Shida ya maji Dodoma itaisha lini?

Shida ya maji Dodoma itaisha lini?

Nipo Hapa Kwenye Hili Jiji Linaloitwa Dodoma Mtaa Wa Kisasa (Nyumba 300), Kuna Shida Ya Maji Hadi Unajiuliza Kweli Hapa Ndio Makao Makuu Ya Nchi?

Wananchi Wa Hapa Hupata Maji Sometimes Mara Moja Kwa Wiki Ama Inaweza Ikatokea Yasitoke Kabisa Ndani Ya Wiki Nzima Mfano Kwa Muda Huu Ni Almost Wiki Mbili Maji Hayajatoka Na Ni Hapa Hapa Mjini.

Je, Huko kwingine hali Ikoje, Wahusika Tunaomba Msaada Kwenye Hili Wawasaidie Wakazi Wa Dodoma Kwenye Suala La Maji.
Itaisha siku CCM ikifa.
 
Nkuhungu yanatoka mara mbili kwa wiki, Maili mbili yanatoka kila siku Alfajiri(niliwahi kuishi kule kipindi cha nyuma ingawa kwa sasa sijui kama bado yanatoka vile vile)
Anhaa sawa na bei za kodi za vyumba zikoje huko nkuhungu na makulu.
N.B chumba kimoja self contained pamoja na sebule.
 
Kadi Za Ccm Mnarudisha Lini Maana Kule Mtwara Wameweza Chap Chap




Dodoma Magumu Yote, Kuna Mtu Anakaa Dodoma Kaenda Dar Kwa Matibabu
Hasa Macho Anasema Doctor Alipomfanyia Vipimo Tu Alimuuliza Unaishi Mkoa Gani?
Akamjibu Dodoma
Naona Vipimo Vinaonyesha Macho Yamejaa Vumbi Tupu
Alifikiria Huenda Kazi Zake Ni Za Kwenye Vumbi



Maji Yanatoka Jeshini Mzakwe Kwenye Visima Tangu Enzi Za Mwalimu Nyerere
Dodoma Dodoma Dodoma
 
Njoo msalato na makole hakuna shida ya Maji kabisaaa
Halafu kisasa miaka ya 2013 hakukuaga na shida kabisa hukoo sikuwahi ona maji yamekatika kabisa nashangaa siku hizi shida Nini Sijui idadi ya watu
Nililala nkuhungu nilihama mwezi tu wee maji kutoka mara mbili Kwa wiki Tena Masaa nane !narudi msalato umeme 24/7 maji sijawahi ona yakikatika ht Siku moja
 
To be specific kule nyumba 300 hata hayo masaa hawajui.. watu wamejaza madumu ndani kama wauza maji ikitokea yametoka tu ni wanasombelea ndani kama hayatatoka mwaka mzima imagine
Kweli nilienda kutembea siku Moja nilishangaa sana mi maisha ya shida ya Maji siyawezi maana sipendi kua na ndio nyingi ,nilihama nkuhungu mapema sana Bora nikae msalato ila nna hakika na maji na umeme mda wote
 
Hapa nilipo hatujawahi kukosa maji siku ya zamu yetu kutoka maji. Haijawahi kutokea. Pole Sana kwa huko ulipo.
Mi ratiba ilinishinda nikarudi zangu msalatooo shida tunaiskia kwenye Bomba tuu!!!Mimi ikitokea nimejenga Dom ntapambana niwe na Hela ya kuchimba kisima kabisa mi shida ya Maji siwezi kumiliki mindoo kama muuza samaki au mihogo au mtu wa hoteli hapanaa
 
Mi ratiba ilinishinda nikarudi zangu msalatooo shida tunaiskia kwenye Bomba tuu!!!Mimi ikitokea nimejenga Dom ntapambana niwe na Hela ya kuchimba kisima kabisa mi shida ya Maji siwezi kumiliki mindoo kama muuza samaki au mihogo au mtu wa hoteli hapanaa
😂 madjaba ni mengi kuliko vyombo vyote
 
Back
Top Bottom