Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Siku chache zilizopita kumekuwa na habari ambayo imejaribu kuonesha umahiri mkubwa wa JWTZ kukabiliana na maharamia. Kwamba watu kama nane wanaosadikiwa kuwa ni maharamia walikamatwa walipojaribu kuiteka meli moja kwenye bahari ya Hindi. Watu hao walikamatwa na baadaye kupelekwa kikosi cha jeshi na sasa imeripotiwa kuwa wanapelekwa Polisi.
Najiuliza kama kuna sheria yoyote ya kusimamia Uharamia (Anti-Piracy in the High Seas) Tanzania. Isije kuwa tunajaribu kuita kosa kitu ambacho si kosa kisheria! Kama kuna sheria inayosimamia haya ni ipi nimejitahidi kutafuta lakini sijaona bado.