Shibuda awashangaa wanaoogopa urais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda awashangaa wanaoogopa urais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Apr 10, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,481
  Trophy Points: 280
  Shibuda awashangaa wanaoogopa urais

  Thursday, 09 April 2009 16:30

  Na Peter Masangwa

  Majira

  MBUNGE wa Maswa (CCM), Bw. John Shibuda ameshangazwa na kitendo cha Kamati Kuu ya Mkoa wa Shinyanga kutoa tamko katika Jimbo lake kuwa Rais Jakaya Kikwete ndiye mgombea pekee katika uchaguzi wa mwakani.

  Akizungumza Dar es Salaam jana, Bw. Shibuda alisema kitendo hicho kinafanywa na wanasiasa wenye mawazo mgando na maoni yaliyopauka kwani mwana demokrasia hawezi kuthubutu kukandamiza katiba kwa kiasi hicho.

  "Inasikitisha sana kwa mtu kama Shibuda niliyeonesha nia ya kugombea urais kuwachanganya watu namna hii na kuanza kujihami kwa kutoa matamko na kufanya maandamano kushinikiza kuwa mgombea abaki kuwa Rais Kikwete," alisema Bw. Shibuda.


  Alisema kuwa demokrasia bila utii ni wendawazimu kwani kitendo cha kumtisha kwa jinsi hiyo haitabadili utashi wake wa kugombea urais kwani anaamini kile anachokisimamia.

  Bw. Shibuda alisema tamko la CCM linasema milango iko wazi kwa mwanachama mwenye sifa kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho lakini tamko la Mkoa wa Shinyanga linasema mtu akijitokeza atafukuzwa.


  "Viongozi ndani ya chama na nje ya chama wanahitaji kufundishwa haki elimu za kiraia ili wajue na kuisemea demokrasia na si kukurupuka kwa kujikosha kwa kiasi hicho," alisisitiza.

  Alifafanua kuwa kitendo chake cha kuonesha nia ya kugombea si kuwa Rais Kikwete hafai na wala hajafanya kazi ila anatambua kazi yake, hivyo kugombea kwake ni jambo la kikatiba na kidemokrasia na kuwaonya wanaojaribu kuvunja katiba kwa kiasi hicho.

  Je, kama Rais Kikwete angekuwa na huruka kama Bw. Idd Amin wananchi wangekubali kumpa vipindi vyote viwili?" Alihoji Bw. Shibuda.

  Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Shinyanga juzi ilitoa tamko kuwa mgombea urais wa chama hicho atakuwa Rais Kikwete kwani ndiyo utamaduni waliojiwekea.

  Pia Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam imeunga mkono Rais Kikwete kuwa mgombea pekee kwa tiketi ya chama hicho.
   
 2. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0  Kwi kwi kwi...mbavu zinauma kwa kicheko...
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,481
  Trophy Points: 280
  LOL!...Si unajua mambo ya 'utamaduni wa kuachiana' tulimuachia Mwinyi vipindi viwili, tulimwachia Mkapa vipindi viwili na sasa tumwachie Kikwete kwa vipindi viwili. Mwaka 2009 kweli nchi itaendeshwa kwa 'utamaduni wetu wa kuachiana'. Naam hayo kweli ni mawazo mgando ambayo hayaendani na wakati.
   
 4. S

  Semjato JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2009
  Joined: Jun 26, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  sawa,hawakuwa sahihi mheshmiwa Shibuda...but sio wewe unaefaa kugombea kwa tiketi ya CCM pia bado...neeeeeeeext!
   
 5. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Afadhali ya Shibuda ameonesha ujasiri wa kusimama kwenye kugombea na Muungwana... Ni wachache wanaojua haki zao za kidemokrasia ndani ya CCM!
   
 6. M

  Mpingo1 Member

  #6
  Apr 10, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wapo watanzania wengi ambao wangeweza kugombea, lakini wanatakiwa kujipima kwanza kwa hatua waliyoifikia hadi sasa.
   
 7. mwakatojofu

  mwakatojofu JF-Expert Member

  #7
  Apr 10, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  shibuda angekuwa waziri pangekuwa patamu zaid

  mambo yetu mengi hayaendi tunavyotarajia au kwa kasi ya kuridhisha. kuna matatizo mengi sehemu nyingi ambayo yanahitaji msukumo kutoka kwa mkuu wa kaya. kwa kukosekana huo msukumo hali inabaki hivyo hivyo kutwa kucha. hii inasababishwa na ukweli kuwa bado sis hapa tz rais ana madaraka na ushawish mkubwa katka mambo mengi sana

  shibuda au mwingine atayetokea aje atuambie mapungufu yaliyopo sasa na jins atakavyo yakabili. asisahau kutuambia jins atavyoendeleza kidogo kilichopatikana au kuanzishwa
   
 8. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  stop prejudging shibuda....
  ni kura ndio itakayoamua kama shibuda hafai na sio keyboard yako..

  wewe semjato ni mawazo mgando
   
 9. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hivi JK kama mwenyekiti wa chama hapaswi kukemea uvunjwaji wa katiba yao? au ndio kauli yake ya chini chini kusafisha njia. Kauli kama hizo hazimaanishi kampeni? maana wapinzania huzuiliwa kupiga kampeni mpaka kipindi cha uchaguzi sasa hii mijadala haina connection na kampeni??? Kinacho shangaza hawa viumbe, sikuzote huwa wanachagua mgombea wao kwa utaratibu mzuri tu hata bila wananchi kujua kama wanautamaduni wakupeana vipindi viwili sasa kunashada gani safari hii kupiga mkwala watu wasijitokeze kugombea ili muungwana akose upinzani?? Hii inaonyesha dhahiri kuwa huyo candidate ni kihiyo na hawezi kuuzika bila kutumia nguvu.
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Apr 10, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  nauliza, hivi Mwinyi na Mkapa walikuwa na Upinzani kipindi cha Pili?..
   
 11. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145

  mdogo wangu amezaliwa 1985 na amegraduate tiyari, kama mtoto wako amezaliwa 1985 sasa hivi atakua amegraduate na yeye.
  Hiyo ni kukuambia tu tokea nyerere alie 1985 na kusema kama si mwinyi nani mwingine angeshika, dunia imebadilika sana, internet imeshika hatamu, google, tv zimebadilika, ukimwi umepamba moto, richmond, dowans, uwanja mpya wa taifa, moi kaondoka madarakani,RUKSA, DECI,KIWIRA, MWINYI KALA KOFI, VIJISENTI, ukitaka kula nguruwe uchague alie nona, youtube, na bila kusahau JAMII FORUMS.

  KWA HIYO LAZIMA UTAMADUNI CCM IBADILIKE UWENDE NA NYAKATI.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Apr 10, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Semilong,
  Inaonyesha wazi kuwa unachanganya mchuzi hapa.. nachouliza mimi ni candidates vipindi vya pili kati ya Mwinyi na Mkapa kulingana na katiba ya chama CCM.. Wewe unazungumza kwa mapana ya taifa na kutofikira kwamba katiba ya chama ni ile ile toka wakubali maximum ya uongozi ni vipindi viwili..Pamoja na kuundwa vyama vingi bado utaratibu ni ule ule ndani ya chama hicho..
  Sasa kama kulikuwepo na Mpinzani aasimama pamoja na mapendekezo ya Nyerere kwa Mwinyi au Mkapa nambie.. Ikiwa kila mmoja wao alipitishwa bila kupingwa ktk kipindi cha pili, naomba kuelemishwa kwa nini leo kwa JK iwe issue..
  Huyo mdogo wako hata kama kazaliwa 1985 ame graduates na kadhalika bado ni mdogo wako, wewe mkubwa kwake utaendelea kuwa mkubwa kwake hadi kaburini kwani ndiyo katiba ya Mwenyezi Mungu..
   
 13. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #13
  Apr 10, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Ndiyo.
  Kwa kumbu kumbu zangu nakumbuka Mwinyi alikuwa na upinzani kwa term la pili na mpinzani wake alikuwa kivuri.

  Mimi nafikiri kama JK anatakiwa naye apewe kivuri agombee naye kama akina shibuda wanakataliwa.
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Apr 10, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  MkamaP,
  haaa haaa haa! unajua niliposoma hii mada mwanzo nilifikiria huyu Shibuda kajitokeza kugombea, kumbe naye anapendekeza JK against Kivuli..,
   
 15. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #15
  Apr 10, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  kwa heshima yako naomba u-copy na u-paste sehemu ya katiba ya chama cha mapinduzi inayosema lazima rais aachiwe vipindi viwili.
  Ndio maana wenzako wanasema utamaduni hawatumii neno katiba, kwa ajili katiba ya ccm haisemi hivyo.
  Sasa hivi ni ulimwengu wa ushindani, sasa hivi unaona ya kikwete lakini rais anayekuja atakuwa na ushindani zaidi ya kikwete.
  Mkandara uwelewi kama dunia na tz kwa ujumla vimebadilika na ndio maana nikatumia neno nyakati. You cannot keep 40m people quite forever.......
   
 16. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #16
  Apr 10, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Mkandara,
  Ndiyo mwaka 2000 kuna jamaa alitaka kusimama kugombea against Mkapa; huyu jamaa alikuwa anaishi nje ya Tanzania. Aliitwa pembeni na kuambiwa asigombee amwachie Mkapa. Hebu kumbuka wakati ule yule kichaa mwenekiti wa Umoja wa Vijana wakati ule aliposimama na kuja juu kupinga mtu yeyote atakayetaka kugombea U-Rais against mkapa basi ni adui wa CCM. Mkapa alisimama na kusema kuwa mtu yoyote ana haki kugombea U-Rais ingawa hakutokea mtu yoyote baadaye.

  Zama za Mwinyi? that was another era; chama kimoja, hata hayo mawazo yalikuwa ni dream; mwenyekiti alikuwa ameshika hatamu na zidumu fikra zake!!
   
 17. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #17
  Apr 10, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Hakuna haja ya uchaguzi bongo,hata uchaguzi ukifanyika ni upotevu wa fedha tu.

  nafikiri tunapoteza mda kuwaelekeza hawa jamaa njia mbadala ama plan B ya maendeleo ,wakati kiuhalisia hawa jamaa wanafahamu vizuri sana kuliko sisi jinsi ya kuleta maendeleo na jinsi ya kuendesha demokrasia ya kweli.Swali kwanini hawafanyi hivyo basi jibu ni wakimletea maisha bora babu na jamaa yangu nafasi zao zitakuwa ktk hali tete.
  Kifupi ni kuwa Viongozi wetu wanajitahidi kujenga utawala wa Umwinyi/ubeberu/ukabaila ili vizazi vyao viendelee kuwapo na kuwpo na kuwapo,yani sawa sawa unapopata mtoto kwanini unampa surname ya familia?
   
 18. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #18
  Apr 10, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  katiba ya mungu ni kwa ajili ya manufaa kwa watu wote na haimzuii mdogo wangu kupata pesa au kuwa na elimu zaidi yangu.

  Lakini katiba ya ccm ni ya elite wa ccm na sio kwa manufaa ya watu wote. Na ndio maana wanafanya juu chini ku maintain status quo.

  katiba ya mungu inamruhusu mdogo wangu kushindana na mimi lakini ingekuwa ndani ya ccm angejaribu kushindana na mimi ningemuita yeye ni adui wa familia na atengwe
   
 19. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #19
  Apr 10, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133


  Yuko sahihi, majority ndani ya chama hicho hawajui hata maana ya siasa ambayo kwayo wao ni waumini. Shibuda ajue kuwa hayuko sehemu sahihi. Ule uamuzi wa wagombea binafsi umefinyangwa mpaka kesho?

  Hapa ndipo ninapochoshwa na mawazo ya wanaCCM. Ni wakati mwafaka wakajaribu kuona kama utaratibu huo umesaidia nchi au CCM tu?


  All the same, unafiki mtupu!!
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Apr 10, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,603
  Likes Received: 18,637
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono ujasiri wa Shibuda kujitokeza kutaka mahitaji ya demokrasia ndani ya chama, yatekelezwe. Hii ndio demokrasia ya kweli.

  Japo Shibuda anajua yeye siyo serious contender, lakini atempt ni haki yake kichama na kikatiba, why not use it?.

  Moja ya matatizo makubwa yetu sisi Watanzania, ni not having a daring heart. Hatuna uthubutu wa kufanya mambo na ndio sababu wengi wetu tumekwama.

  Maadamu Shibuda has guts to dare, lets support him hata kama ni mbio za sakafuni, lakini at least he tries.
   
Loading...