Mwitongo
JF-Expert Member
- Jan 30, 2009
- 312
- 362
Aah, mimi nilifikiri unakanusha kwamba hakuna upotevu wa hizo shs. bil 80! Kumbe umekasirishwa tu na kitendo cha Zitto kushikia bango fedha zilizobainika kuibwa. Zirudisheni kwanza fedha hizi, then Zitto naye atashughulikiwa accordingly.
Sijakasirishwa na hilo, kinachoshangaza hapa ni kuona wachangiaji wengi wanachukulia jambo hili kuwa ni jipya! Ndiyo maana wapo wengine wanadiriki kusema, "Ufisadi mwingine Tanzania"! Mwingine upi? Jambo la zamani lazima lielezwe kuwa la zamani.
Vinginevyo kuna mtu ataibuka hapa na kuandika, "Mwalimu Julius Nyerere afariki dunia"-na sisi wa ukosefu wa kumbukumbu tukaanza kuchangia-wa kusikitika, na wa kufurahia kifo.
Ninachosema hapa ni kwamba kama ni jambo la kujua hao wezi wa Bilioni 80 wameshughulikiwa au laa, hapo ni sahihi; lakini si kuleta posti na mbwembwe za kuonesha kuwa kinachosema na Ziwa ni Breaking News!