Mzee wa Rula
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 8,169
- 3,359
Jamani maneno aliyoyatoa Shibuda na makofi aliyokua anapigiwa na ccm, ni dhahiri amenunuliwa kuiua CHADEMA. Alikua akiimba mashairi aliyokua ameyandaa kwenye karatasi bila hata spika kumwambia asisome kama kananu inavyotaka. Kimakusudi alipomaliza Cheyo nae akafanya kama alivyoagizwa na ccm afanye. Hali inatisha, yaani mbunge badala ya kuchangia hoja zenye maslahi unaanza kwa kuwasema wengine kana kwamba hawajui wamo mle kufanya nini, hii maana yake ni nini?
Hata mimi maana nikitaka kupata flow yake nashindwa maana hajamaliza hiki karukia hiki yaani vurugu tupu!Hata mie nimemsikia ila kweli sikuweza kuelewa anasema nini na nini ni msimamo wake kweli umenikumbusha MAHOKA
Jamani maneno aliyoyatoa Shibuda na makofi aliyokua anapigiwa na ccm, ni dhahiri amenunuliwa kuiua CHADEMA. Alikua akiimba mashairi aliyokua ameyandaa kwenye karatasi bila hata spika kumwambia asisome kama kananu inavyotaka. Kimakusudi alipomaliza Cheyo nae akafanya kama alivyoagizwa na ccm afanye. Hali inatisha, yaani mbunge badala ya kuchangia hoja zenye maslahi unaanza kwa kuwasema wengine kana kwamba hawajui wamo mle kufanya nini, hii maana yake ni nini?
Baba mpinzani kuleta mipasho ni aibu kwani kila wakati wanatakiwa kutoa vitu vya kuumiza vichwa na si mipasho. CCM tumewazoe mbona jana Komba kalala na leo kafuka moshi balaa kwenye kikao lakini siyo habari lakini angekuwa mbunge wa CDM kalala sijui ingekuwaje? Kuwa mpinzani ni kazi siyo lelemama!Watu wengine wapumbavu sana... Mbona ccm wanafanya mipasho ham semi acheni mambo ya kipumbavu
Alianza kwa kushukuru kama kawaida lakini baadae ni kama alikuwa mshahiri hivi kwa jinsi alivyokuwa akiongea mpaka kengele inagonga akaomba aendelee kama wabunge wataridhia.
Kiujumla siwezi kumquote accurate lakini alikuwa kama mahoka kwa jinsi alivyokuwa akichangia hoja bila mwelekeo. Haaaaah Shibuda ukiendelea hivi sijui kama utafika mbali?
Ni kweli huku akijua kuwa nguzo kubwa ya CDM ni vijana amewaponda wabunge vijana kuwa wawe na busara na kuwa wazee ni hazina, yaani hata nimeshindwa kuwa specific ya yale aliongea lakini kwa tuliomuona amefuka Moshi sana.Baada ya kikao cha Bunge kuahirishwa Katibu wa wabunge wa CDM John Mnyika aliomba wabunge wote wakutane.Nadhani suala la Shibuda litakuwa linajadiliwa.To me Shibuda ni wa kusimamishwa ubunge na kama ikiwezekana Kamati Kuu ya CDM imtimue mara moja.Kwa kilichojitokeza leo bungeni ni fedheha kubwa.Shibuda ni makapi na hafai kuwa ndani ya CDM