Sheria mkononi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria mkononi!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MkamaP, Feb 21, 2009.

 1. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Na Mpoki Bukuku

  MKAZI wa Manzese Uzuri, jijini Dar es Salaam, amenusurika kufa baada ya kupigiliwa na misumari kwenye msalaba na wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira, kwa tuhuma za kuiba baiskeli.

  Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana maeneo ya Manzese Uzuri baada ya kijana huyo kukutwa na baiskeli iliyodaiwa kuwa ya wizi.

  Wakazi wa eneo hilo walimkamata na kisha kutengeneza msalaba na kumtundika juu kwa kumpigilia misumari ya nchi sita kisha kumwacha hapo.

  Baadaye wasamaria wema waliopita katika eneo hilo walimwona wakautoa ubao mmoja na kisha kijana huyo akaenda kujisalimisha katika kituo cha polisi akiwa na ubao wa mikononi ambako alipigiliwa mishumari.

  Polisi wa kituo hicho wakamkimbiza katika Hospitali ya Mwananyamala akiwa kwenye msalaba huo kwa ajili matibabu.

  "Sijawahi kuiona katika maisha yangu, wananchi kweli wamekuwa wanyama," alisema mfanyakazi mmoja wa hospitali hiyo mara baada ya kumpokea mtu huyo aliyeletwa na polisi hospitalini hapo mapema asubuhi jana.

  Akisimulia mkasa huo baada ya kumhudumia kwa kumtoa misumari iliyokuwa imepigiliwa mikononi na mabegani; mtumishi wa hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alisema: 'Baadhi misumari iliingia katika mifupa ya mikono na kumuumiza vibaya."

  "Ameumia sana na kuna mifupa ambayo imevunjika baada ya kutobolewa na misumari hiyo mikubwa, lakini ana bahati hajafa," alisema mtumishi huyo.

  Imeelezwa kuwa kijana huyo mara baada ya kukutwa na baiskeli hiyo, wananchi walimkamata na kumsulubu kwa kutengeneza msalaba na baadaye kumpigilia kwenye msalaba na kumwacha akiwa ananing’inia.

  Baadaye walipita wasamaria wema walioamua kumsaidia kwa kuondoa ubao mkubwa uliokatisha mgongoni na hivyo yeye kujisalimisha polisi huku ubao uliopigiliwa mikono ukiwa bado mwilini mwake.

  Polisi walimchukua na kumpeleka hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu na hakufunguliwa mashtaka yoyote kwani hakukuwa na mtu aliyelalamika kuibiwa.

  Baada ya kufikishwa hospitalini hapo kijana huyo alikuwa kivutio kwa wagonjwa na ndugu waliowatembelea pamoja na baadhi ya watumishi waliokuwa hapo.

  Wengine kwa kushangazwa ama kuvutiwa na kitendo hicho waliamua kupiga picha kwa kutumia simu zao ambazo zilimwonyesha kijana huyo akiwa katika maumivu makali.
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hii ndo dawa ya kukomesha vibaka.
  Kama serikali imeshindwa kumlinda raia hii ndo njia pekee ya kutokemeza ualifu sehemu mbalimbali nchini watu wamechoka na hivi vitendo.Bado kidogo wananchi wenye hasira kali wataanza kuwaadhibu hata viongozi wao.
   
 3. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Walitaka kumsulubisha nini!
  Huyo kijana hatarudia tena kwa hilo fundisho alilopata. Kumbe siku hizi hawachomi tena vibaka/wezi moto? Staili mpya hiyo ya kupigilia viganja vya mkono kwa misumari ubaoni ni kali sana. Ila dawa ya uhalifu ni kuadhibiwa hapo hapo!
   
 4. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Eh! kweli kali, wameachana na kuchoma moto sasa wanawatundika msalabani!! Haya walitakiwa wafanyiwe mafisadi, si mwizi wa baskeli.
   
 5. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ungebandika kapicha kake hapa kangevutia Mkuu....
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Desperation ya wananchi, uhuni, kushindwa kufanya kazi kwa law management system au nini?
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  Feb 21, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  hakuna serikali tanzania, kila m2 na lwake!
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Feb 21, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hapa jamaa akitolewa misumari
  1 akitolewa misumari.jpg


  Jamaa akiwa hoi baada ya kutolewa misumari
  23 akiwa hoi.jpg
   
 9. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #9
  Feb 21, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Du kweli haya maisha duu.

  Naomba kuuliza swali Hivi sisi tupo hapa duniani ili iweje?
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Feb 21, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Miafrika Ndivyo Tulivyo....anayebisha athubutu kupinga...
   
 11. I

  Isskia Member

  #11
  Feb 21, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nadhani hiyo ndio dawa sahihi, kumtia tu maumivu ili akipata ahueni arudi mtaani akawahadithie wenziwe, that is good.
   
 12. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #12
  Feb 21, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Nchi ambazo zinatumia Sharia, kosa la kwanza la wizi unakatwa kiganja cha mkono wa kushoto. Kosa la pili, kiganja cha kulia. Kosa la tatu, kanyagio la mguu wa kushoto. La nne, kanyagio la kulia. Bado utaendelea kuiba? Ninavyoupenda mwili wangu, ya nini yote hayo?
   
 13. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #13
  Feb 21, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Serikali ipo ndiyo hiyo ilitoa hukumu ya msalaba
  This is Pinda style, Tanzania ndiyo maendeleo haya, ukikamata mtuhumiwa hukumu ni onspot,mahakama zinachelewesha sana au kuwaachia. vibaka hawakomi na serikali imechoshwa nao bora hivi hivi tu
   
 14. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #14
  Feb 21, 2009
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haikubaliki kamwe kumsulubu mwenzako hivi. Tuwe wastaarabu
   
 15. JohnShaaban

  JohnShaaban JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2009
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 465
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Pinda alishatoa ruhusa baada ya kuona Polisi na Wizara ya Mambo ya ndani wamepoteza sifa ya kulinda raia wa URT. Wizara iko likizo kufuatia mchakato wa vitambulisho vya Taifa kuingiliwa!!
   
 16. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huyo kaiba baiskeli tu anapata kipigo kama hicho. Mbona wezi wetu wa EPA wanapeta mitaani?
   
 17. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #17
  Feb 22, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Haya bwana!!! athari za watu kukimbia shule, sasa hata kuwafundisha kuhusu haki za binadamu utaanzia wapi?

  Kuna kizazi mpaka kiondoke ndio Tanzania itabadilika.
   
 18. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Ni dalili dhahiri za Watanzania kukata tamaaa....
   
 19. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2009
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wananchi wamechoka maana wanaona kila kitu ni usanii, la msingi wao wafanye wawezavyo. Kimsingi si sawa kuruhusu haya kutokea lakini hatuwezi kuyatibu kwa kuwanyima kufanya hivyo tuu, tunapaswa kujua vyanzo vya mambo haya na kuvishughulikia kwanza. Hapo tukiwasisitizia wananchi kuacha wataacha. Jeshi letu limeduwaa sana kwenye kuthibiti uhalifu, hata hivyo nao wao kwenye wakati mgumu maana maisha yao magumu, kipato chao kidogo na masikini kuliko wahalifu (obvious rushwa itachukua nafasi). Serikali yenyewe bado intakiwa kulaumiwa kwa yote, muundo mzima ni mbovu na kuna mambo mengi sana ya kurekebisha walau taratibu, kibaya ni kwamba juhudi kubwa za serikali ni kupambana na wananchi ili huu muundo mbovu uendelee kutumika.

  Zamani ilikuwa ajabu sana kusikia kiongozi anasemwa semwa, wakaanza kusemwa lakini ilikuwa ajabu sana kuandikwa gazetini hata kwa tetesi za ubadhirifu. Lakini hayo yote yameendelea na sio ajabu sasa kutukana viongozi live kwenye internet, kuwatukana live kwenye magazeti, kusema habari zao za ubadhirifu live kwenye tv, kuwazomea viongozi wakubwa kama rais na mawaziri, kurushia misafara mawe n.k.., nina mashaka siku sio nyingi haitakuwa ajabu kuvunja-vunja na kuchoma moto magari ya viongozi wa serikali kisha baadaye kidogo itakuwa sio ajabu pia kuwakamata na hata kuwachoma moto viongozi wa serikali tulioona wazi ni wezi kama akina Chenge, Karamagi na wegineo kabla hatujaja kwa prezidaa ambaye atakuwa akilaza damu kuwashughulikia wezi wa nchi hii.

  Maandamano na mashinikizo mengi ya kuwang'oa watawala yanayotokea katika nchi nyingi duniani hayakuanza siku moja, yalianza kwa wananchi kuminywa sana, kisha kupata habari na kujanjaruka kwamba wanaminywa. Kisha huendelea kwa wao kuanza kudai haki zao taratibu na wasipposikilizwa hufikia kutumia nguvu ikiwa ndio njia iliyobaki kwao kupata haki zao.

  Watawala wanajifariji kwamba wanayofanya kwa sasa yatatupooza, mfano Kikwete anapopiga kelele na mambo ya mbolea anashawishika kwamba watu watapoa. Kimsingi itamsaidia kupunguza kasi ya ukuaji wa hasira za wananchi, lakini sio kusafisha kutu zilowaingia watanzania kwa kugundua wanatapeliwa. Kikubwa hapa mfumo mzima ushughulikiwe tena "in-time" la sivyo ngoma iko pale maana tunaona wazi na tunazo data za kutosha kwamba wote huu ni usanii.

  Watawala pia wanajitia moyo kwamba asilimia kubwa ya wananchi hawajui nini kinaendelea kwahiyo bado wanayo nguvu na muda wa kukaa, niwape tu wana-usalama tahadhari kwamba hii kampuni ya SEACOM inayoleta mkonga wa internet hapa kwetu italeta mabadiliko makubwa kwenye nchi hii ikiwemo wananchi wengi zaidi kupata taarifa haraka haraka zaidi na kwa urahisi zaidi. Sijafanya utafiti lakini naamini taarifa zitaenea over 10 times faster in few time to come. Tukumbuke kwamba kwa kipindi cha karibuni internet imechangia sana kulipua mabomu mengi yahusuyo ubadhirifu katika nchi hii, ina maana matumizi ya internet yakiongezeka pamoja na mambo mengine harakati za kupambana na mafisadi zitaongezeka maradufu. Kibaya ni kwamba wae wenye nguvu ndogo watakuwa wamepata msaada na kwa vyovyote nguvu ya umma kui-resist serikali itaongezeka kuliko uwezo wa serikali kuithibiti kwa njia ya demokrasia. Serikali itachagua vita ama ipoe ifanye itakachoelekezwa.

  Naomba niishie hapa kwa leo maana naona simalizi wakuu, ni mengi sana na naomba tujifunze kutathmini mbeleni kutokana na historia zetu.
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Feb 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Akili ya Kitumwa

  Matokeo ya dhamira ya wananchi kuchukua sheria mkononi haitokani na usemi wa Pinda..hali hii ilikuwepo toka enzi za Mkapa baada ya hali halisi ya adui wetu wakubwa UJINGA na UMASKINI kuanza kufanya kazi yake..ktk mazingira ya Ubepari (kila mtu na chake)..

  Ubepari kwa aina fulani hautofautiani kihistoria na Ukoloni au Utumwa ktk tawala na mifumo yake ya biashara..Katika mifumo yote Mtumwa siku zote hawezi kumhukumu Tajiri wake!.. tuliona wakati wa Utumwa wafungwa wakiuana wao kwa kipande cha mkate, wakiuana wao kama mchezo wa kumfurahisha tajiri..
  Ukoloni vile vile, tuliokuwa tukijimaliza ni sisi wenyewe. Majeshi ya mkoloni yalijengwa na sisi weusi wenyewe, hata huko South Afrika askari wake wengi walikuwa weusi na walifanyiza kichizi ndugu zao wakiwa na silaha ambayo ungejiuliza kwa nini wasimgeuke kaburu mtawala aliyewakandamiza...
  Yote haya yanatokana na umaskini na Ujinga, ni hali halisi inayotushinda leo hii kunyoosha kidole kwa watawala wetu badala yake hasira zetu za unyonge zinakomea kuumizana sisi wenyewe wakati watawala wakila kuku na kutunga siasa...
  Hata mauaji ya Albino, wenmye vipara, bibi vizee na hawa vibaka ambao sasa hivi kumezuka kundi linalojiita Kiboko Msheri ambao wanavizia watu ktk magari yao wafikapo ktk stop sign.. ukisimama tu umekwisha!..enzi za mwalimu kiboko msheri walikuwa washabiki tu wa timu ya mpira, leo hii limekuwa kundi la majambazi wanaovizia watu kwa mapanga na visu...
  Nina hakika ukimuuliza Waziri wa mambo ya ndani Masha kuhusiana na usalama wa Tanzania atasema nchi ni shwari kabisa, haya ni matukio madogo madogo tu..
  Hivyo Miafrika ndivyo tulivyo inaanza mbali toka serikali kupuuza, wezi wenyewe (criminals) na wananchi kupinga au kukubali hali inayoendelea bila kutafuta solution ni matendo ktk mfulululizo wa Ndivyo Tulivyo!
   
Loading...