Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,277
- 105,478
Ni makosa kuchagua mbunge kwa misingi ya chama achaguliwe kwa uwezo wake hata kama ni mgombea binafsi.
Until tutakapokuwa na sheria ya kuruhusu mgombea binafsi, kumchagua mgombea kwa uwezo wake binafsi tu, bila kujali falsafa za chama chake ni kutafuta matatizo. Vipi kama mgombea anaamini ubepari na chama kinaamini usoshalisti na somehow ameweza kupata ugombea kwa style hii ya "kutemwa na CCM na kwenda CHADEMA" ? Huoni kwamba hapa kumchagua huyu kutakuwa ni kupika majungu tu ? Kesho mgombea ataingia mjengoni na kutoa siasa zake kichwani ambazo zinapingana na manifesto ya chama, migogoro itakuwa haiiishi.
Haya ndiyo matatizo ya nchi changa ninayoyaongelea kila siku, watu hatuna institutions tunaenda na personalities tu. Kama ni hivyo tuondoe na katiba kabisa, tuondoe vyama, turudi kwenye uchifu tu, siku Kikwete akiwa bored akijisikia kuchinja wapinzani awachinje tu.
Si tunafuata uwezo wa mtu bwana? Hamna rule of law, hamna institutions, hamna procedures, kila kitu kitokane na mtu tu.
Sikatai kwamba kuna umuhimu wa kuwa na wagombea binafsi, ili watu kama mimi ambao hatuna chama na hatuoni chama cha kuunga mkono tuweze kushiriki katika kuchaguliwa. Lakini hili halina maana kwamba kama hatuna mgombea binafsi, mtu yeyote wa mrengo wowote anaweza kuingia chama chochote cha mrengo wowote, akapiga gabfest, akakubalika. This is a recipe for disaster.
Mgombea akishakubali kuwa nominated na chama fulani, ana wajibu wa kutekeleza manifesto ya chama. Sasa ni lazima kuwe na ndoa kati ya mawazo ya mgombea na manifesto ya chama.
Huwezi kusema umchague mufti wa Baghdad aende kuwa Askofu wa wakatoliki wa Roma, eti kwa sababu tu mufti huyu ana uwezo wa kuongoza watu. Utakuwa huna akili, utakuwa unataka kusababisha mgogoro mkubwa kabisa wa utendaji.
Kwa hiyo hii habari hii, hii habari ya kumchagua mtu kwa uwezo wake inaweza ku make sense kama tu tuna sheria ya kuruhusu wagombea binafsi, kwa sasa hivi kwa sababu hatuna sheria hii, labda kama tunataka kuchagua watu kwa uwezo wao tu tufikirie zaidi kuileta hii sheria ya kuruhusu private candidates, maana si haki kuwadhulumu watu kama mie nisiye na chama haki hii ya msingi.
Lakini usiseme tuwachague wagombea wa vyama kwa maoni yao tu, bila kujali miongozo na manifesto za vyama vyao. Hii itakuwa kituko kikubwa sana.