Sheria mbaya zimechangia ukosekanaji wa Dola Tanzania

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Sheria mbaya za wakati wa Magufuli zimechangia sana ukosefu wa dollar

1. Vitendo vya kuingiza jeshi na Polisi kwenye biashara ni kitendo kibaya. Kitendo cha kuvamia maduka ya pesa za kigeni karibu yote na kuchukuwa pesa bila amri ya mahakama, bila kuwa na kesi za wizi kulitoa mwanya kwa wezi ndani ya serikali. Hii pia imeleta kutokuiamini serikali hasa kwa wafanya biashara

2. Kietendo cha kuongeza milolongo ya vibali wakati wa kubadilisha pesa kumefanya diaspora wakija Tanzania waone ni bora kujitumia pesa kwenye Mpesa zao kuliko kubeba dollar wakija kufanya shughuli zao. Hii mitandao wanayoitumia kutuma pesa haipeleki dollar Tanzania!. Sikuhizi kubadilisha pesa unatakiwa uwe na copy ya passport na kukaa muda mrefu kwenye maduka au bank chache zilizoko wazi. Usumbufu huu umesababisha diaspora kuona ni bora watumie Apps kutuma pesa kwa shughuli mbalimbali.

3. Wenye kampuni za utalii wanauza package huko nje na pesa haziji Tanzania. Hii ni kutokana na uoga wa serikali bila kibali cha mahakama kuwafuatilia pesa zao bank na kuwafanyia uchunguzi bila sababu . Ilifika wakati mpaka ku freeze pesa zao wakati huduma walizolipwa hawajatoa. Bank wamekuwa kama wambeya wa serikali ! Hii imesababisha kampuni nyingi kuacha pesa nje

- Mapendekezo kutatua tatizo la Dollar Tanzania
 
Back
Top Bottom