bila kuwekewa vikwazo vya kusafiri.

Tukikaidi kupewa chanjo hakuna Mtanzania ataruhusiwa kusafiri nje ya Mipaka.
 
Nimekagua maktaba ya Taifa kuona kama kuna Rais yeyote wa Afrika aliyewahi kupambana na the so called mabeberu akashinda. Aibu inamnyemelea Jiwe.
Hatuangalii historia we mtu mwetu mweusi. Huyuu ndo atakuwa wa kwanza kushinda hao waume zako beberuru..alaf kizaz chako cha vilaza ndo kitaanza kutambua kuwa kuna rais wa africa aliewah kuahinda beberu.
 
Hatupokei chanjo za kuletewa, watusubiri tutengeneze zetu na wao wawe tayari kuzipokea! Wapuuzi sana hawa! Kwetu tatizo siyo corona sisi tunataka chanjo ya malaria, kifua kikuu, ukimwi, kisonono, gonora, pressure, na kansa!

Hiyo covid-19 wapambane nayo wenyewe, siye huku Mungu ameshatuchanja! Huo ujuha wapeane wenyewe! Tanzania tutasimama kwa neema ya Mungu!
 
Back
Top Bottom