Shibuda awashangaa wanaoogopa urais

Kwa mtazamo wangu, hawa wote wanaojitokeza hivi sasa kudai JK aendelee na kipindi cha pili wanatetea maslahi yao, kwani nani kawaeleza kuwa hatagombea!!!! Hawana lolote hawa, wanaelewa wadanganyika watamchagua tena, kwa hiyo wanajitengenezea mazingira ya bwana mkubwa kuwaona ataporudi madarakani.

Si hata Commandoo walikuwepo waliompigia debe ivunjwe katiba aendelee kwa kipindi cha tatu! Hata Mkapa walijitokeza wa kumpigia debe aendelee na kipindi cha tatu. CCM ni unafiki kwa kwenda mbele!

Mabadiliko nchi hii yanawezekana kabisa, tatizo letu ni ubinafsi ulipo kwenye upinzani. Wananchi wa Tarime na Mbeya Vijijini wameonyesha kuwa inawezekana, lakini wamkabidhi naniii, hapo ndio penye tatizo.
 
nauliza, hivi Mwinyi na Mkapa walikuwa na Upinzani kipindi cha Pili?..

Mkandara,

Sina uhakika kuhusu Mwinyi, ila Mkapa alikuwa apate upinzani ukazimwa kimya kimya!

Nitaandika kwa kirefu maoni yangu kuhusu hili la kuachiana panapo majaliwa!
 
Rev. Kishoka,
Tatizo sio kuwepo na Mpinzani ila tunazungumzia utaratibu wa chama hicho miaka yote ni kwamba rais aliyepo madarakani hupewa pass ya kurudia awamu ya pili unless kavurunda..
Sasa nashindwa kuelewa hizi habari za Kikwete asiwe mwakilishi pekee wa CCM zinatoka wapi?.. wanasema katiba ndio nauliza hiyo katiba ime kataza mgombea asirudie kipindi cha pili au kuna kipengele maalum kinachokataza kumpendekeza rais aliyepo madarakani kuwa mgombea pekee - Hakuna..
Kikwete hakuvurunda kitu chochote kiasi kwamba asipewe nafasi hiyo isipokluwa Kikwete ameshindwa ku deliver maendeleo kwa wananchi kama walivyoshindwa kina Mwinyi na Mkapa.. He deserve the same treatment kulingana na utaratibu wa chama hicho na kama Kuna mtu alijaribu kugombea wakati wa Mkapa na akazuiwa ndicho nachozungumzia kuwa ni utaratibu wa CCM kuwazuia watu wanaotaka kugombea dhidi ya mtu wanayemteua..Salim alikataliwa wakati wa Mwinyi awamu zote mbili..
Na kama sisi hatupendi kinachoendelea huko tuchague chama kingine why stick na CCM, kila kukicha CCM kama vile hatuna mfumo wa vyama vingi...
Sasa ni kina nani wenye mawazo mgando kama sio sisi kufikiria CCM tu ndio wanafaa kuongoza nchi.
 
Mkuu,

Hawa watu hapa chini ndio unategemea wamgeuke JK? Labda kama tunaota ndoto.

8. Ndugu Edward Ngoyai Lowassa - Mjumbe

11. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mjumbe

22. Ndugu Rostum Aziz - Mjumbe

25. Ndugu Andrew Chenge - Mjumbe

34 . Ndugu Zakia Hamdan Meghji - Mjumbe

Mtanzania,

Just imagine hizi kura tano hapo juu, what is their common denominator vile...?
 
Mtanzania,

Just imagine hizi kura tano hapo juu, what is their common denominator vile...?

Common denominator hapo ni Ni ufisadi, JK kawalinda wasifikishwe mahakamani, unafikiri wana hata nguvu ya kumpigira kura ya NO.

Umepatia kabisa, tunao wengi kwenye CC ambao hata kama rais ametoka nje ya kikao bado wanaweza kuogopa hata kutamka neno moja baya la kumgusa JK.
 
Mkandara,

Umenifanya nijibu hii hoja mapema ya utashi wangu. Sijali watakachoamua CCM, wakimchagua Kikwete sawa, wakimchagua mwingine sawa.

Ila sisi ni Taifa ambalo limeanza kujijenga katika mfumo mpya wa Demokrasia ya vyama vingi. Tumeona udhaifu uliotufikisha hapa tulipo kutumia chama kimoja na hata sasa tukiwa na vyama vingi.

Neno kuu lililotamkwa ni Utamaduni wetu, lakini je Utmaduni huu ni bora na unafaa katika Taifa linalotaka kujenga mfumo bora wa Demokrasia ambao lengo ni kuwa na uongozi na Utawala bora?

Jibu ni hapana, Utamaduni haujatusadia hata siku moja. Leo ni Kikwete, kesho ni kwenye jimbo la Ubungo, tutaambiwa tumuachie Keenja, ukija kule kwetu UK tutaambiwa tumuachie Msekwa na Mongela, kisa tuwaheshimu na ni Utamaduni.

Sasa makovu ya Utamaduni yameshakomaa hata kwenye Upinzani. Ukimpinga Mrema au Sefu, unafukuzwa uanachama, ukipingana na Mbowe, unaundiwa tume na kamati!

Sasa kama tutaendelea kusema ni Utamaduni bora, hatuoni kuwa unaleta Siasa Chafu?

Leo hii Nape aliondolewa kwa Mizengwe, mwaka 1995 waliondolewa kwa Mizengwe Kikwete, Msuya, Malecela. Mwaka 2005 waliondolewa kwa mizengwe Salim, Malecela na Dr. Bilali.

Sasa wakishaondolewa watu kwa Mizengwe, huja kauli za Utamaduni, na hivyo kumpa mtu anayeingizwa madarakani kwa Mizengwe, kibali cha kuongoza bila kupimwa kwa kipindi cha miaka 10 ndani ya chama.

Angalia Lipumba, Sefu, Mrema na Mtikila, wamekuwa wao ndio Miungu watu wa vyama vyao na huwezi thubutu kutoa neno dhidi yao kwa kuwa ni Utamaduni kuwaheshimu na kuwaachia wafanye watakalo!

Nakubaliana nawe kuwa kama kuna mwana CCM ambaye ana nia ya kweli kugombea 2010, basi achukue fomu, na aanze kampeni yake bila woga wa kutengwa na Chama.

Nao CCM kama wao ni watu wa Demokrasia, basi wajibu hoja za huyu anayegombania kuwawakilisha kwa kutaka kumuondoa Rais wa sasa na si kumtenga kwa vitisho au kutumia dola.

Leo Shibuda akija na kusema kuwa Kikwete hajafanya kazi ilivyopaswa kwa mujibu wa Ilani ya 2005, wana-CCM wamsikilize na si kumbeza kisa ni Utamaduni.

Nchi nyingi za Afrika zitashindwa kuwa na maendeleo ya kweli na Demokrasia kutokana na huu Utamaduni wa kuachiana! Anaboronga mtu, wanashindwa kumwambia kweli na kumpa upinzani kwa kuwa mtu huyo huyo ndiye anayewapa mlo na sauti.

Kama miuondo ya vyama vya Siasas Tanzania vingeachana na mfumo butu wa Wagombea kuteuliwa na CC au NEC, tungeona wigo wa fikra na kampeni ukipanuka na hivyo kuongeza Demokrasia na kujituma kwa kujizatiti.

Leo hii nikiwa alosto nikaingia Ikulu ya Dar, nina uhakika nitakaa kipindi cha miaka 10 bila wasi wasi na hata nikivurunda namna gani, hakuna atakayenotoa maana tayari kuna utamaduni.

Ni haki yao CCM kuwa na utamaduni huu, lakini je ni sawa kwa jamii yetu na wengi wetu ambao ndio wapiga kura tusio na nafasi au sauti ila kutimiza tunacholazimishwa?
 
Rev. Kishoka,

CCM wafanye kile walichokifanya kwa wagombea ubunge na udiwani. Hiyo nafasi iamuliwe na wananchama nchi nzima.

Ninaamini kama hilo zoezi litaenda kwa wananchi, kutakuwa na ushindani mkubwa ndani ya CCM.

Ila mimi sishangazwi na kauli za Malecela na wazee wengine na pia kauli zao si katiba. Kama kuna wananchama wengine wanataka kugombea naona wanaweza kugombea tu.

Tatizo langu ni hiyo CC kuwa na uwezo mkubwa wa kufyeka majina ya watu kwa lengo moja tu la kusafisha njia kwa ajili ya mtu wanayemtaka.
 
Mkandara na Mtanzania,

On second note, nadhani maneno ya Mwalimu Nyerere kusema Upinzani imara utatoka CCM haukuwa na maana ya kusubiri kila miaka 10 dnipo kuwe na mabadiliko ya falsafa kutokana na mgombea wa urais, bali ni aliye mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania/Zanzibar, kupata upinzani wa hoja, sera, itikadi na utendaji wakiwa madarakani na hata wakati wanapogombea kwa mara ya pili.

Tukirudi kwenye utamaduni, jiulizeni ni vipi Tanzania inashindwa kusonga mbele ukianzia kwenye ngazi za Ujumbe wa nyumba kumi, shina, kata, kijiji, tarafa, wilaya, manispaa na hata mkoa kutokana na Utamaduni?

Mnakumbuka yule kijana wa Kairuki aliyeenda gombea Kawe dhidi ya Adamjee na Rita Mlaki, aliangushwa kwa ajili ya mizengwe na utamaduni!

Warioba alipata upinzani na kwa ajili ya utamaduni Wasira (Tyson) akaondolewa kwenye mchakato kwa mizengwe na kumlazimu kuingia upinzani ambapo alishinda uchaguzi.

Watu kama kina Chenge, Mramba, Sefu Khatibu, Lowassa, Keenja, Malecela, Msuya, Msekwa, Mzindakaya, Mwakawago, Bilali, na wenginewe ambao wamekuwa wabunge na wawakilishi kwa muda mrefu, wamenufaika sana kutokana na "Utamaduni" mpaka siku walipoamua ama kwa binafsi yao au kukosana na walio katika hatamu za Chama ndipo waliporithiwa viti vyao au kupata Wapinzani.

Mzee Malecela mwaka ule wa go to hell, Lawrence Gama alivyokumbana na Nchimbi, na hata Kasaka na Kimiti, umaarufu wao uliingia mchanga kutokana na kuwapo kwa mgongano wa fikra na kimaslahi kati yao na tabaka la uongozi na ndio maana wakaishia kupata upinzani kwenye majimbo na hata kuangushwa ndani ya vikao vya chama!
 
Rev. Kishoka,
Mkuu nimekusikia sana na hata siku moja huwezi kubadilisha utamaduni kama huna utamaduni bora zaidi kwani demokrasia husimama tu pale chombo cha Taifa kinapoafikiana na mageuzi hayo..Mkuu ni lazima tukubali reality. Sii wote walioukubali UJAMAA na utamaduni wake wote ulokuja nao. Na kati ya utamaduni wa Kijamaa hata Nyerere mwenye kuna mambo hakukubaliana nayo akayabadilisha na kuifanya sheria ya nchi.. Wapo watu hawakupenda pia ma pengine ilikuwa kinyume cha Ujamaa as Socialism, Ukomunist au Ujamaa wa Kiafrika.
Utamaduni wa demokrasia na uchaguzi wa viongozi wetu hauwezi kubadilika leo au Kesho na wala watu kama sisi hatuwezi kuubadilisha isipokuwa kwa vigezo ambavyo vinatupa sisi mamlaka ya kufanya hivyo - Ni kura zetu..
Maswala ya Mrema na Mbowe kuweka vikao kuhusiana na watu wanaopingana nao ni swala la chama na mara zote ni muhimu kwetu kutambua utamaduni wa chama husika..

Tofauti za uongozi ndani ya chama unaweza kutokana na matusi, kubeza na hata kusema chama kimefilisika kifikra na kadhalika huwezi kuachiwa huru ati kwa sababu unatoa challenge. Tatizo la siasa Tanzania watu wengi wanaopinga uongozi wa nchi au chama hutumia watu wengine kukizungumzia chama na pengine sisi ni wepesi wa kutukana kwani Shibuda kawaita wazee wa Shinyanga wana mawazo mgando.. haya ni matusi, hawa wazee ni moja ya jimbo waliofikia maamuzi hayo..hivyo Shibuda alitakiwa kuzungumza kuwakilisha hoja yake na sio kutukana wazee ambao wana kila haki ya kumteua Kikwete kama mgombea pekee kutokana na hoja iliyopo mbele yao.. pengine nao hawaoni kiongozi bora zaidi ya Kikwete ndani ya chama hicho kama navyoona mimi..Ni utamaduni wa maoni. hadi sasa hivi wanachama na wananchi hawajalazimishwa kumchagua Kikwete..

Nachosema mimi, utamaduni wa Mchagga (CCM) ni kunywa Mbege siwezi kutoa hukumu kwa sababu ya tamaduni za nje inayokataza kunywa Pombe na hata kama pombe ni haramu na ina madhara...Uharamu wa pombe hiyo upo nyumbani kwangu, na nitahakikisha nyumbani kwangu mbege hainyweki lakini siwezi kuingia nyumba ya jirani ambaye ni Mchagga na kumfundisha utamaduni..
Kama Chadema leo watasema Mbowe atapita bila mpinzani nitauliza sababu, nitatazama katiba na utamaduni wetu kwani sii lazima utamaduni uambatane kimaandishi ndani ya katiba..

Ni baada ya kupitia sehemu hizi zote ndipo naweza kupima tena uwezekano wa Chadema kushinda bila Mbowe, kitu ambacho hakipo kwenye katiba wala utamaduni wa chama isipokuwa - Ushindani nje. Je, Chadema wanaweza kushinda Uchaguzi 2010 bila Mbowe? ni muhimu sana kwangu kwa sababu dhamira kubwa ya utamaduni huu wa uchaguzi ni kupata Ushindi..Pamoja na yote haya siwezi kutumia lugha ya matusi kudhoofia hoja ya wanachama wengine..
 
Ndugu Yangu Mkerewe, na sikitika saaana tena saana kwa jinsi unavyo taka kuhalalisha kitu kwa kutumia Neno Utamaduni, lakini ukumbuke katika maisha kitu hiko kinatokana na mazingira ya wakati huo. Eg zamani tulikuwa na chama kimoja, lakini ukweli wa wakati umetupeleka kwenye vyama vingi, hapo zamani tulikuwa tunavaa kama watindiga, tuseme kwa wanawake kipande cha nguo kuficha sehemu muhimu za mwili, leo hii, watu wana vaa kuanzia, sketi, gauni, kitop mpaka suruali. Zamani watu walikuwa na utamaduni wa kubwia ugoro, sasa hivi watu wanavuta sigara. Kwa hiyo neno utamaduni unatakiwa ulitumia vizuri, sio kulikariri tu. Na Nime furahishwa saana na Majibu ya Reverend. kuhusiana na hilo neno Utamaduni wa Msekwa na Mongella etc so nakuomba usitishe matumizi ya neno utamaduni kujustify jambo lisilo na tija katika maisha ya Mtanzania wa Sasa na hata hili la kusema Shibuda amewatukana wazee wa Shinyanga ni jitihada zako za kutaka kuhalalisha kitu unacho kitaka.
 
Rev. Kishoka,

CCM wafanye kile walichokifanya kwa wagombea ubunge na udiwani. Hiyo nafasi iamuliwe na wananchama nchi nzima.

hii sheria itapitisha baada ya JK kushinda 2010.

kwani hata mwinyi si ali ruhusu uchaguzi wa vyama vingi baada ya yeye kuondoka.

embu fikiria mjumbe angesema na hii sheria itumike kwa rais na JK yupo hapo anamsikiliza..........
 
Katiba ya CCM, ilochapishwa kusambazwa na kuwezesha kila mwenye macho kuisoma, inasaidia kuwarubuni walio kua Wakoloni wetu kuendelea kutupa misaada ili kutatua upumbavu wetu.

Katiba halisi inayotumika kuendesha mambo ya kila siku ya CCM ambayo huonyeshwa ndani ya vikao by implication ni tofauti na hiyo ya kwanza hapo juu.
Katiba hiyo ilojaa Ufashist na udikiteta kama siyo Ushetani ndiyo kioo na mwanga wa kuionyesha dira CCM.

Huko ndani ya vikao wazee wenye mvi hunguruma kama simba dume kwa hasira , huku macho yao yakiwakazia wenye thubutu yakiwa na nia ya kudhuru mwili na roho, nyuso zao hukunjana na kuweka mawimbi ya ndita na kufanya nyuso zao zifanane na vigagula watambuzi wa wachawi kwenye ngoma za wanga. Mambo yote hayo hufanywa hali migongo yao imepinda mithili ya nyau anyejihami na shingo zao kuonyesha kuelemewa na uzito wa vichwa vyao vikubwa na vizito vyenye kujaa kila aina ya upumbavu ulogandamana kwa miaka takriban 48 ya Uhuru.

Wale waliopo ndani ya CCM wamedumu humo kwa vile tu mlo wao unategemea kuienzi CCM na kuvumilia machungu ya hasira yake. Vinginevyo sioni cha kuwaweka humo.
Kingunge na hata Kikwete mwenyewe wasingeona haya kurudisha kadi za CCM kwa sababu hekima yote ndani ya CCM imechojolewa, chama kimebaki uchi.
 
Last edited:
- Ahsante mkuu, mimi ni Capitalist sasa kama unaijua vizuri it is about individualism, misifa sifa yangu ni part of it na mwenyewe unakubali kuwa I got the juice, hapa it about taifa kwanza punguza jazba, hii ni forums tu! Naomba kukurekebisha, huwa nina dataz za kila sekta sio CCM tu comeon! you know that!

- By the way, Pasaka njema kwa wana-JF wote, na familia zenu popote mlipo, Mungu awajaze baraka na busara zaidi za kulisaidia taifa letu. Sasa ni wakati wa kumpa nafasi Mungu, safari kidogo, tutaonana tena next week Mungu akipenda, salam kwa familia na wote huko majumbani wakuu!

Pasaka Njema!

Respect.

Wazee wa sauti ya umeme FMES!

Wazee wa sauti za umeme easter njema na familia pia.sasa ukirudi na wewe uache jazba manake huwezi kuona kibanzi cha kwenye jicho la mwenzako wakati kuna boriti kwako
asante mkuu
 
August,
Mkuu wala usisititike wewe, nasikitika miye hapa Mkerewe ambaye nalazimika kumkubali Msekwa na Mongella kwa sababu wananchi wamewachagua.. Wapo wagombea wengi sana wamejaribu dhidi ya hao wazee lakini sisi ndio tunaboronga na sio CCM..Na sidhani kama hata kuchaguliwa kwao kulitokana na utamaduni wa Wakerewe kwa sababu CCM imewapitisha hao..Wakati huo huo utamaduni wa Wakerewe ktk chaguzi za MaChief -mara zote hutokana na koo ya Utemi kina Ruhumbika, Lukumbuzya na mtu kama miye husubiri yule aliyeteuliwa na kumpa heshima zote. Katika uteuzi huo kuna katiba yao na taratibu ambazo zinakubalika ingawa hazikuandikwa mahala..

Ni utamaduni ambao pengine siukubali lakini ndio hekima ya wazee wangu kufahamu yale nisiyoyafahamu inabidi niheshimu maamuzi hayo..Kama vile Michelle Obama alipomkumbatia Queen au Pbama kumsalimia Sultan wa Saudia. Ni swala la mimi kukubali tamaduni za watu wengine na kuzipa heshima yake.

CCM wana utamaduni wao na mimi kama sii mwanachama wa CCM nalazimika kuziheshimu hata kama zina matatizo.. CCM wameweza kuwaweza kusimamisha kina Kighoma Malima, Mwaikembe na wengineo kwa sababu tu walitaka kukihama chama. Ni utamaduni wao kuwaondoa wapinzani ndani ya chama. CCM walimkwamisha Kikwete< salim, Malecela na wengineo wengi tu toka chaguzi za kata hadi urais -ni utamaduni wao mimi sina sababu ya kuupinga wakati sii mwanachama, ndio sababu ya kuleta mfano wa Wachagga.

Lakini pamoja na utamaduni wao huo mchafu bado nina choice, natazama utamaduini wangu miye, kutokuwa na vyama vingi haina maana huo ni utamaduni uliopitwa na wakati, kuvuta sigara badala ya Ugoro sii utamaduni mpya na mengineyo yote haya yanatokana na choice zangu...bado wapo watu wanavuta Ugoro na wengine wanavaa kaniki isipokuwa kwa design inakwenda na wakati..Nenda ktk michezo ya baseball utaona wachezaji wakivuta ugoro, Majuzi tu Valentino katoka design ya gauni akitumia gunia na watu wanavaa..Wamasai wanaendelea kuvaa lubega haina maana wanapungua kitu fulani ktk uchaguzi wao, ikiwa lengo kubwa ni kuuficha Uchi..

jambo muhimu hapa ni kwetu sisi, wana JF kutambua kwamba ktk list ya uongozi wa juu wa CCM hao CC ni watu ambao hakuna hata mmoja wao anayeweza kusimamia maslahi ya Taifa acha mbali kumchagua Kikwete. sasa ikiwa Kamati kuu ni watu ambao hawana muda wala fikra za kukuendeleza wewe itasaidia nini kama watamweka mgombea mwingine dhidi ya Kikwete?..
Na mtu huyo nani ambaye atakuwa anapingana na qualifications za hao wakulu wa CC, na akapitishwa kugombea..Jibu ni HAKUNA na HAIWEZEKANI.. sasa wewe na mimi kwa nini tupoteze muda kuomba mgombea dhidi ya Kikwete ndani ya utamaduni ambao haukubaliani na fikra zetu..Waacheni wachague Kikwete kisha sisi tujipange na utamaduni wetu.. wananchi wenyewe wataamua kwani majibu yao ndio Final..Kesho CCM watajifunza na kubadilisha utamnaduni huo lakini kama wataendelea kushinda kwa nini wabadilishe! Lengo la uchaguzi wowote ni USHINDI sasa kama wapata Ushindi tena wa kimbunga kwa nini wabadilishe mfumo!

Utamaduni mpya hautokani na chaguzi za watu ndani ya CCM isipokuwa ni utamaduni mpya ni Mfumo wa vyama vingi..Tatizo la mada hii inatazama mfumo wa wagombea wengi badala ya mfumo wa vyama vingi kuwa solution ya matatizo kama haya..
 
Urais wa Tanzania si mali ya mtu au kikundi cha watu wachache wanaotaka kumtetea Rais abaki madarakani hata kama kuna ushahidi wa kutosha kwamba utendaji wake haukufikia mategemeo waliyokuwa nayo Watanzania.

Watanzania wengi tulikuwa na imani kubwa na ahadi za Kikwete lakini baada ya kuwa madarakani kwa miaka minne inaonekana ahadi hizo zilikuwa ni hewa maana hakuna hata moja iliyotekelezwa. Wanaotaka Urais ni lazima wajue kwamba utendaji wao ni lazima uwe wa kuridhisha ili wawe na uwezekano wa kurudi katika awamu ya pili vinginevyo awamu moja tu kama wananchi hawajaridhika basi ukae pembeni ili mwingine naye ajaribu kuiongoza nchi yetu. Katiba ya CCM inaruhusu yeyote yule ambaye ni mwanachama hai na anatimiza masharti ya kuwa Rais wa Tanzania kugombea nafasi hiyo kupitia chama chake. Hivyo kutaka kutumia vitisho na ubabe ili kupindisha katiba ya CCM na kumtetea kiongozi ambaye utendaji wake umekuwa finyu kamwe ni lazima kupigwe vita na Watanzania wote wanaopenda maendeleo ya nchi yetu.
 
Mkandara,

Sasa kama tutaendelea kusema ni Utamaduni bora, hatuoni kuwa unaleta Siasa Chafu?

Leo hii nikiwa alosto nikaingia Ikulu ya Dar, nina uhakika nitakaa kipindi cha miaka 10 bila wasi wasi na hata nikivurunda namna gani, hakuna atakayenotoa maana tayari kuna utamaduni.

Ni haki yao CCM kuwa na utamaduni huu, lakini je ni sawa kwa jamii yetu na wengi wetu ambao ndio wapiga kura tusio na nafasi au sauti ila kutimiza tunacholazimishwa?

Naam kuna watu wanaotaka kutetea utamaduni huu potofu bila kuangalia athari yake kubwa kwa nchi yetu.
 
nauliza, hivi Mwinyi na Mkapa walikuwa na Upinzani kipindi cha Pili?..

Mfumo mzima hautoi nafasi kuleta upinzani hata kama watu wangetamani vipi.
Hata 2010 tusitarajie mabadiliko maana ndio utamaduni tayari na itakuwa muujiza kama rais atatawala kipindi kimoja tu.

Chama chake kitafanya kila liwezekanalo kuhakikisha awamu ya pili nayo inapatikana maana tukumbuke kuna wadau wengi sana wenye interests mbalimbali na unfinished business hivyo kwa pamoja watapambana na kila anayeonyesha upinzani iwe ndani au nje ya chama.
 
Naam huo ndiyo ukweli kabisa WoS watapambana naye hata kama kufanya hivyo hakuweki mbele maslahi ya Tanzania na Watanzania. Huu utamaduni potofu ndiyo inabidi tuupige vita kwa nguvu zetu zote.
 
Back
Top Bottom