Shida ya maji Dodoma itaisha lini?

Shida ya maji Dodoma itaisha lini?

Mgao n maeneo mengi kwa dodoma maji yanatoka saa 12 asubuhi hadi 11 jioni. Kwa kisasa nadhani na population inachangia kwa kiasi kikubwa.
Maji Dodoma tokea enzi za mwaalimu , maji hayapogi walikuwa wanatumia vijisehemu vidogo vilivyokuwa na maji sasa hakunaga maisha ndio hayoo .

Ila hata ukichimba kisima maji ni ya udongo
 
Nipo Hapa Kwenye Hili Jiji Linaloitwa Dodoma Mtaa Wa Kisasa (Nyumba 300), Kuna Shida Ya Maji Hadi Unajiuliza Kweli Hapa Ndio Makao Makuu Ya Nchi?

Wananchi Wa Hapa Hupata Maji Sometimes Mara Moja Kwa Wiki Ama Inaweza Ikatokea Yasitoke Kabisa Ndani Ya Wiki Nzima Mfano Kwa Muda Huu Ni Almost Wiki Mbili Maji Hayajatoka Na Ni Hapa Hapa Mjini.

Je, Huko kwingine hali Ikoje, Wahusika Tunaomba Msaada Kwenye Hili Wawasaidie Wakazi Wa Dodoma Kwenye Suala La Maji.
Mkuu huko hakuna shida ya maji.
Shida ya maji ipo Mpwapwa maeneo ya Ng'hambi,Chunyu ni hatari ! Dumu la lita 20 Tsh 700na maji yenyewe yanaharufu ya kinyesi cha punda,ngombe mbuzi yaani ni machafu hata uyapike vipi ukinyanywa ni kama unakunywa supu ya kongoro harufu yake
 
Nkuhungu yanatoka mara mbili kwa wiki, Maili mbili yanatoka kila siku Alfajiri(niliwahi kuishi kule kipindi cha nyuma ingawa kwa sasa sijui kama bado yanatoka vile vile)
Makulu ni kila siku
 
Ile kauli mbiu ya "maji kwa wote ifikapo mwaka 2000" ili ishia wapi? Ikafuautiwa "Ally Hassan Mwinyi apewe kura za ndio" "Maisha bora kwa kila mtanzania" "Serikali ya Viwanda" "hapa kazi tu" na sasa "RRRR" "nani kama Mama"

Halafu laghai yao ni kwamba ati adui yetu ni "Mabeberu" for sixty years hii laghai imeendelea.

Ukweli ni kwamba adui wa Nchi hii ni CCM.
 
Kila tapeli huwa hakosi slogans tamutamu.😂😂😂
 
Back
Top Bottom