mwana wa africa
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 548
- 128
jaribuni mfe! Hivi mnamuonaje Shibuda? Mnamchukulia simple sana,sasa mkimtimua Chadema atahama na kwenda chama kingine na mtakutana bungeni.Mbowe take it frm me.yaonyesha kuwa Shibuda si mmojawapo wa CDM. Hana taarifa na yanayofanywa na WanaCDM kama wabunge. Yupo yupo tu kama mtu aliyekosea njia. Kama hayo ni maoni binafsi je na posho anachukua!!??
Kwa sababu ametofautiana na wewe. Tatizo chenu si chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa kuwa kingekuwa hiko kingestawisha fikra huru na kukubali mtawanyiko wa mawazo. Haiwezekani chama kikaendekeza ukiritimba wa mawazo kiasi kwamba mtu akija na fikra zilizo nje ya wigo wa Slaa au Mbowe anahesabiwa kama muasi. Hizi si enzi za zidumu fikra za mwenyekiti. Hakuna sababu ya kubinya uhuru wa kujieleza. Mkishika nchi mtakuwa madikteta.huyu muheshimiwa ana ka ugonjwa kanakoitwa BIPOLAR DISORDER.
Kwa hiliCDM wanadhihirisha utoto wa kiwango cha juu. Mbona CCM wengine wamepinga suala la posho na wengine kama Makamba wameunga mkono lakini hatujawaona wakiitisha press conference za kizembe kuwafundisha watu jinsi ya kufikiri. Nawaambia na narudia tena. lazima muwe makini sana na jinsi ya kushughulikia tofauti za mawazo. Vinginevyo mtauharakisha mwisho wenu.Kwa hili naona sasa viongozi wa CHADEMA watajifunza kwamba kuna umuhimu kuwachunguza kwa makini watu wanaotaka kuwapa dhamana ndani ya chama. Huyu jamaa alishakuwa wa hovyohovyo tangu bado yupo magamba na wasipomdhibiti mapema ataleta shida nyingi sana huko mbele. Mimi binafsi simpendi mtu huyu!
Imefika muda sasa Wasukuma kutoka kanda ya ziwa kuachana na CDM chama cha kikanda na kikabila, Shibuda ananyanyashwa kutoka na Usukuma wake angekuwa ametoka kaskazini wala usingesikia maneno yoyote ya kashfa! Shibuda nakushauri ili swala kawashitakie wazee wa Kisukuma kama ulivyomshitaki Wenje, kwa wazee wa Mwanza na wazee wakakuelewa kama Wenje ni Mkenya hawana tena shida nae amalize kipindi chake aende zake kwao Kenya, Wasukuma mnaona mnavyodharauliwa na CDM.Mbona kina Selasini wanaipongeza CCM kila siku ata siku moja hawajaguswa au kwa sababu ni Wachagga!.
JF, kuna watu wana akili masizi kama huyu, ngoja nikuulize kwa hiyo Mungu yupo Chadema?mshikaji unajua kila siku huwa unatema pumba mpaka basi. mi nadhani umefunga ndoa na magamba na ujue Mungu atakuchoma moto kwa kuendekeza tamaa mbele
hali ya mambo ndani ya chama cha democrasia na maendeleo chadema si shwari baada ya mbunge wa maswa magharibi, john shibuda, kuwatolea uvivu viongozi wa juu wa chama hicho, akisema hatishiki na vitisho vinavyofanywa na viongozi hao, alisema kutokana kutoka na hali hiyo, yuko tayari kufukuzwa katika chama kwa kosa la kusema ukweli siku zote, hivi karibuni amfadaiwa kwenda kinyume na msimamo wa chama chake, kuhusiana na suala la posho za wabunge,kitendo ambacho kimemfanya aonekane muasi ndani ya chamana hivyo kuundiwa tume ya kumchunguza. shibuda alibeza shutuma hizo na kuwataka viongozi wa kumuomc radhi hata hivyo atandaa mikutano ya hadhara kuwaeleza wanainchi tabia ya viongozi hao(mbowe na zitto)..... nukuu MTANZANIA la leo
Mkuu naona unaongelea watu wawili tofauti, unaeleza habari za Mpendazoe halafu unamtaja Shibuda, aliyetoka CCM na kwenda CCJ kisha Chadema ni Mpendazoe na kwa sasa sio mbunge, anayesuguana na Chadema kwa sasa ni Shibuda na ndo mbunge wa Maswa Magharibi.Ndugu zangu katika hali ya siasa sijawahi kumuona mtu asiye na adabu wala hekima kama Shibuda. Shibuda alianza kwa kumtishia rais Jakaya kuwa angeweza kugombea na kumuondoa katika utawala ndani ya ccm. Baada ya kuona kuwa anaota ndogo za alasiri,aliamua kuchanga hela ya kumchukulia mh.rais fomu za kugombea urais. Shibuda aliamua kuhama ccm kwa kukejeli na kurusha vijembe vya ajabu ajabu kwa mwenyekiti wake wa zamani mh.Kikwete,akaenda chadema akapata ubunge. Alipoambiwa afuate masharti ya cdm ya kuisusia hotuba ya yule aliyesema hana uwezo wa kumuongoza na kuliongoza taifa,bado akaendelea kukataa na kuhudhuria. Pia akaudhuria sherehe ya kumwapisha waziri mkuu wakati chama chake kilipinga. Akaja katika maandamano ya cdm akawaponda na kuwadharirisha mh.Nape, mwakyembe na mzee sitta kuwa ni wanasaliti,wanafiki na ndumila kuwili kwa kuwa ni wanachama na waanzilishi wa CCJ. Watu wakajua siri nyingi zilizojificha katika nyoyo za wanaccm hawa. Pia kawaharibia uaminifu na uadilifu katika ccm. Kama haitoshi Shibuda alipewa ilani ya chadema ambayo pia ndani yake inayokataza kuwa na posho zisizo na mashiko pamoja na kuyakataa mashangingi,kama 'punguani' ameenda bungeni na kupinga hadharani na anataka posho ipande. Cha ajabu hata ccm kupitia waziri mkuu wameweka wazi kuwa posho zitaondolewa au kuunganishwa na mishahara ili ikatwe kodi. Sasa Shibuda anaipinga cdm akiwa ndani na anaipinga ccm akiwa nje,alaf anadai vyama vingne ni mamluki,je shibuda anasimama wapi? Kwa kumpinga Zitto na mbowe,nape,jk,6,mwakyembe,sasa anataka tuone kuwa yeye tu ndo yuko msafi??! Chadema ichukueni kadi ya shibuda muiweke makumbusho. Shibuda hatapata mwenyeji mwingine kwa tabia zake za ajabu. Kabla hapajakuwa na harakati za kudai haki sawa,zamani wazee wetu wangesema Shibuda ana tabia za kike. Ila kwa kuwa ishaonekana sio sahihi kuwasema wanawake,basi hata mi sitasema ivo. Shibuda kama ni mti basi ni mpapai,hafai kwa kujengea,hafai kwa kuni,hafai kwa kuchomwa hata mkaa,zaidi hatofaa hata kujengea daraja. Siwezi kumuita shibuda mamluki ndani ya cdm ila namuona kama mtu anayekosa malezi na kuota sharubu. Chadema muweke kando uyu mtu,arudishe kadi,turudi kwenye uchaguzi ili hata ikiwezakana twende maswa kama ccm na cdm kuwaomba wananchi kura bila ya kuwa na shibuda. Mwache aende kama mgombea binafsi au hata ajiunge chama cha tatu kama watamwitaji. Taifa lisisumbuke na mtu uyu maana alipotoka ccm tukajua labda kachoshwa, kaenda ccj hakukaa,kaja cdm na sasa analeta maajabu. Iyo inaonesha kuwa yeye ndo mwenye vilema. Chadema mfukuzeni Shibuda.