Hebu wanajamvi nikumbusheni Wizara hii ni ile aliyotoka Ngeleja halafu akapewa mtu Mongo zaidi na katibu wake sijui Maswi? si ni hawa jamaa miezi michache iliyopita walikuja na porojo kibao kwamba wao wamekuja na muarobaini wa kukosa wa mgao wa umeme? hebu nikumbusheni kama ndiyo niwadharau zaidi kwa kuwa niliwadharau tangu siku ya kwanza walipokuja na majungu badala ya strategies, sasa mambo ni magumu Mgao upo zaidi ya ilivyokuwa siwasikii tena, visingizio vimekwisha? mto ndiyo huo unakauka wako wapi watolee maelezo? kama sikosei niiwasikia wakifoka kama chatu mpaka povu likawatoka mdomoni kwamba hata kuendesha mitambo ya mafuta mazito ni wizi mtupu wao wangeweza kuleta umeme wa mtera bila kutumia hata lita moja ya mafuta, ama ilikuwa kupagawa kupewa uwaziri? tumewazoa hata mkirudi tena tutawataka mujizuru hala nanyi mtakaa kwa hiyo maisha yataendelea rudini tuu mtutake radhi labda tutawapa mawazo mbadala badala ya kukimbia kabisa.
basi kama hawa jamaa ni walewale ninaowafikiria naombeni muwape pole zao, Uwaziri ni kazi kubwa si ya kuropoka.