A
Anonymous
Guest
Wafanyakazi wa Idara ya Ardhi Mkoa wa Shinyanga na wale wa Manispaa ya Shinyanga wanafanya kazi zao kwa mazoea sana huku wakitengeneza mazingira ya kupokea rushwa kutoka kwa wananchi.
Kama week mbili zilizopita kulikuwa na zoezi la urasimishaji wa ardhi katika kata ya Kizumbi, kijiji cha Nhalegani, zoezi lililoratibiwa na watajwa hapo juu, wananchi walitakiwa kufika kwenye kituo kilichoandaliwa katika shule ya msingi Nhalegani wakiwa na nyalaka muhimu ili waweze kufanya utaratibu wa kupewa hati miliki za viwanja vyao.
Tatizo lilianza tu siku ya mwanzo kwa sababu zoezi zima lilikuwa disorganized huku watumishi wakiwa kama miungu watu pale mwananchi anapohitaji huduma zao na hili lilisabishwa na wao kutaka kutengeneza mazingira ya rushwa.
Kufupisha story ni kuwa baada ya mambo yote mwananchi alitakiwa kufunguliwa maombi kupitia mfumo wa e-ardhi na hapo kupokea control number ya kulipia maombi hayo shilingi 5000/= na baada ya hapo mwananchi anapokea control number nyingine kwa ajili ya kulipia hati.
Watu wote walilipia 5000/=hizo control number hazikuwa na shida lakini control number kwa ajili ya kulipia hati hapo watumishi hao walianza kutengeneza mazingira ya rushwa kwamba kama haujaongea nao vizur hawakupi control number, wanakwambia subiri, nenda nyumbani itaingia kwenye simu.
Sasa ni week ya tatu inaingia na bado watu wengi hawajapokea control number wanataka wananchi wawafuate ofisini kwao pale Manispaa ili wawaombe rushwa.
Hata ukifika pale ofisi kwao hakuna msaada wanajifanya wapo bize tu.
Tafadhali mamlaka husika liangalie hili jambo, watu wanateseka, wazee wanateseka kwenda kufuatilia jambo ambalo halikutakiwa kuwa na usumbufu wa hivyo kwa sababu huu ni mradi ambao kwa taarifa tulizo nazo unafadhiliwa na World Bank.
Kama hawatabadilika nitarudi hapa kuwataja majina watumishi wanao omba rushwa kwa wananchi.