Shetani anawapepeta vijana kadri atakavyo, vijana wanakufa wakiwa wadogo. Acheni dhambi vijana hamtatoboa

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,703
36,143
Hello!

Tangu kale na kale vijana, wazee, watoto na watu wa Rika zote wanakufa lakini sasa hii trending ya vifo vya vijana ina walakini.

Nimetafakari kwanini vijana wanakufa sana, kijana anakufa anawaacha wazazi wake wakiwa na nguvu, kijana anakufa anawaacha bibi na babu zake wangali hai.

Mungu kanipa jibu kuwa dhambi ndizo zinawaua vijana mapema. Mimi sijui ni dhambi gani, nimeambiwa tu dhambi ndio sababu kubwa.

Acheni dhambi vijana mtakwisha na kuwaachia wazazi wenu makovu moyoni. Kijana anasoma anahangahikiwa kazi anaanza kazi tu anakufa.

Kijana mwingine anaoa tu anakufa. Kijana mwingine anamaliza ujenzi wa nyumba yake anataka ahamie umauti unamkuta.

Acheni dhambi vijana, naongea katika Roho.
 
Hongera sana mkuu uko sahihi, dhambi inaua Mambo mengi sana, uchumi, kazi, maisha, na mengine mengi sana, acha wa kubeze lakini huo ndio ukweli,dunia Ina waovu wengi sana, fanya yaliyo sahihi, Linda moyo wako, maana hakuna anayekupa mbingu hapa duniani,Leo tuko wengi, ukifika unaenda mwenyewe, acha na na vijana wa hovyo, wanaotoa majibu yasiyo na adabu.
 
Mungu na atusaidie..Nimekuelewa sana.Ambae hayajampata hawezi kuelewa.Mwaka huu tumezika wawili kwenye familia moja ndan ya miez sita..chanzo ajali na homa zisizoeleweka.
Mungu atie nuru katika macho ya vijana
 
Tatizo vijana wa sasa wanapenda sana kuiga mambo ya hovyo hovyo ya westerners wanadhani ndio ujanja kumbe upumbavu na dhambi tupu. Sasa kama hilo li Manara Haji, ndani ya miaka 10 limeshakua na wanawake wanaofahamika si chini ya 8, sasa hio ni nini? Na vijana wanavyopenda tigo =dhambi.kiukweli vijana wanaisha sana kwa kukosa maarifa. Tigo si ujanja ni ufirauni tu huo.
 
Kila nafsi itaonja mauti c kijana ,Mzee Wala mtt.

Ushaenda hospital mkuu ujue wtt wangap wanaozaliwa wanakufa Kwa cku, na hao nao wakufa Kwa sbb ya dhambi au .
 
Kila nafsi itaonja mauti c kijana ,Mzee Wala mtt.

Ushaenda hospital mkuu ujue wtt wangap wanaozaliwa wanakufa Kwa cku, na hao nao wakufa Kwa sbb ya dhambi au .
Well said Mkuu!
Takwimu zake sio sahihi
 
Naona watu wa rika lako wadogo kumbe nyote mmekuwa watu wazima ....Umri wa miaka 25 sio mdogo
 
Ninafikiri kama taifa tumetenda dhambi pia labda ndiyo maana maisha yetu yanazidi kuwa magumu.
kila siku. Dhambi tunazotenda ambazo zinamchukiza Mungu ambazo tunatakiwa kutubu na kuacha ni kama hizi hapa.

1. Uzinzi na uasherati vimeongezeka sana. Hii dhambi ni chukizo sana mbele za Mungu inaleta laana, balaa na mikosi tuntakiwa tutubu

2. Wizi wa mali za uma. Wafanyakazi wengi wa serikali wanalijua hili na ni chukizo mbele za Mungu kunahitajika toba mbele za Mungu.

3.0 Rushwa katika kutoa haki. Watu wanapoteza haki zao kwa ajili ya rushwa ili nalo ni chukizo mbele za Mungu tunatakiwa tutubu.

4.0 Huu wizi wa kura unaotokea kila uchaguzi na kuwaweka watu madarakani kwa wizi ni dhambi mbele za Mungu na ni chukizo. hii tunatakiwa kutubu

5.0 Mwaka 1967 Serikali ilichukua mali za watu bila ridhaa yao wakisema wanatangaza Azimio la Arusha. ili nalo halimpendezi Mungu na kama Taifa tunatakiwa kutubu.

6.0 Uvivu ni mwingi sana na watu wanakaa tu bila kufanya kazi. Hii nayo ni dhambi mbele za Mungu. Asiyefanya kazi na asile.

7.0 Ulevi nao umeongezeka nao ni chukizo mbele za Mungu. angali familia nying zinauwa maskini maana baba siku zote analewa nalo hili tuntakiwa toba.

Mimi ni hayo tu unaweza kuongezea mengine.

Kama hatutatubu tutegemee maanagmizo zaidi kutoka kwa Mungu.

2 Nya 7:14 SUV​

Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
 
Mtumishi umeongea Kwa hisia sana, Ila Katika kitabu cha 50 cent kazungumzia hayo mambo ya kuishi maisha yenye mtindo wa usafi ili kuweza kuyapa maisha yako maana
Screenshot_20231212-121215.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom