Shida ni Mali??

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Ni dhairi kuwa hakuna binadamu ambaye uzaliwa na mali, hali kadhali, umauti unapomfika inakuwa ndio siku yake ya mwisho ya kumiliki mali alizozichuma hapa duniani. Kwa hali halisi, inaonekana kuwa matatizo yanayohusiana na mirathi yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku hasa kutokana mambo yafuatayo:
1. Pale Mume na Mke wanapoachana/ kutengana hata kama hawakuwa na ndoa (wameishi kama hawara) wakiwa tayari wamechuma mali na wana watoto.
2. Pale marehemu anapokufa akiwa ameacha mali nyingi
3. Pale marehemu anapokufa akiwa ameacha watoto wengi
4. Pale marehemu anapokuwa ameamua kurithisha mali zake kwa mtu/taasisi nje ya familia yake.
5. Pale marehemu anapokufa akiwa katika mahusiano yaliyotetereka (mgogoro wa ndoa)
6. Pale Mume mwenye wake zaidi ya mmoja wenye watoto anapofariki akiwa katika nyumba ya mmoja ya hao wake zake.
7. Pale familia ya upande ndugu wa Mume au Mke wanapokuwa masikini na kuishi kwa utegemezi.
8. Pale marehemu anapokuwa ameacha watoto wengi ambao wanaishi na familia zao katika nyumba za wazazi (wameoa/kuolewa na kuzaa wakiwa bado wanaishi katika nyumba ya wazazi wao).
Kwa vifo vinavyotokea katika mazingira kama haya, hata kama marehemu atakuwa ameacha wosia, bado kunakuwa na mvutano mkubwa sana wa familia kuhusu uhalaili wa huo wosis na urithi wa mali za marehemu.
Wapo wale ambao wanadiriki hata kuharibu/kudanganya juu ya wosia wa marehemu ilimradi wawemo kwenye orodha ya urithi na pia wapo wale ambao wapo tayari kutoa mtu roho ili waweze kuendelea kukalia mali za marehemu.
Zipo pia familia ambazo zimesambaratika kabisa kutokana na mambo ya mirathi na kuona kuwa Waume/Wake/baba/mama, au ndugu zao hakuwa na maana yeyote kwao hapa duniani kwa kushindwa kuwatambua katika urithi, hivyo kutowaenzi katika lolote lile mara baada ya kifo......
Tufanyeje sasa: tusiwe na mali, tusioe/kuolewa, tusizae, au tutafune mali zetu zoote kabla umauti haujatufika??
 
tuandike wosia tu basi..............

watu waache dhana kuwa ukiandika wosia unajichuria, mnasababishia familia zenu matatizo.
 
1.tuwe na mali,tuoe,tuzae na tutumie vema.
2.LAKINI,siku zote ishi kana kwamba leo ndio siku ya mwisho.kwa ajili hiyo utaandaa mambo na urithi wako vizuri
3.TATIZO TUNAISHI UTADHANI TUTAISHI MILELE.HATUWAZI YA KESHO.TUBADILIKE.
 
This is what I was talking kwenye topic ya Mke anatamaa ...na kama mtu atakuwa na mali nyingi ni bora kuweka lawyer na kila kitu kiandikwe kwenye paper, ukisha kufa kila mtu apewe haki yake..manake hiyo mali inaweza kukuchoma moto na utawaachia wenzako matatizo na kudhalilishwa...

Lakini watu hawapendi kuface reality... wanadhani wataishi forever...
 
Shida ni kubwa zaidi Afrika kwetu huku...Hata walioandika hapo juu, hawajaanda wosia!
Pia kwahali ya kimaadili ilivyo SASA, kuna hatari sana ya kuvuja kwa usiri wa contents za document ya WOSIA.
 
Shida ni kubwa zaidi Afrika kwetu huku...Hata walioandika hapo juu, hawajaanda wosia!
Pia kwahali ya kimaadili ilivyo SASA, kuna hatari sana ya kuvuja kwa usiri wa contents za document ya WOSIA.

na siri ikivuja tena tabu.....
na si wengi wanauwezo kuuweka wosia mahala ambapo patakuwa na uhakika wa kutovuja k
 
Pia watu tujitahidi kutafuta sisi kama sisi sio kutegemea mali ya ndugu au jamaa ..
kama kila mtu ana uwezo wake wa kujitegemea sidhani kama mirathi itakuwa inasumbua vichwa vya watu..
Mbona sioni nchi zilizoendelea watu wakigombea urithi??
 
Ni dhairi kuwa hakuna binadamu ambaye uzaliwa na mali, hali kadhali, umauti unapomfika inakuwa ndio siku yake ya mwisho ya kumiliki mali alizozichuma hapa duniani. Kwa hali halisi, inaonekana kuwa matatizo yanayohusiana na mirathi yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku hasa kutokana mambo yafuatayo:
ufanyeje sasa:[/B] tusiwe na mali, tusioe/kuolewa, tusizae, au tutafune mali zetu zoote kabla umauti haujatufika??[/SIZE][/FONT]




Swali lako la mwisho bwana ngoshwe limeniacha hoi

Tukitafuna mali zetu itakuwaje kwa wale wanaoacha kama una mke/mme/watoto wadogo ambao hawajaanza kujitegemea..\
Nachoona sio sahihi kwa mtu mwenye uweze wa kujitegemea kutolea macho urithi usiomuhusu..
Swala la msingi ni Wosia uwepo kwani hatujui siku wala saa ...
 
Andika Wosia... ni muhimu sana

Askofu,

Wosia huwa unatunzwa wapi? Kwenye briefcase pale nyumbani au benki au wapi? Maan wengine tukishapenda password inatolewa kirahisi (be it ya safe, briefcase, ATM, e.t.c)

Wasiwasi wangu ni kwamba wosia ukidondoka mikononi mwa wanyang'anyi unaweza kukuwaisha "mochwari"!
 
Ili wosia pia usilete matatizo nadhani ni vema kukawa na some sort ya guidline ya jinsi ya kugawanya mali ya mtu. Kuliacha hili libaki wazi tu kwa mtu kujiamulia kuna uwezekano mkubwa wa kutokea matatizo.
 
Swali lako la mwisho bwana ngoshwe limeniacha hoi

Tukitafuna mali zetu itakuwaje kwa wale wanaoacha kama una mke/mme/watoto wadogo ambao hawajaanza kujitegemea..\
Nachoona sio sahihi kwa mtu mwenye uweze wa kujitegemea kutolea macho urithi usiomuhusu..
Swala la msingi ni Wosia uwepo kwani hatujui siku wala saa ...


FLI, kwanza kabisa nadhani itabidi ubari hii Avatar yako sasa manake vijana wanakuja kasi na sie tushajizeekea tusije kuingia mkenge bure!.

Hoja nilizouliza zinatokana na visa vya kweli kabisa:


Kama ifuatavyo:
  • Baba ameishi akawa na mali nyingi, na alikuwa na wake wawili (mila inamruhusu) mmoja anawatoto wakubwa na mweingine wadogo, kaacha wosia ambao andaa kwa Mwanasheria na alimkabidhi mdogo wake atunze, siku alipokufa mdogo mtu akaja na wosia ambao unaelekeza mgao mkubwa kwa Mke wa pili, watoto wake na mama e mzazi. Familia ya mama mkubwa ikaja juu kuwa huyu Bwana mdogo kagushi wosia na kuwa alikuwa siku zote sambamba na mama Mdogo na ameonyesh sasa bayana baada ya kaka yake kufa anataka kurithi mke.
  • Kuna ndugu aliandika wosia, akiwa ana mali ambayo aliirithisha kwa dada zake wadodo watatu, mkewe na watoto wake. Kumbe wakati anakaribia kufa, zile mali hazikuwepo tena, ndizo zilizotumika kumuuguza akiwa mjini. alipokufa na kusafirishwa kwao, Mke akatika kupekua pekua akakuta huo wosia, siku ya kikao cha ndugu cha kumaliza msiba akautoa..hapo zogo kubwa likiaibuka kuwa mali za ndugy yao alizowarithisha zipo wapi mbona kwenye wosia zimetajwa lakini Mke anasema hazipo. Mke akabeba lawama kuwa amelamba mali zote.
  • Yupo mmoja aliandika Wosia katika kipindi ambapo ana mahusiano mazuri na mkewe na akampa rafiki yake kipenzi amhifadhie. katika orodha ya warithi, jamaa alitaja wanae wote (ambao walikwisha kuwa wakubwa), mkewe na mama yake mzazi. Mke wa rafilki yake ambae alitunza ule wosia akabahatika kuuona ule wosia akauchukua na kupelekea mke wa jamaa. Mke wa jamaa hakufurahishwa na kitendo cha jamaa kumweka mama yake katika orodha ya warithi wa sehemu ya mali. Akaanzisha timbwili kubwa, jamaa akapata shinikizo la dam. Lakini wakati akifa aliwaeleza nduguze kuwa mkewe ndie aliyemsababishia hayo na ndipo ndugu wakadai kuwa mke ndie kamuua na hasitahili kurithi chochote japo alitajwa katika wosia hata ikiwa kwa kuchanjana mapanga...
  • Baada ya mfarakano na mkewe ambaye alizaa nae watoto wanne, mume akaamua kwenda kuishi mbali akimwacha mke na wanae katika nyumba ya familia iliyokuwa na vyumba saba, huko akapata mama mwingine, akazaa nae watoto watatu. Kwa nia nje akaandika wosia, ambao uliwajumuisha watoto hao watatu. Katika huo wosia, alitaja kuwa watoto wote watarithi vyuma vya nyumba yake kwa usawa. wakati alipokuwa akiandik huo wosia, watoto walikuwa badao wadogo alipokuwa akifariki, baadhi yao walikuwa wameoa na kuolewa na wengine wakiishi katika nyumba ambayo wamerithishwa vyumba imerithishwa. Wakati wale watoto wa mama mwwingine walipodai kumilikishwa vyumba vyao, zogo kubwa likaibuka, yule mama mkubwa na wanae akidai kuwa hiyo nyumba haikuwa ya marehemu pekee yake na kuwa hata hivyo vyumba tayari watoto wake na marehemu wanaishi na familia zao. Hakuna mtu atayethubutu kuingia humo hata kama kuna wosia vingnevyo damu itamwagika kwani wao hawawatambui hao wataoto wengine....
 
Back
Top Bottom