Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,305
- 33,924
Shida ya wapinzani wa Lissu ni kwamba wanakosa njia ya kumsingizia kwamba kwenye maisha yake ya Uwakili na siasa amewahi kula au kutoa Rushwa. Ukiona nguvu ya CCM inayotumika kwa Lissu tangu mwaka 2010, basi unajua ni kwa nini CCM wanafikia hadi kutamani kufa kwa Lissu.
Kama Lissu angekuwa na makando kando kwenye maisha yake ya kisiasa zamani sana angekuwa tayari "keshanyamazishwa" na maadui zake. Tangu enzi za Mkapa mpa sasa imeshapita zaidi ya miaka 18 lakini CCM wameshindwa kumzushia Lissu kashifa ya matendo ya kiufisadi.
Mbowe anaitwa Mchaga na siyo msomi, Maalimu Seifu anaitwa Sultan na mpemba, Lowassa anaitwa mgonjwa na mroho wa madaraka. Lakini kwa sasa Lissu anazushiwa kwamba hana staha, si muungwana na akili zake haziko sawa.
Vita ya CCM dhidi Lissu inakuwa ngumu kwa kuwa yeye si mla rushwa na wala hategemei upendeleo kuendesha maisha yake. Nakumbuka Zitto alipopaza sauti kuhusu Escrow wabaya zake wakamkumbusha jinsi anavyojipatia hela toka kwenye mifuko ya Hifadhi ya jamii kwa njia ya upendeleo.
Safi sana Lissu kwa kutokuwa mla Rushwa!