Shilingi bilioni 86 zaibwa Wizara ya Nishati/TANESCO


n00b

n00b

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Messages
961
Likes
160
Points
60
n00b

n00b

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2008
961 160 60


Shilingi bilioni 86 zaibwa Wizara ya Nishati/TANESCO, Gridi ya Taifa hatarini

Gazeti la The East African la Novemba 24 – 30, 2012 limetoa taarifa kwamba jumla ya dola za kimarekani milioni 54 zimegundulika kuibwa na watumishi waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la TANESCO kupitia manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mtambo wa Umeme wa IPTL. Gazeti hili limenukuu taarifa ya ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Tanzania (Controller and Auditor General). Taarifa hiyo inasema kuna kikundi (racket) ambacho kazi yake kubwa ni kujifaidisha binafsi na mpango wa umeme wa dharura kupitia manunuzi ya Mafuta mazito ya IPTL.

Itakumbukwa kwamba toka mwaka 2011 kumekuwa na shinikizo lililotolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba zabuni za ununuzi wa mafuta ya kuendesha mpango wa umeme wa dharura na mchakato mzima wa manunuzi ya mafuta haya ufanyiwe uchunguzi wa kina (forensic audit).

Katika mkutano wa 3 wa Bunge la Kumi (April 2011) niliuliza swali Bungeni kuhusu kashfa hii ya ununuzi wa mafuta ya kuendesha mtambo wa IPTL na baadaye tarehe 16 Aprili 2011 nilimwomba Spika airuhusu Kamati ya Nishati na Madini kufanya uchunguzi kuhusu kashfa hii. Kamati ya Nishati na Madini chini ya aliyekuwa Mwenyekiti ndugu January Makamba ililitaka Bunge kuazimia kufanyika kwa uchunguzi kuhusu suala hili kwenye Taarifa yake ya mwaka 2011 iliyowasilishwa Bungeni mwezi Aprili mwaka 2012. Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ndugu John Mnyika katika Hotuba yake ya Bajeti ya Wizara hiyo mwaka 2011 alipendekeza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu kashfa hii pia. Juhudi zote hizo hazikuzaa matunda.

Kipindi hicho kiwango kilichokuwa kinahojiwa kuibwa ni shilingi bilioni 15 tu. Taarifa ya The East African kama walivyonukuu kutoka kwenye taarifa ya CAG inaonyesha fedha zilizoibwa ni shilingi bilioni 86. Zabuni za kununua mafuta ya kuendesha umeme wa dharura zimekuwa zikitolewa bila kufuata utaratibu wa zabuni kwa mujibu wa Sheria ya manunuzi. Hivi sasa kila mwezi Tanzania inatumia dola milioni 70 kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme.

Fedha hizi zinatoka Hazina na sehemu ndogo kutoka TANESCO. Wakati fedha hizi bilioni 112 zinachomwa kila mwezi kununua mafuta mazito na dizeli ya kuendesha mitambo ya umeme, Taarifa za kitaalamu zinaonyesha kwamba Bwawa la Mtera hivi lina kina cha maji chini ya kiwango kinachotakiwa na uzalishaji wa umeme ni asilimia 20 tu ya uwezo (installed capacity). Iwapo TANESCO wataendelea kutumia zaidi maji yaliyopo Mtera, Mitambo itashindwa kazi na Gridi nzima itasimama maana Mtera ndio nguzo kuu ya Gridi ya Taifa. Hali hii ni hatari sana kwa uchumi na ulinzi na usalama wa Taifa. Kimsingi Gridi ya Taifa ipo hatarini kutokana na kiwango cha Maji kilichopo Mtera hivi sasa na kuendelea kupungua kwa kina hicho cha maji.

Wananchi wanapaswa kuelezwa kinaga ubaga nini kinaendelea katika sekta ndogo ya umeme hapa nchini;

1. Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kuhusu zabuni za manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura iwekwe wazi na ‘racket' inayosemekana kuiba jumla ya shilingi bilioni 86 ionyeshwe na hatua za kisheria zichukuliwe mara moja na bila kuchelewa.

2. Waziri wa Nishati na Maadini auleze umma hali yalisi ya sekta ya umeme nchini, uzalishaji wa umeme upoje, hali ya maji katika bwawa mkakati la Mtera na nini hatma ya mitambo ya IPTL, kesi zake na utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge kuwa kesi za kampuni hii zimalizwe nje ya mahakama. Pia Taifa lielezwe Mpango wa Dharura wa umeme unakwisha lini maana muda uliotolewa na Bunge mwezi Agosti mwaka 2011 tayari umekamilika. Waziri aeleze hatua agni amechukua baada ya kukabidhiwa taarifa na CAG kuhusu maafisa waandamizi wa Wizara waliohusika na wizi wa shilingi bilioni 86 za kununua mafuta ya IPTL.

3.Waziri wa Fedha na Uchumi aueleze umma ni kiwango gani cha fedha Hazina imetoa kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura kati ya Mwezi Novemba mwaka 2011 na Oktoba mwaka 2012 na kama taratibu zote za zabuni zilifuatwa na pale ambapo hazikufuatwa ni hatua gani PPRA wamechukua dhidi ya waliokiuka sheria ya manunuzi na kuleta hasara ya mabilioni ya fedha kwa Serikali.

Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa Fedha
Dar es Salaam. Novemba 25, 2012
 
M

Mr jokes and serious

Member
Joined
Oct 4, 2012
Messages
78
Likes
0
Points
0
Age
30
M

Mr jokes and serious

Member
Joined Oct 4, 2012
78 0 0
Aise du acha wale nchi imeoza.
 
S

swrc

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2012
Messages
442
Likes
1
Points
0
Age
48
S

swrc

JF-Expert Member
Joined Jun 17, 2012
442 1 0
ufisadi ni tatizo kubwa sana ktk serekali inayoongozwa na chama chetu kitukufu. Ikiwa wewe baba ni mwizi na utakopomuona mtoto anaiba utaweza kweli kumuonya? Hapa hata zipigwe kelele za namna gani hakuna hatua zozote zitakazochukuliwa. Wanalindana kwa sababu wote ni majizi yaliyokubuhu, hakuna wa kumchukulia hatua mwenzake.
 
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
31,874
Likes
65,377
Points
280
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2012
31,874 65,377 280
Nchi hii, tunahitaji mapinduzi kama yale ya Misri na kwingineko.Serikali iliyopo madarakani imekubuhu kwa kulea wizi na ufisadi.Kwa maana hiyo, ukombozi wa taifa letu uko mikononi mwetu sisi wabongo wenyewe na kamwe tusiitegemee serikali hii ya magamba.Kwani hili sasa ni genge la wahujumu uchumi na si tena chama cha siasa kinachostahili kuendelea kuongoza nchi hii.

Tafakari na chukua hatua sahihi bila kuchelewa.
 
K

Kagalala

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Messages
2,373
Likes
93
Points
145
K

Kagalala

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2010
2,373 93 145
Tunapoambiwa Elimu Bure inawezekana tunaona kama ni ndoto. Imagine hizi pesa zote zinazoliwa na watu wachache wenye uchoyo wa hali ya juu zingekuwa zinatumika katika maendeleo ya nchi tungekuwa wapi. Hii kwa wenzetu waziri angeachia ngazi mara moja, lakini kwetu ukiwa mwizi mkubwa Polisi wanakuogopa.
 
Lukolo

Lukolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
5,147
Likes
103
Points
160
Lukolo

Lukolo

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
5,147 103 160
Here we go again. Na Kikwete bado tu hajiuzuru na anajiona ni salama kupita usalama kwakuwa tu analindwa na wanajeshi. Kama watu wanaweza kuiba kiasi kikubwa namna hii cha pesa bila ya rais kujua ni kwa vipi watashindwa kupanga mipango ya kuipindua serikali yake bila ya yeye kujua pia?
 
M

MPEGA Jr

New Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
1
Likes
0
Points
0
M

MPEGA Jr

New Member
Joined Nov 18, 2012
1 0 0
nafasi ya kila kiongozi ni kutumia kiasi cha mali (resources) kilichopo kwa manufaa ya Wananchi.
Ni dhahiri tuna aina ya viongozi wasiojua majukumu yao kwa Taifa. Ni jukumu la Serikali kufuatulia na kuhakikisha mianya nyote ya ubadhirifu wa fedha za uuma zinadhibitiwa. Mwananhi nini mchango wako wa kulinda mali yako?
 
D

DR. PHONE

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2012
Messages
504
Likes
0
Points
0
D

DR. PHONE

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2012
504 0 0
aiseeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee hakya mama tena yani mwisho wao ushatimia
 
Manyi

Manyi

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2011
Messages
3,255
Likes
11
Points
135
Manyi

Manyi

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2011
3,255 11 135
Hivi sheria ya kunyonga wahujumu uchumi si bado ipo?
 
B

blueray

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Messages
2,219
Likes
6
Points
0
B

blueray

JF-Expert Member
Joined Sep 15, 2012
2,219 6 0
Nchi haina rais, na pia haina wananchi?

Haya ndio kina Le Mutuz et al wanasimamia na kushinda kwenye mitandao kuyatetea na kuyapigania!

Ndugu zangu wananchi amkeni tuikomboe nchi yetu kutoka mikononi mwa mafisadi, la sivyo sisi na vizazi vyetu wote tutaangamia!
 
N

namweni

Member
Joined
Jan 16, 2012
Messages
25
Likes
0
Points
0
N

namweni

Member
Joined Jan 16, 2012
25 0 0
kwa jinsi ilivyo taarifa nyingi za CAG hupelekwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa kama ilivyofanyika awali na watu wengi kutoka madarakani, kwa nini taarifa haikufika bungeni na maamuzi kutolewa kama taarifa zingine zilizoenda, kuna nini ndani kinajificha?
 
2hery

2hery

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2011
Messages
4,108
Likes
2,957
Points
280
2hery

2hery

JF-Expert Member
Joined May 27, 2011
4,108 2,957 280
Kwa kweli hali ya maji bwawa la mtera ni mbaya sana na ni juzi tu wamemaliza kufanya ukarabati wa mitambo ila tatizo litabaki palepale
 
B

Bangoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Messages
5,600
Likes
5
Points
135
B

Bangoo

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2011
5,600 5 135
#Nchi yetu iko chini ya chama cha ufisadi,
#Tuna Raisi muoga asiye na maamuzi zaidi ya kwenda kuomba omba,
tuombe Mungu atujaalie amuondoe madarakani mapema.
 
K

Kirokolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2008
Messages
236
Likes
101
Points
60
K

Kirokolo

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2008
236 101 60
Kengele ni ya moto na paka amekuwa kichaa! Utawala wa panya na himaya yake itadumuje? Hatua ya juu kabisa inayoweza kuchukuliwa ni kupiga kelele humu na kuandika kwenye magazeti na blogs. Hatuna uwanja wa Tahriri?
 
Zogwale

Zogwale

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2008
Messages
12,027
Likes
1,379
Points
280
Zogwale

Zogwale

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2008
12,027 1,379 280
Tanzania kila kitu kinawezekana!! Ulaji nao utakuwa ni wa mtandao!! Haya tena!!
 
SHERRIF ARPAIO

SHERRIF ARPAIO

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2010
Messages
8,464
Likes
2,760
Points
280
SHERRIF ARPAIO

SHERRIF ARPAIO

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2010
8,464 2,760 280
Uko wapi kaka William Malecela. Nataka kusikia maoni yako wewe na wana CCM mliopo diaspora
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,875
Likes
8,032
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,875 8,032 280
yeah yeah yeah.. can somebody something we don't already know about ufisadi.. hivi ni ofisi gani ambapo watendaji wake hawatumii madaraka yao kujitengenezea njuluku kwa njia za ufisadi?
 
U

Ubungo

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2012
Messages
1,238
Likes
14
Points
0
Age
38
U

Ubungo

JF-Expert Member
Joined Apr 7, 2012
1,238 14 0
Mhe. Zitto, taarifa hii inasikitisha sana. Wahusika watajwe na wapelekwe mahakamani kwa kuhujumu uchumi.
 

Forum statistics

Threads 1,237,857
Members 475,675
Posts 29,303,701