Si niliwambia msioe:- Kuna mwanamke anaenda kuangukiwa na chuma kizito kisa ndoa..!!!

Liverpool VPN

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
5,833
13,088
INTRODUCTION...
Za muda Wana JF .......

Unaukumbuka mkasa huu wa John, Michael na Mkewe....


MAIN BODY....
Basi bana kwa story za mwenyewe John, ndoa yao ilianza kuingia doa March/2021 ila mimi nilikuja kujua (alikuja kunihadithia) October/2021.

Katika hii ndoa yao, wazazi, washenga na viongozi wa dini walifanya sanaa Kazi ya kumbembeleza John asamehe ili ndoa isivunjwe.

Sasa bana, baada ya jitihada za kuinusuru hii ndoa basi John alirudi kwake March/2022 na maisha yakaendelea.

SCENARIO
John baada ya kurudi alirudi tu kimwili ila sio kiroho wala ki akili.
Kwanza kabisa humo ndani waligawana vyumba na kila mtu alikuwa na maisha yake japo wanaishi nyumba moja.

Si unakumbuka John alihama nyumbani na kuanza maisha kabla ya kurudi kwenye ndoa yake.
Basi kule kwenye maisha yake alinunua (ga) kitanda, sabufa, TV na vyombo.
Alivyorudi home alikuwa na chumba chake akaweka Kitanda chake, TV yake na Sabufa yake (vyombo aliuza).

Hivyo ndani ya nyumba John amekuwa kama mpangaji.

Akitoka kazini, anafikia chumbani kwake nakucheki TV, sebuleni hatimbi...!!!!

Mke unaambiwa alivyoona hivi na mume abadiliki alimua kuanza mchakato wa talaka mahakamani kimya kimyaaa.

Sasa bana hapa ndipo kwenye mada....

Kuna jambo John kafanya sijaelewa, wanasheria na wataalamu wengine mtanisaidia uelewa..!!!

John kabla ya kuoa alikuwa na viwanja chenye pangala ila baada ya kuoa alinunua (ga) kiwanja kengine akajenga nyumba nyengine na shamba (ndio wanapoishi na mkewe).

Sasa bana John alivyosikia mkewe anaongelea talaka alichofanya, kwa mali zotee ambazo zimepatikana kwenye ndoa kaandika jina la mama ake..!!!

Shamba lake lina hati ya mama yake
Gari lake Lina card jina la mama ake.

Hizi ndio nazozijua ila nahisi pia kuna mali nyingi tu aidha kazificha mkewe hajui au kazimilikisha kwa mama ake.

Kilichonishangaza sijajua kabadilishaje majina kutoka yake kwenda kwa mama ake au sijui alifanya kama kumuuzia mama ake (wataalamu wa Sheria mtanisaidia kwa hili...!!)

Na yote haya kafanya mwaka huu baada ya kusikia habari za kuwa mkewe ana mpango wa kwenda Mahakamani.

BIG PROBLEM...
Juzi aliitwa ofisi ya mtendaji wa kijiji.
Alipofika alikutana na summons ya kuitwa mahakamani kwa kesi ya hiyo ya talaka na mkewe....
Then IT'S OVER..!!!

Mwamba alisaini "dispach" akasepa na barua yake home na alivyofika home hajaongea na mkewe chochote..!!!

BIG MIND...
Mi binafsi nahitaji John ashinde hii kesi...!!!

Na nilichompenda alivyorudi nyumbani baada ya ndoa kusuluhishwa aliamua kumiliki document zotee za mali na kuzifanya za mama ake ...!!!!

Ni kama mtu alijua mbele kuna kitu kinakuja akamua kujiandaa.

Tukiwa kwenye kupiga bia John aliniambia(ga) kuwa nyumba anayoishi pekee ndio ina jina lake ila mali zengine zotee ni jina la mama ake.

Na Kuna mali kama shamba alinunua bila hati ila mwaka huu ndio kahaingaika na kapata hati kwa jina la mama ake.

Japo yeye anasema ana Shamba, gari na nyumba ndivyo alivyovipata kwenye ndoa ila mimi naamini ana mali nyingi tu zipo sehemu kaficha kama mashamba, maana kuna kipindi alisema ana lima miti Iringa ila aliongea kimasihala tuuu..!!!

ANYWAY ....
Nasubiri siku ya mahakama nikajifunze na hasa hii point ya mali, kwa ujanja huu alioufanya John ""Je atashinda?""

Na hizo ndio ndoa zenu.

PUNGUZENI ubishi.

Kuoa HAKUNA MAANA ""in this millennial world"" iliyojaa wasaliti.

Unatafuta kwa jashoo anatokea mtoto wa mtu ""anakupeleka mahakamani ili mgawane kisa eti umemuoa""

Okey; ""If you think money does not buy happiness, nenda kuwaulize ajira mpya walijisikiaje walivyopata mshahara mwezi huu""

NA HIZI NDIO NDOA ZENU.

#YNWA
 
Matokeo yoyote ktk maisha ya ndoa ni kama watu tunapotoka asubuhi na kurudi jioni,wote tunabahatisha utakuta huyu kafanikiwa yule kakosa,huyu karudi salama wale wamepata ajali mmoja kaenda mortuary mwengine kaishia ICU yupo pia aliyejikung’uta mavumbi akaondoka wapo waliokuwa na kazi wamefukuzwa wapo waliokuwa hawana kazi wamepata kazi in short hakuna aliye guaranteed kwamba alichoamka nacho leo atakuwa nacho kesho.

Yote hayo ni matokeo usually yanamkuta binadamu anayepumua,mimi nina ndoa nautafuta mwaka wa kumi na moja hizo changamoto sizioni labda nitaambiwa bado wakati wangu haujafika?nimeambiwa hivi zaidi ya miaka tisa nyuma huo wakati siuoni ukifika so kinachomkuta John ni kama mfano nilioutoa hapo juu
 
1698475017015.jpg

Man of The Century.
Con Queens Destroyer CQD
 
Matokeo ya chochote ktk maisha ya ndoa ni kama watu tunapotoka asubuhi na kurudi jioni,wote tunabahatisha utakuta huyu kafanikiwa yule kakosa,huyu karudi salama wale wamepata ajali mmoja kaenda mortuary mwengine kaishia ICU yupo pia aliyejikung’uta mavumbi akaondoka wapo waliokuwa na kazi wamefukuzwa wapo waliokuwa hawana kazi wamepata kazi in short hakuna aliye guaranteed kwamba alichoamka nacho leo atakuwa nacho kesho.

Yote hayo ni matokeo usually yanamkuta binadamu anayepumua,mimi nina ndoa nautafuta mwaka wa kumi na moja hizo changamoto sizioni labda nitaambiwa bado wakati wangu haujafika?nimeambiwa hivi zaidi ya miaka tisa nyuma huo wakati siuoni ukifika so kinachomkuta John ni kama mfano nilioutoa hapo juu
Umeelezea kwa mifano halisia kabisa.

Nilivokuelewa ni kuwa sio wote kwenye ndoa wanamatatizo.Shida kubwa ni vijana atupati watu sahihi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom