Sheria ya Ndoa inasemaje kuhusu mali zilizochumwa kabla ya ndoa?

Sikumbuki ni redio gani na kipindi kinaitwaje ila nlimsikiliza mwanasheria akiwa analijibu hili, alisema kuwa wakati mnaoana unaweza kuziainisha zile mali ulizochuma mwenyewe kabla ya ndoa na mke pia kama ana zake ataziainisha na ikitokea mkaachana basi hizo mali hazitahusika kwenye mgawo ila kama hukufanya hivyo wakati mnaoana basi mali zote zitahusika
 
Mungu wangu kumbe ni hivyo tena?!?hii sheria mbona INA upendeleo mbovu kabisa kwa wanawake!!!!. Wabeja sana wang'wise.
Upo sahihi sana
Sheria ya ndoa nadhani ni mojawapo kati ya sheria zinazohitaji kuwa reviewed, ipo biased sana.
Ukiwa na mali yoyote kabla ya ndoa na ikawa imeandikishwa kwa jina lako, itahesabiwa ni yako, ukioa, kama mkeo hajawahi ijua na hajawahi kujishirikisha kwa namna yoyote ktk mali hiyo itahesabiwa ni yako mkitengana, lakini tu, akijishirikisha vyovyote vile na mali hiyo, itahesabiwa amehusika kuiendeleza na mtagawana 50/50.
Mali zote mlizopata mkiwa ktk ndoa, na zikaandikwa jina la mume, mtagawana 50/50, lakini tu, ikitokea mmezipata mkiwa ktk ndoa, na zikaandikishwa kwa jina la mke, itahesabiwa kuwa ulimpa zawadi, na ni "transfer of ownership" na kwakweli hizo hupati hata senti tano.
ANGALIZO; Kuweni makini na mali mnazowaandika wake zenu!!!
 
Kabla ya kuoa ulikuwa na mali zako ulizomiliki kama nyumba, gari na ardhi(shamba). Ukaja kuoa baadae mkazinguana na mwanamke mkatalikiana.

Sasa katika kugawana mali; je, zile mali ulizochuma kabla ya ndoa zitahusika ktk mgawanyo?! Msaada tafadhali wanasheria wasomi
rejea kesi ya Bi hawa mohamed na mumewake
 
rejea kesi ya Bi hawa mohamed na mumewake
nimejenga nyumba kwenye kiwanja cha mke wangu alichonunua tukiwa kwenye ndoa,je nyumba ni yake au yetu?..akichukulia mkopo bila kunishirikisha na akashindwa kurejesha,wakopeshaji wana haki ya kuiuza?
 
NAHITAJI MTAALAM ATAKAYEWEZA KUNIONGOZA NAMNA YA KUACHANA NA MKE KWA USALAMA NIPO SONGEA PIA ANAWEZA KUNICHEKI KUPITIA 0764093436
 
Back
Top Bottom