Shindano la Serebuka TBC1.. Ni utumwa mambo leo au Ujasiriamali?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shindano la Serebuka TBC1.. Ni utumwa mambo leo au Ujasiriamali??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sajenti, Apr 26, 2010.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikifatilia shindano linaloendeshwa na kituo cha Televisheni cha TBC 1 kwa jina la Serebuka. Vijana wa kike na kiume hushindanishwa kucheza aina ya muziki kutoka Latin Amerika na Caribian. Mshindi (pea) wa shindano hilo anategemewa kuondoka na zawadi ya Sh. 25,000,000. Kwa mtazamo wangu kwa muda wote niliongalia shindano hilo sijaona mantiki au nini zao la mwisho la shindano hilo. Kwani sehemu kubwa ya muziki unaochezwa pale aina ya Salsa, charanga, Merengwe na mingine yenye asili ya Latini Amerika sioni kama itakuja kuwajenga watanzania kuthamini muziki wao. Kuna siku eti washiriki walijaribu kucheza baadhi ya ngoma za asili za Tanzania ambazo kwa mtazamo wangu wengi wao waliharibu.

  Tofauti na jinsi wanavyoiga hayo macharanga yao. Pia hata hao majaji wa shindano hilo Masoud Masoud, Joan na Zahir Ally Zoro katika kutathmini kile kilichofanywa na washiriki sioni kama wanawaelekeza kujenga asili ya muziki wa Kitanzania zaidi ya kusifia mavazi, staili za nywele, na uchezaji kwa ujumla, mwishowe watu wanatiwa moyo ili waje kuondoka na hiyo 25ml.

  Nadhani kuna haja ya kuanzisha mashindano yenye uelekeo wa kujenga asili ya muziki wa kitanzania zaidi kuliko haya mambo ya kuigaiga tu. Mpaka leo Tanzania tunahangaika kupata vitu vyenye asili ya kitanzania kama vile muziki na mavazi lakini hatujafanikiwa. Ila kwa ku-copy na ku-paste tuko vizuri sana. Tuboreshe basi achimenengule na mitindo mingine na wa huko Latin Amerika waige....Ni mtazamo wangu!
   
 2. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2010
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 80
  Hayo mashindano ni ufinyu wa mawazo na uchovu wa kufikiri. Yaani ni mwendo wa ku-COPY NA ku-PASTE michezo au mashindano ya ulaya kama American idol. Tubadilike ndugu zangu!!!!!!!!!!!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ukiacha hizo Montuno na Merengwe, pia nyimbo zote za twist wanazocheza ni za nchi jirani ya Kenya!...Inatisha sana hii!
  Anyway, they have MONEY to give AWAY, acha wampe mtu apate maisha bora!
   
 4. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Ah, Afadhali! Nilidhani ni mimi tu ninayeuona huu ulimbukeni unaondelea TBC! Kinachowazuia angalau siku moja watu washindane kucheza muziki wa Sikinde ama Msondo ni nini??????
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Wangefanya ziwe ngoma za kienyeji tupu ningewasifu. Ngoma kama gobogobo ya wasukuma, kiduo ya wahehe, msakamale na mkwaju ngoma pale Morogoro, gombesugu na mdundiko uzaramoni, Kambindi, ligihu, lizombe, kitoto za pale bombi hii nyumbi hii aka Songea, TANGA kunani zipo kibao tuu. kwa nini lkn tucheze za wenzetu? za kwetu nani ataziendeleza?
   
 6. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Aaaghhhh... Aliyetuloga keshajifia...
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Mhh wabongo bana
  .kazi ya tv ni kuvutia watazamaji.......
  Hicho kipindi si cha tbc ni cha watu binafsi wamenunua air time na kutafuta
  wadhamini...........

  Kama nyinyi mna mawazo yenu mnaruhusiwa ni nyinyi
  kwenda kwenye tv na kununua air time na kutafuta wadhamini na kuendesha kipindi
  mnachokipenda nyinyi........

  Kuponda ponda kila kitu sometime ni ujinga zaidi......

  Fanyeni yenu tuone.........
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Nadhani hapa Mkuu Boss hujaelewa kinachoboa watu ninini.
  Ishu ni kwamba watu hawapendi nyimbo zinazoshindaniwa, (salsa, merengwe,kumbya etc)regardless ya nani anarusha kipindi, whether ni TBC1 au cnn...
  Sa sijui unapata wapi kuwa watu wanaboreka na TBC!
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  wanaosema hiki kipindi ni copy and paste
  angalau nawaelewa na nakubaliana nao.........

  tatizo la vipindi hivi vya copy and paste ni kuwa ni ngumu kuweka
  mambo yako mengine bila kuharibu format........

  kwa yeyote aliewahi kutazama" dance with stars"
  wala hawezi kutokielewa kipindi cha selebuka........

  ni kama american idol na bongo star search.........
   
 10. n

  nndondo JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana sana na wewe ila sijui kama kuna anaetusikiliza, Tanzania imegeuka shamba la wendawazimu, hakuna wa kusikiliza la mtu, hakuna asiyejua kitu watu wanahangaika kutafuta umaarufu kwa njia yoyote, ni kuganga njaa kwa njia ya aibu na kuigaiga tu, sasa charanga na TBC wapi na wapi? pili hiyo TBC ni tatizo lingine, hakuna programming ni show off tupu kwa hela za kodi, hakuna biashara hakuna nini ni mchezo tu magazeti yameshaaandika mzee utoh wa mahesabu ameshasema ndio hayo hayo mambo ya JK ya kubebana, hawana vipindi zaidi ya taarifa ya habari maana hata jambo tanzania marin hassan kaamua kuigeuza uwanja wa taarab na kusafishia wanasiasa wa CCM. Its so sad, nadhani tuandike petition ukusanye sahihi za kutosha tupeleke TCRA maana maelezo nako ni kimbembe kipya, tuwaambie wafunge vipindi vyote vya kipumbavu.

   
 11. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Unajua kuna mambo mengine tusipoelezana sisi wenyewe sidhani kama kuna mtu atakayekuja kueleza kwa niaba yetu. Nimejaribu kueleza katika thread kuwa Tanzania tumekuwa tukihangaika kwa muda mrefu kutafuta utambulisho wetu kama watanzania kuanzia muziki mpaka mavazi lakini mpaka leo hii hatujafanikiwa. Kama mtu ana mipesa yake ni kweli hatumkatazi asitapanye atakavyo. Lakini mwisho wa siku ni vizuri tuwe na mtazamo mpana zaidi katika kupata huo utambulisho. Tumekuwa mafundi wa kuiga mambo ya wenzetu sana kiasi kwamba sioni huko tuendako kama tutafika. Hiyo serebuka inaburudisha kwa maana ya muziki unaochezwa mle lakini mwisho wa siku jamii inavuna nini? Kuna vyombo vinavyoshughulika na haya mambo ya utamaduni vinatakiwa kuamka na kuonyesha njia....Nina jamaa yangu alikuwa Abuja just last week wakati yuko huko nilimuomba akipata muda ajaribu kuangalia katika maduka ya kuuza kanda za video na CD kama kuna sinema yoyote iliyoigizwa na wasanii wa kitanzania, katika maduka 8 aliyopita hakuona hata moja. Lakini angalia hapa mjini na huko mikoani kila siku wafanyabiashara wanajaza sinema za ki-nigeria. Sasa sie tuwe watu wa kutukuza vya wenzetu na sie vyetu atavitukuza nani jamani??
   
 12. 124 Ali

  124 Ali JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 5,709
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  Mimi nafikiri tufike mahali tujiulize,haya tushuhudiayo ni matokeo ya fikra finyu za wasambazaji au kutojua wakitakacho walaji?

  Nini ugumu wa hitaji halisi la mtanzania wa sasa na baadaye kwa maana ya upatikanaji wa burudani za kiasili za tanzania .

  Kuna tabu burudani zetu asilia kuzifanyia modification kiasi ili ziendane na wakati tuliona-,hapa namaanisha matumizi ya lugha baadhi ya ala na majukwaa !

  Yote juu ya yote TBC wanachefua!
   
 13. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2010
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145

  na umenena sawa kabisa
  mimi niliangalia mara 2 baada ya watu kunishtua,kwakweli nilisiktika sana adi nikajiuliza "ivi izi pesa za kulipana ivo,kwa lipi hasa?je hakuna jambo la kitanzania zaidi kulipana izo milioni ambalo litajenga hasa kizazi chetu na kuthamini utanzania?"
  kwakweli ni kipindi ambacho hakifai hata kidogo na hakina maana zaidi ya kuuza sura na kutafuta ujinga wa umaarufu
  ovyo kabisa
   
 14. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2010
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  tena nyimbo za majirani zetu,,,hapa ndo nilichoka kabisaaaaa
  ivi ulishawai kwenda kwa mairani zetu (maana tusiazie mbali)ukaona wanatukuza chochote cha tanzania?
  zaidi sana wanasema ni vya kwao kisa ukisimama kwao unaona kwa tanzania
  kazi kweli kweli
   
 15. Bollo Yang

  Bollo Yang JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2010
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 440
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Thank God..sijawahi kuangalia hiko kipindi hata siku moja....
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Apr 26, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mwanzisha mada anaweza kuwa hajaridhika kwa sababu malengo yake, kama alivyoyaelezea kwenye bandiko lake, hayajatimia kupitia shindanio hili. Lakini pia inabidi tuangalie walioanzisha shindano hilo walikuwa na malengo gani. Labda hawakulenga kudumisha muziki au ngoma za asili
   
 17. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #17
  Apr 26, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Ndio maana nikauliza ni ule mzimu wa kutawaliwa bado unatusumbua au ndio kiu ya kupata 25ml watu watoke kimaisha?? Maana hata Raisi wa awamu ya tatu aliwahi kusema kuwa imefikia mahali watanzani wanataka kufanikiwa maishani kwa ujanja tu....Wewe kama una hayo mahela yako nenda hospitali ya amana pale akina mama wajawazito wanalala mzungu wa 4 kanunue vitanda na magodoro uwawekee tutakuona una kichwa chenye akili na sio kutuwekea eti Charanga, Merengwe na Twist tunaweza kununua CD na kanda madukani tukaenda kusikiliza majumbani mwetu....
   
 18. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #18
  Apr 27, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  By the way wapo watu wanaopendezewa na kipindi hicho! Licha ya mapungufu yaliyopo lakini ni haki yao TBC kurusha, kwani wana mambo mengi yanayochefua wanayarusha na watu bado wanapendelea kuangalia.
   
 19. edwinito

  edwinito JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35


  thank god.......mimi tv yangu haikamati tbc!!!!!! Tehe tehe tehe!!
   
 20. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2010
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwa maoni yangu ni kuwa kwanini wasingechukua watu wageni wacheze hayo macharanga yao na salsa kuliko hao celebs wa bongo si tayari wako vizuri ni bora hizo pesa ziende kwa underground, hao celebs wa bongo tayari wameshatoka ya nini tena washindanishwe wapate hizo 25M.
   
Loading...