Sheria zinaruhusu uchinjaji wa mifugo kwenye maeneo ya Ibada kisha kugawiwa hovyo kwa raia?

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
4,138
10,539
Siku mbili nyuma nimeshuhudia tukio ambalo serikali imelikalia kimya ila lingeweza kuleta madhara makubwa sana kwa Jamii.

kondoo zaidi ya mia 4 zimechinjwa bila kufuata taratibu za kiafya na kisha kugawiwa kwa raia!

Je, hii mifugo ilikuwa salama kiafya haikua na magonjwa yoyote?

serikali ilituma wawakilishi wake kusimamia usalama katika machinjio yale yasiyokuwa rasmi?
 
Sheria zinataka uchinjaji wa wanyama kwa ajili ya matumizi ya umma (jamii au watu wengi) ufanyike chini ya usimamizi wa afisa mifugo au afisa afya wa eneo husika.

Kuna makosa huwa tunayafanya kutokana na mazoea. Nadhani hilo ulilolizungumza linaangaukia hapo.

Miaka kadhaa iliyopita nilikua nafanya kazi kwenye kata fulani kama afisa mifugo, moja ya majukumu yangu yalikua ni ukaguzi wa nyama (meat inspection).
Nakumbuka nimeshiriki kukagua nyama inayochinjwa kwenye misiba, sherehe za makanisani, n.k

Ikumbukwe kuwa nyama ni miongoni mwa vyakula ambavyo vinapaswa kuangaliwa usalama wake kabla ya kuliwa. Hi ni kwa sababu nyama hiyo inaweza kuambatana na madhara makubwa kwa walaji endapo wanyama waliochinjwa watakua na aina fulani za maradhi.

NB: Natambua kwamba hayo uliyoyaeleza "makosa yaliyozoeleka", ni kama vile kuendesha gari bila kufunga mkanda, au kuendesha pikipiki bila kuvaa kofia ngumu kichwani.

Lakini msimamo wa sheria uko hivyo nilivyoeleza hapo juu (as far as my experience matters).
 
Kwahiyo kila anayechinja mnyama nyumbani kwake,wewe unatakiwa uende ukahakiki?

Ingekua hao wanyama waliochinjwa ni Nguruwe hii thd ingeanzishwa hapa JF?
 
Siku mbili nyuma nimeshuhudia tukio ambalo serikali imelikalia kimya ila lingeweza kuleta madhara makubwa sana kwa Jamii.

kondoo zaidi ya mia 4 zimechinjwa bila kufuata taratibu za kiafya na kisha kugawiwa kwa raia!

Je, hii mifugo ilikuwa salama kiafya haikua na magonjwa yoyote?

serikali ilituma wawakilishi wake kusimamia usalama katika machinjio yale yasiyokuwa rasmi?
Kama lengo ni kujua either walikuwa sawa au hawakuwa sawa kuchinja hao wanyama na kugaia watu basi Naomba nikupe majibu

Serikali haikukaa kimya kama unavyodhani, bali ilikuwa ishamaliza taratibu zote ambazo wao walipaswa kuzifanya ili kuhakikisha usalama wa raia wao

Kinachofanyika ni kwamba, mtu alieamua kujitolea kununua wanyama na kuwachinja ili agaie watu, lazima aende Halmashauri husika kuonana na mkurugenzi

Kwakuwa lengo ni kutoa msaada/suna/zawadi Sijui wenzangu waislamu wanaitaje hii kitu watanisadia, hivo mkurugenzi hutoa taarifa kwa Maafisa Mifugo waliopo chini ya Halmashauri yake na sehemu ambayo tukio litatokea

Baada ya hapo hutolewa kibali Maalimu ambacho hutoa ruhusa ya kuchinja wanyama sehemu tofauti na machinjioni na kukabidhia hao watu ambao wataendesha hilo zoezi

Na taratibu zingine za ukaguzi huanza rasmi baada ya hao wanyama kuwasiri, ambapo kama zoezi la uchinjaji ni kesho, basi leo hii hao wanyama watakaguliwa wakiwa hai ili kujiridhisha kama watafaa kwa kuchinjwa

Na siku ya tukio zoezi la uchinjaji litaendelea likiwa chini ya Afisa Mifugo wa Eneo husika akishirkiana na wengine katika ukaguzi wa wanyama watakaochinjwa, na baada ya zoezi kimalizika Maafisa mifugo walioshirki hupewa pesa pamoja na nyama kama Asante

Kwahiyo nikutoe hofu mkuu, Serikali ilikuwa na taarifa zote na wakajiridhisha juu ya usalama wa wanachi wao
 
Kwahiyo kila anayechinja mnyama nyumbani kwake,wewe unatakiwa uende ukahakiki?

Ingekua hao wanyama waliochinjwa ni Nguruwe hii thd ingeanzishwa hapa JF?
Kuna sehemu nimeandika kwa ajili ya MATUMIZI YA UMMA, JAMII AU WATU WENGI.

Kama huwezi kuelewa hapo basi naomba hii mada tuachane nayo, tujadili mambo ya Simba na Yanga.
 
Siku mbili nyuma nimeshuhudia tukio ambalo serikali imelikalia kimya ila lingeweza kuleta madhara makubwa sana kwa Jamii.

kondoo zaidi ya mia 4 zimechinjwa bila kufuata taratibu za kiafya na kisha kugawiwa kwa raia!

Je, hii mifugo ilikuwa salama kiafya haikua na magonjwa yoyote?

serikali ilituma wawakilishi wake kusimamia usalama katika machinjio yale yasiyokuwa rasmi?
Ni hatari kwa afya ya walaji tunaweza chukulia kimzaha mzaha ila kama kulikuwa na mnyama mgonjwa hapo baadae ingeunda tume kuchunguza
 
Back
Top Bottom