Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 412
Nimekuwa nikifatilia shindano linaloendeshwa na kituo cha Televisheni cha TBC 1 kwa jina la Serebuka. Vijana wa kike na kiume hushindanishwa kucheza aina ya muziki kutoka Latin Amerika na Caribian. Mshindi (pea) wa shindano hilo anategemewa kuondoka na zawadi ya Sh. 25,000,000. Kwa mtazamo wangu kwa muda wote niliongalia shindano hilo sijaona mantiki au nini zao la mwisho la shindano hilo. Kwani sehemu kubwa ya muziki unaochezwa pale aina ya Salsa, charanga, Merengwe na mingine yenye asili ya Latini Amerika sioni kama itakuja kuwajenga watanzania kuthamini muziki wao. Kuna siku eti washiriki walijaribu kucheza baadhi ya ngoma za asili za Tanzania ambazo kwa mtazamo wangu wengi wao waliharibu.
Tofauti na jinsi wanavyoiga hayo macharanga yao. Pia hata hao majaji wa shindano hilo Masoud Masoud, Joan na Zahir Ally Zoro katika kutathmini kile kilichofanywa na washiriki sioni kama wanawaelekeza kujenga asili ya muziki wa Kitanzania zaidi ya kusifia mavazi, staili za nywele, na uchezaji kwa ujumla, mwishowe watu wanatiwa moyo ili waje kuondoka na hiyo 25ml.
Nadhani kuna haja ya kuanzisha mashindano yenye uelekeo wa kujenga asili ya muziki wa kitanzania zaidi kuliko haya mambo ya kuigaiga tu. Mpaka leo Tanzania tunahangaika kupata vitu vyenye asili ya kitanzania kama vile muziki na mavazi lakini hatujafanikiwa. Ila kwa ku-copy na ku-paste tuko vizuri sana. Tuboreshe basi achimenengule na mitindo mingine na wa huko Latin Amerika waige....Ni mtazamo wangu!