Sheria Ya Ndoa

Msanii

Msanii

JF-Expert Member
Jul 4, 2007
6,987
2,000
tatizo tunalolipata hapa ni hicho kitu kinachoitwa tafsiri.
Nategemea kufunga ndoa hivi karibuni na mtarajiwa wangu ni mwanasheria hivyo tulikuwa tunapitia hatua kwa hatua kuhusu haki na wajibu a wanandoa. na pia hata mambo ya kuwekana kinyumba ambayo yanafanyika sana siku hizi na watu hawajui madhila yake ila nawashauri mfungue ile link aliyotoa Mwanakijiji in firt page ya thread hii kisha angalieni mambo yooote maana ukipata matata usije ukalalama kuwa sikujua....

Ila bado nina quarel na kutajwa Tanganyika badala ya Tanzania. Je ina maana hata draftsman ni kilaza?? miaka yote hii hakuna marekebisho hata ya kisarufi??? my god
 
S

Stone Town

Senior Member
May 28, 2007
108
195
Asalamu alaykum.

Kwani hamjui kuwa Zanzibar ina sheria zake na Bara na sheria zake? hata kama wamo wabunge lakini kuna baadhi ya wizara sio za muungano kwa hivyo mambo mengine yanakuwa ni ya Bara tu na Zanzibar wana Baraza lao la wawakilishi kama vile Bunge kwa hivyo wao hurekebisha sheria zao huko barazani na zile zinazohusu muungano ndio hupelekwa bungeni na kujadiliwa na wote yaani Tanzania nzima.

Sheria za kurithi na kila kitu zipo wazi kabisa.

Kwa kwa nini mtu azae nje ya ndoa ovyo? wakati kuna ndoa za kidini na kimila? inakuwaje hasa kutaka kuwakosesha haki watoto wako?

Mtoto anajisikia mchonge wenzake wanapojitambulisha kuwa baba yao fulani na mama fulani akijiangalia yeye anasema wazee wake hawajaowana... inatia huzuni sana
 
P

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
45,048
2,000
Jamani Hizi Sheria Zimenifurahisha Sana ,,,kuna Swalai Nauliza Kuna Ndugu Yangu Walioana Na Mwanamke Na Baada Ya Miezi Sita Wakatengana ,,baada Ya Hapo Mwanamke Akakimbilia Mahakamani Baada Ya Miezi Saba Mahakama Ikatengua Ndoa Ile,,,baada Ya Miezi 7 Kuachana Mwanamke Anapiga Kumkumbusha Mumewe Bado Nakupenda Na Ndoa Ya Kikristo Haivunjiki,,embu Tusaidiane Kidogo Hapo Jamani
Hapo Ndoa Ipo Au Lah.,,,,,,???????????????????
 
S

Stone Town

Senior Member
May 28, 2007
108
195
Kwa swali hilo rudi kwenye kitabu chako cha dini kinakufundisha nini? ikiwa unasema wamefunga ndoa ya kikristo si uende huko kanisani ukaulize au kwa aliyekufundisha ndoa atakupa ufafanuzi wote bila ya kuhangaika kutafuta sheria zinasema nini kwa sababu ndoa inayofungwa kidini ni ahisi sana kusolve kuliko zile ndoa za kimila na zinazofungwa bomani bila ya dini.

laiti ingelikuwa binaadamu anapopatwa na matatizo yoyote anarudi katika kitabu kitukufu anachikifuata basi bila ya shaka kusingekuwa na matatizo maana kila kitu kimeelezwa ndani ya kitabu lakini tatizo letu tunaiga mambo ya kizungu badala ya kufuata mafundisho ya dini zetu.
 
Mushobozi

Mushobozi

JF-Expert Member
Aug 20, 2007
543
195
katika swala la ndoa, ndoa za mila ndoa za kikristu na ndoa za kiislamu zate zinafungwa kwa niaba ya serikali. ndiyo maana wanaofungisha ndoa wote lazima wawe na certificate ya serikali akiwa ni pamoja na padre shehe au mchungaji.

swala la kutenganisha ndoa, ni mahakama tu yenye mamlaka ya kutenganisha ndoa ikiwemo kuangalia sababu ambazo haziwezi kustahimirika. hivyo hata zile taraka tatu za kiislamu hazifanyi ndoa kuvunjika kisheria kama hiyo ndoa haijatenganishwa na mahakama. hata kama wakristu huamini kuwa anayetenganisha ni mungu tu, sheria ya ndoa ya mwaka 1971, haijui hilo.
 
C

Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,329
0
msichana miaka 15 si mtoto..msipoteze muda kujadili..acheni ya fikra ya kudefine mtoto miaka 18....mtu mzima anaanza miaka 15..so far mwanamke anapevuka akili kabla ya miaka 15.Wafunzeni watoto mapema mambo ya kijamii acheni Uzembe wa Kulea.
 
M

mwehozi

Member
Nov 5, 2007
9
0
tunaangalia sheria ya ndoa inavyosema. mtoto wa miaka 15 ni mtoto kwa maana kwamba ukiLALA NAYE UTAKUWA UMEBAKA AWE AMEKUBALI AU LA. hii inatolewa na SOSPA=sheria za mabadiliko ya kujamiana.

ila katika kufunga ndoa sheria inatoa mwanya kidogo kuwa unaweza kufunga ndoa ilimradi tu wazazi wake waafiki. yeye anachukuliwa kama mdogo katika kutoa maamuzi. ila baada ya kufikisha miaka 18 anaweza kukataa na kuacha ndoa kwamba yeye haafiki na ile ndoa.
 
Augustoons

Augustoons

JF-Expert Member
Oct 31, 2007
411
195
Jamani Hizi Sheria Zimenifurahisha Sana ,,,kuna Swalai Nauliza Kuna Ndugu Yangu Walioana Na Mwanamke Na Baada Ya Miezi Sita Wakatengana ,,baada Ya Hapo Mwanamke Akakimbilia Mahakamani Baada Ya Miezi Saba Mahakama Ikatengua Ndoa Ile,,,baada Ya Miezi 7 Kuachana Mwanamke Anapiga Kumkumbusha Mumewe Bado Nakupenda Na Ndoa Ya Kikristo Haivunjiki,,embu Tusaidiane Kidogo Hapo Jamani
Hapo Ndoa Ipo Au Lah.,,,,,,???????????????????
Bwana Pdidy,hao ndugu zako sijui walifunga ndoa ya namna gani japo baadhi ya facts kwenye swali lako zinamiss nitakuambia.Kutengana si kuvunja ndoa watu wakitengana bado ndoa yao ipo hai,hapo ni separation tu.Na kama baada ya miezi 7 mahakama ilitengua ndoa,nashindwa kuelewa kama ilitoa talaka au ilitengua ndoa kwa maana ya kutengua,kutengua ndoa ina maana nullity of marriage,kwa maana nyingine kati ya hao watu wawili kisheria hakukua na ndoa kutokana na kukiuka taratibu fulani za kisheria,hivyo basi kama kuna nullity order ina maana wanaweza kuoana tena kwa kurekebisha makosa.Na nullity inatokana na mambo mengi likiwemo nani consumation of marriage,yaani tangu kufunwa kwa ndoa hawakuwahi kuingiliana au mmoja wao alikuwa akikataa.Kama ni talaka basi hao wameachana hakuna tena kusema swala la nakupenda tena aah,kikristo sawa hawa watu bado wanandoa hadi mmoja wao afariki lakini kiserikali ndoa kati yao haipo,japo kikristo ndoa ikitenguliwa kwa maana ya nullification hata kwenyewe hakuna ndoa. Kanisa linatambua nulity of marriage na sio divorce.
 
Mushobozi

Mushobozi

JF-Expert Member
Aug 20, 2007
543
195
safi sana Augustno
Pdidy, tukiongezea hapo, ndoa zote za kikristu zinafungwa kwa niaba ya serikali. na hata hao mapadre na wachungaji hufungisha ndoa kwa vibali mahalumu kutoka serikalini.

swala kuwa mahakama ilitengua ndoa hata kama ilikuwa ya kikristu, imetenguliwa. wanaweza kurudiana na kufanya mapenzi kama kawaida ila litakapozuka jambo kama vile kutengana tena na mmoja wao kutaka mali zilizochumwa kugawana, au mambo ya miradhi, kuwa ndugu wa mme wamemnyang'anya mali, mahakama haitatambua hata kama zimechumwa sana.

ndiyo mahana mahakama huwa haitengui ndoa hovyo hovyo mpaka sababu zilizoorodheshwa kwenye vifungu vya 36 na 39, 'voidable marriage' na 107 vya 'void marriage'

pia kifungu cha 100 kinaitaka mahakama ijidhishe bila mashaka yoyote kuwa ndoa haiwezi kuimarika katakata. it has broken ireparably

na ili kuhalalisha hii, basi kuna mabaraza ya usuluhishi reconciliation boards ambayo yatajaribu kufanya hivyo ila yakishindwa yatatoa certificate kwa mlalamikaji aende nayo mahakamani kudhihirisha kuwa usuruhishi umeshindikana.

voidable marriages zinapewa annullment, na yale ambayo ni void yanapewa decree of divorce.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,933
2,000
Naamini Mkandara ulikuwa unaulizia hii. Nimesearch hapo juu kutoka threads alizoanzisha bongolander.. duh.. tumetoka mbali.!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom