Sheria ya Ndoa inasemaje kuhusu mali zilizochumwa kabla ya ndoa?

Mbalamwezi1

Mbalamwezi1

JF-Expert Member
2,071
2,000
Kabla ya kuoa ulikuwa na mali zako ulizomiliki kama nyumba, gari na ardhi(shamba). Ukaja kuoa baadae mkazinguana na mwanamke mkatalikiana.

Sasa katika kugawana mali; je, zile mali ulizochuma kabla ya ndoa zitahusika ktk mgawanyo?! Msaada tafadhali wanasheria wasomi
 
kabwigwa

kabwigwa

JF-Expert Member
744
1,000
zinahusika mkuu labda Kama hazijui akizijua imekula kwako
 
C

chororingo

Member
77
125
Hamna kitu kama hicho. Mali ulizopata kabla ya ndoa haziingii kwenye mgawanyo wa Mali.
 
Mbalamwezi1

Mbalamwezi1

JF-Expert Member
2,071
2,000
zinahusika mkuu labda Kama hazijui akizijua imekula kwako
Duh!hasa km ndo hivi mwanamke akigundua una mali si anaweza akajilengesha kwako akatia drama na maigizo ili mwanaume uone umepata then unamuoa kumbe yy analenga mali zako tu,ukishamuoa anaanza kuzingua ili mgawane mali.Hii naona km imekaa vbaya hv!!
 
lemidius mbalwohi

lemidius mbalwohi

Senior Member
104
195
Jasho lako kabla ya ndoa ni lakwako pke ako labda kma mlishirikiana kuviendeleza wte ktk kpnd cha ndoa S.38 of Law of marriage Act cap 39 R.E 2002
 
Mbalamwezi1

Mbalamwezi1

JF-Expert Member
2,071
2,000
Ukweli ni upi sasa hapo wakuu zinahusika ama la!!
 
Mbalamwezi1

Mbalamwezi1

JF-Expert Member
2,071
2,000
Jasho lako kabla ya ndoa ni lakwako pke ako labda kma mlishirikiana kuviendeleza wte ktk kpnd cha ndoa S.38 of Law of marriage Act cap 39 R.E 2002
Asante mkuu!Je,kuna mwenye tofauti na hili wajuzi wa mambo?
 
Stunt

Stunt

Senior Member
124
250
Jasho lako kabla ya ndoa ni lakwako pke ako labda kma mlishirikiana kuviendeleza wte ktk kpnd cha ndoa S.38 of Law of marriage Act cap 39 R.E 2002
Upo sahihi sana
Sheria ya ndoa nadhani ni mojawapo kati ya sheria zinazohitaji kuwa reviewed, ipo biased sana.
Ukiwa na mali yoyote kabla ya ndoa na ikawa imeandikishwa kwa jina lako, itahesabiwa ni yako, ukioa, kama mkeo hajawahi ijua na hajawahi kujishirikisha kwa namna yoyote ktk mali hiyo itahesabiwa ni yako mkitengana, lakini tu, akijishirikisha vyovyote vile na mali hiyo, itahesabiwa amehusika kuiendeleza na mtagawana 50/50.
Mali zote mlizopata mkiwa ktk ndoa, na zikaandikwa jina la mume, mtagawana 50/50, lakini tu, ikitokea mmezipata mkiwa ktk ndoa, na zikaandikishwa kwa jina la mke, itahesabiwa kuwa ulimpa zawadi, na ni "transfer of ownership" na kwakweli hizo hupati hata senti tano.
ANGALIZO; Kuweni makini na mali mnazowaandika wake zenu!!!
 
Lukaku Tanzania

Lukaku Tanzania

JF-Expert Member
839
1,000
Jasho lako kabla ya ndoa ni lakwako pke ako labda kma mlishirikiana kuviendeleza wte ktk kpnd cha ndoa S.38 of Law of marriage Act cap 39 R.E 2002
Ungeiandka kabsaa mkuu coz hzo ibara wengne hatuna
 
Beef Lasagna

Beef Lasagna

JF-Expert Member
16,572
2,000
Upo sahihi sana
Sheria ya ndoa nadhani ni mojawapo kati ya sheria zinazohitaji kuwa reviewed, ipo biased sana.
Ukiwa na mali yoyote kabla ya ndoa na ikawa imeandikishwa kwa jina lako, itahesabiwa ni yako, ukioa, kama mkeo hajawahi ijua na hajawahi kujishirikisha kwa namna yoyote ktk mali hiyo itahesabiwa ni yako mkitengana, lakini tu, akijishirikisha vyovyote vile na mali hiyo, itahesabiwa amehusika kuiendeleza na mtagawana 50/50.
Mali zote mlizopata mkiwa ktk ndoa, na zikaandikwa jina la mume, mtagawana 50/50, lakini tu, ikitokea mmezipata mkiwa ktk ndoa, na zikaandikishwa kwa jina la mke, itahesabiwa kuwa ulimpa zawadi, na ni "transfer of ownership" na kwakweli hizo hupati hata senti tano.
ANGALIZO; Kuweni makini na mali mnazowaandika wake zenu!!!
Mh hatari
 
Dah!kwa hyo mkuu ina maana kama kuna mali mke wangu kainunua ndani ya ndoa na ina jina lake tukitalikiana mimi haitanihusu na itasomeka km nilimpa zawadi tu hata kama sikumpa mimi?!
 
J

Jozi 1

JF-Expert Member
6,204
2,000
Jasho lako kabla ya ndoa ni lakwako pke ako labda kma mlishirikiana kuviendeleza wte ktk kpnd cha ndoa S.38 of Law of marriage Act cap 39 R.E 2002
Isipokuwa tu pale mali hizo zimeendelea kutumiwa na kutunzwa na wanandoa kwa jasho lao wote wawili wakati wa ndoa.
 
balibabambonahi

balibabambonahi

JF-Expert Member
8,567
2,000
Kabla ya kuoa ulikuwa na mali zako ulizomiliki kama nyumba, gari na ardhi(shamba). Ukaja kuoa baadae mkazinguana na mwanamke mkatalikiana.

Sasa katika kugawana mali; je, zile mali ulizochuma kabla ya ndoa zitahusika ktk mgawanyo?! Msaada tafadhali wanasheria wasomi
Kifungu 114 cha Sheria ya ndoa ya 1971,sura ya 29,ya Sheria za Tanzania,inataka mchango wa kila mwanandoa lazima uzingatiwe Wakati wa kugawana Mali iliyochumwa na wanandoa Wakati wa ndoa yao.Kesi ya Bi Hawa Mohamed v Alli Sefu ya 1983,ilileta kanuni ya kutambua shughuli za mama wa nyumbani ambazo siyo mchango wa mwanandoa katika kutafuta Mali.Mali ulizochuma Kabla ya ndoa kuwepo hazihesabiwi kama Mali ya wanandoa,kama mwenzio anadai zimechumwa Wakati wa uhai wa ndoa itachukuliwa kuwa ni kweli hadi pale utakapothibitishwa vinginevyo.
 
balibabambonahi

balibabambonahi

JF-Expert Member
8,567
2,000
Jasho lako kabla ya ndoa ni lakwako pke ako labda kma mlishirikiana kuviendeleza wte ktk kpnd cha ndoa S.38 of Law of marriage Act cap 39 R.E 2002
Mkuu vifungu na sura ya Sheria husika siyo vya Tanzania.
 
lushalila

lushalila

JF-Expert Member
279
250
Upo sahihi sana
Sheria ya ndoa nadhani ni mojawapo kati ya sheria zinazohitaji kuwa reviewed, ipo biased sana.
Ukiwa na mali yoyote kabla ya ndoa na ikawa imeandikishwa kwa jina lako, itahesabiwa ni yako, ukioa, kama mkeo hajawahi ijua na hajawahi kujishirikisha kwa namna yoyote ktk mali hiyo itahesabiwa ni yako mkitengana, lakini tu, akijishirikisha vyovyote vile na mali hiyo, itahesabiwa amehusika kuiendeleza na mtagawana 50/50.
Mali zote mlizopata mkiwa ktk ndoa, na zikaandikwa jina la mume, mtagawana 50/50, lakini tu, ikitokea mmezipata mkiwa ktk ndoa, na zikaandikishwa kwa jina la mke, itahesabiwa kuwa ulimpa zawadi, na ni "transfer of ownership" na kwakweli hizo hupati hata senti tano.
ANGALIZO; Kuweni makini na mali mnazowaandika wake zenu!!!
Ndani Uko kijijini mwanamke kakukuta na shamba lako la uridhi au umenunua, mmekaa mkilima na k up and a mazao mbalimbali ya kudumu na ya muda, VP nayo hiyo ni moja ya uenderezaji? Kwamba mnagawana wakati mkiachana.
 
balibabambonahi

balibabambonahi

JF-Expert Member
8,567
2,000
Dah!kwa hyo mkuu ina maana kama kuna mali mke wangu kainunua ndani ya ndoa na ina jina lake tukitalikiana mimi haitanihusu na itasomeka km nilimpa zawadi tu hata kama sikumpa mimi?!
Kugawana Mali siyo lazima nusu kwa nusu,mahakama itaamua kulingana na mchango wa kila mtu.
 
The Transporter

The Transporter

JF-Expert Member
2,653
2,000
haya mambo hatari sana bora tuanze kuchukua hatua mapema
 
Forum statistics

Threads
1,425,226

Messages
35,085,100

Members
538,249
Top Bottom