CHADEMA kwafukuta moto mkali, Mbowe na Lissu hakuna maelewano

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,280
9,719
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa jirani hakukaliki wala hakuna utulivu wala amani ndani ya nyumba yao. Hii ni baada ya hali ya kutoelewana kati ya Mbowe na lissu kwa muda mrefu sana kunakochangiwa na mambo mengi sana. Kwa kiasi kikubwa hali hiyo imetokana na misimamo Bayana ya wawili hao kuwa tofauti na kila mmoja akiona mwenzake hayupo sawa. Mbowe hamkubali na anatofautiana pakubwa sana na misimamo ya lissu.anaona Lissu anaendesha na kutaka kufanya siasa kali zenye misimamo mikali yenye kukiathiri chama.siasa za Lissu ni za mashambulizi ya lugha mbaya na chafu.

Wakati yeye Lissu anamuona na kumtuhumu Mbowe kuwa anaendesha siasa laini na kwamba amelambishwa asali iliyomkolea na kumzidi utamu na kujisahau,jambo ambalo mbowe amekuwa akilipinga na kulikanusha hadharani na kueleza namna alivyokipambania chama hicho kwa jasho,damu,machozi na maumivu makali sana ,na kwamba amehatarisha uhai wake na hata uchumi wake kwa misimamo yake ya kukipigania na kukijenga chama hicho kwa miaka mingi sana.

Hata maridhiano yaliyokuwa yakiendelea kati ya CHADEMA na CCM au Serikali ya CCM Ambayo kwa kiasi kikubwa sana yamezaa matunda mazuri ikiwepo kufunguliwa na kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara,kufutwa kwa kesi zenye sura za kisiasa kwa viongozi wake,kuwarejesha nchini waliokuwa uhamishoni akiwepo Lissu mwenyewe na mengine mengi tu.imeonyesha kumkera sana lissu na kutohitaji njia hiyo au mipango hiyo ya vikao vya maridhiano kuendelea kufanyika au kukutana katika kujadili Masuala mbalimbali.

Inasemekana Lissu yeye anataka siasa za kianaharakati zaidi,jino kwa jino,mavurugu na kutunishiana misuli kati ya serikali na yeye, inasemekana mambo hayo yamekigawa hata chama ndani yake ambapo wapo walio upande wa Lissu na wengine upande wa mbowe. Inaelezwa kuwa ndio sababu hata ya Lissu kukwepa kuja katika ziara ya kanda ya nyasa kwa kisingizio kuwa atakuwa na ziara nchini Marekani,lakini lengo likiwa ni kutotaka kuwa karibu na mbowe.

Habari zinaeleza kuwa ndio sababu hata Lissu akija na kufanya mikutano nchini huwa anakuwa pekee yake wakati wote na mwisho hujiondokea kimya kimya kwenda ulaya,kwa kuwa hataki kuwa nchini na kuendelea kuwa karibu ya Mbowe. Lakini pia ndio sababu hata kampeni za 2020 mbowe hakuwa akiambatana na Lissu popote pale kwa kuwa hakuwa anataka lissu apeperushe bendera ya chama hicho ila ilibidi tu ampe ili kuwaridhisha vijana waliokuwa wanataka Lissu agombee lakini mbowe halikuwa chaguo lake kabisa.

Inaelezwa kuwa ndio sababu hata mbowe hataki kuachia uenyekiti wa chama kama ilivyokuwa inatarajiwa kuwa mwaka huu angeachia uenyekiti,sababu ni hofu ya Mbowe iliyomjaa ndani yake kuwa akitangaza kuachia uenyekiti wake chama kinaweza kuangukia mikononi mwa Lissu jambo ambalo litakuwa la hatari sana tena sana kwa ustawi wa chama ,kwa kuwa mbowe anamfahamu vyema Lissu kuwa atakipasua chama ,kukimaliza ,kukisambaratisha na kukiangamiza kabisa au kukifuta kabisa katika Ramani ya siasa hapa nchini kutokana na tabia yake na majibu yake ya dharau,ujeuri,ujuaji,kiburi na kujiona yeye ni yeye na mawazo yake ndio sahihi muda wote na wengine ni wapumbavu.lakini pia ni tabia yake ya kutokutaka ushauri,maridhiano,subira na kifua cha uongozi chenye kuwavumilia wale anaotofautiana nao kimsimamo na kimtazamo ndani ya chama.

Inaelezwa kuwa mbowe anajuwa aina ya vijana alionao ndani ya chama chake na namna ya kuwaongoza.anajuwa ni vijana wenye mihemuko, kukurupuka,kukosa subira na uvumilivu,waropokaji na wenye haraka kwa kila jambo,hivyo namna ya kuwaongoza ni kuwa na hekima ya hali ya juu sana,utulivu,subira ,kifua na busara ya kipekee.

vitu na mambo ambayo Lissu hajafanikiwa kuwa navyo hata chembe,hivyo ikiwa chama kitaangukia mikononi mwake basi ndio utakuwa mwisho wa chama hicho hapa nchini na hivyo kubakia historia kama ilivyo NCCR mageuzi.jambo ambalo mbowe asingependa kuliona likitokea akiwa hai ,kutokana na kukisotea chama hicho asingependa kuona hayo yakitokea machoni pake.ndio maana Anaendelea kupambana kuhakikisha sumu ya Lissu haiathiri chama na wala hakiteki chama na wala hakiangukii mikononi pake. .

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa jirani hakukaliki wala hakuna utulivu wala amani ndani ya nyumba yao. Hii ni baada ya hali ya kutoelewana kati ya Mbowe na lissu kwa muda mrefu sana kunakochangiwa na mambo mengi sana. Kwa kiasi kikubwa hali hiyo imetokana na

0742-676627.
Ningekuelewa kama ungesema Chongolo na Makonda hakuna maelewano! Ona Chongolo hadi sasa anajitafuta ampongeze au yeye mwenyewe asepe!
 
Ningekuelewa kama ungesema Chongolo na Makonda hakuna maelewano! Ona Chongolo hadi sasa anajitafuta ampongeze au yeye mwenyewe asepe!
Ndani ya CCM amani na upendo vimetawala na ndio maana unaona viongozi wakiendelea kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza kazi na majukumu ya chama.
 
Kazi yangu ni kuhabarisha tu ukweli .
Hadithi zako za alinacha hata wanaccm wenzako wana kudharau siku hizi.
Wamegundua kuwa "mtu akikudanganya kila siku huku akijua unajua kuwa unadanganya, basi anakudharau".
Sasa wamechoka kwa wewe kuwadharau na hadithi zako za Alinacha au Kalumekenge ili upate nafasi ya kuweka namba ya Simu.
Kifupi una fanya Betting ya maokoto.
 
Kwahiyo unamuwekea namba ya Simu Mwamba akutumie na ya kutokea 😂😂😂🐼
Kaombe majibu ya mahali zilipo pesa za join the chain na Zilipatikana shilingi ngapi. Ndio utaelewa CHADEMA ipo kwa ajili ya Usaka Tonge tu na siyo kuwasadia watanzania kwa aina yoyote ile. Muulize mbowe kama amewahi tuma pesa mikoani kusaidia shughuli za chama.
 
Hadithi zako za alinacha hata wanaccm wenzako wana kudharau siku hizi.
Wamegundua kuwa "mtu akikudanganya kila siku huku akijua unajua kuwa unadanganya, basi anakudharau".
Sasa wamechoka kwa wewe kuwadharau na hadithi zako za Alinacha au Kalumekenge ili upate nafasi ya kuweka namba ya Simu.
Kifupi una fanya Betting ya maokoto.
Mimi naeleza ukweli tu ili mjue na kupata ukweli wa mambo mbalimbali msiyoyajua .
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa jirani hakukaliki wala hakuna utulivu wala amani ndani ya nyumba yao. Hii ni baada ya hali ya kutoelewana kati ya Mbowe na lissu kwa muda mrefu sana kunakochangiwa na mambo mengi sana. Kwa kiasi kikubwa hali hiyo imetokana na
Mpaka ulambe teuzi hakuna kukata tamaa
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa jirani hakukaliki wala hakuna utulivu wala amani ndani ya nyumba yao. Hii ni baada ya hali ya kutoelewana kati ya Mbowe na lissu kwa muda mrefu sana kunakochangiwa na mambo mengi sana. Kwa kiasi kikubwa hali hiyo imetokana na

0742-676627.
Haya ndio matamanio ya kila jizi la kura la ccm.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom