Mauaji ya Polisi wetu ni Ujambazi, Ugaidi au Retaliation? Nini kifanyike kukomesha hali hii?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,620
Wanabodi,

Taifa bado liko kwenye shock ya nini haswa kilichotokea kwa askari wetu?

Mauaji haya ya Polisi Wetu ni Ujambazi tuu, ni Ugaidi au Retaliation?. Wakati vyombo vya uchunguzi vikiendelea na kazi yake, Sisi Watanzania kama taifa lazima tujiulize, Nini Kifanyike Kukomesha Hali Hii?

Kwanza nikiri nimesikitishwa na vifo hivi vya vijana wetu askari polisi kushambuliwa na kuuwawa na majambazi wenye silaha.

Swali ni jee huu ni ujambazi tuu wa kawaida, uvamizi kwa lengo la kuiba silaha, ni ugaidi, ambush au nini haswa?

Hili kuwaweka polisi wetu kwenye risk na kuwa an easy target, kwa majambazi wanaotumia silaha, niliwahi kulizungumza hapa kwa kirefu Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje

Kwa tukio kama la jana,jee mnadhani huu sasa ni wakati muafaka wa kuzibadili sheria zetu za jeshi la polisi ili kuwalinda polisi wetu wawe licenced to kill officially na serikali itangaze rasmi kuwa ujambazi wa kutumia silaha adhabu yake ni kifo cha papo kwa papo, no prosecution no kesi, bali ni hukumu ya kifo there and then ili kuwaogofya kabisa majambazi wote wanaotumia silaha wasithubutu?!.

Kama ni ugaidi au retaliation, tufanye nini?

Natoa pole kwa rais wetu wa JMT, waziri wa Mambo ya Ndani, IGP na familia za askari hao!

RIP Askari Wetu
Nini Kifanyike?
Ijumaa Kuu Chungu!
Paskali
Update 1
Nionavyo mimi ni makundi ya maharifu yanakusanya silaha.

Halfu kitu kingine kule yanakotokea haya ni kule kule kwenye pwani isiyokuwa na ulinzii. Ulinzi uimarishwe katika njia chocho za bahari.

Ninaomba JWTZ wafanye operation maalumu katika misitu iliyokatika maeneo hayo. Kunaweza kuwa na kambi maalumu ya uahrifu.

Tatu viongozi wa dini ya kiisilam, wale wanaowaza mema, wakae na wajadili namna ya kukomesha mitazazmo mibovu ya baadhi ya watu walio nao juu ya maisha. Bila shaka wanafahamu haya ni kwa nini yanatokea kwa kuwa eneo yanakotokea haya ni kule kwenye wingi wa wafuasi wao ambao wameshindwa maisha. Wanatakiwa wawape elimu sahihi namna wataboresha maisha yao badala ya kutafuta njia za kiharamia au kutaka kuharibu nchi ili wakose wote. Hii ni roho ya shetani yule mwenye wivu.

Nne jeshi la polisi lirudi katika misingi ya kutenda haki. Waacha uharamia wa kudhulumu na kuonea raia. Polisi waache unyanganyi wa mali na haki za raia ili jamii iwaone kuwa ni sehemu yake na iwape ushirikiano. Polisi wamejitenga na wananchi ki malengo na ndiyo sababu wananchi wako kimya hata wanapoona mipango miovu inatokea. Ninasema hivi kwa sababu, bila shaka hata katika tukio hili kulikuwa na watu karibu. Hao jambazi hakutoka hewani na hakuyeyeyuka baada ya ushetani wake. Watu walimwona akiingia na alikoelelkea wanajua. Jeshi la polisi linahitaji kuhamasisha umoja kati yake na raia ili raia walisaidie kuzuia matukio ya kishetani kama haya.

Tano serikali iache kuwatumia polisi vibaya. Inawajengea chuki dhidi ya wananchi. Wanachi wanaoan polisi ni watesi wao na si wasaidizi n ahivyo kujitenga nao mbali. Viongozi wa ccm na serikali wawekeane mikakati ya kudhibiti matumizi ya jeshi la polisi yasiyo halali. Yanalidhalilisha jeshi letu na kuliweka katika wakati mgumu sana wa kutengwa na umma.

Serikali itambue kwamba hii ni karne nyingine. Budget za serikali ziangalie suala la technolojia ya ulinzi na usalama ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu. Ikiwa tetemeko lilitokea Bukoba na hapakuwa na hata kipimo cha kutambua kabla hatua stahiki zikachukuliwa, na bado serikali ikasema haikuleta tetemeko, niina mashaka na uwepo wa technolojia ya ulizini wa mipaka yetu hasa katika bahari na sehemu zisizokaliwa na watu. Kuliko kutumia nguvu kubwa kudhibiti wapinzani, ninaomba serikali iwekeze kweney technolojia surveillance ndani na nje ya mipaka yetu. Polisi wanaoonyesha uharamia kama kunyang'anya mali za mahabusu kwa nguvu, kutetea uharlfu ndani ya jeshi, kuonea na kusingizia raia, wanatakiwa kuondolewa kwenye kikosi hivi kwa sababu hawa ini hatari kwa jeshi lenyewe. Wanaweza kuuza taarifa hata mipango ya dani ya jeshi kwa maslahi ya 1000,000. Ondoeni maharamia kati ya polisi, sukeni jeshi letu upya, kisha liwezeshwe kwa technolojia inayoona na kutoa taarifa ya matukio hasa katika maeneo yenye wasialam wengi kama huko pwani na mkuranga.

Watanzania ninaomba sana tuendelee kuishauri serikali japo inakataa kushauriwa. Hii la kukataa ushauri wa wanaoongozwa tulichukue kama tatizo linalohitaji tiba kama maradhi lakini hatwezi kujenga taifa pasipo kushauriana na kusikilizana. Ccm ninyi ndio wenye viburi, ninaomba muwe wa kwanza kujirekebisha. Tambueni bila taifa lenye amani ccm haipo.

Viongozi acheni kujenga matabaka miongoni mwa wananchi. Acheni kuwadharau watanzania na kuwabagua, huku mkifanya kebehi za wazi kwa viburi. Migawanyikio mnayoijenga ndiyo inayoondoka mishkikamano na mioyo ya uzalendo . Bila kuwa na umoja na uzalendo, hakuna suluhu rahisi ya matatkzo yanayoinuka.

NINAOMBA NISIITWE MCHOCHEZI MAANA SERIKALI INADHANI IKIWAUNGA WATU VINYWA NDIYO INASHINDA, KUMBE INAJENGA ROHO MBAYA ZA KIKATILI NA MTAWANYIKO UANOANZA KULIGHARIMU TAIFA KWA KASI HII YA AJBU.
Thanks very objective.

Paskali
Update 2 ya michango very objective
Pasco licence to kill inaweza kutumika kwenye nchi zenye Polisi watenda haki, hivi hiyo licence to kill wangepewa leo Nape angekuwa hai?

Kutazuka mauwaji ya kubambikiana ujambazi fake kisa kugombea demu.

Kwa upeo wangu mdogo jeshi la polisi linaujuwa vizuri mtandao wa ujambazi.

Inasikitisha sana jeshi letu kutumia resource nyingi pesa za umma kukimbizana na kina Tundu Lisu wanaotimiza wajibu wao wa kikatiba na kuwaacha hasa maadui halisi wa usalama wao na wa raia.

Jeshi la Polisi lijitenge na siasa na litapata sapoti ya umma.

Hakuna nchi yenye majambazi waliopinda hapa Africa zaidi ya South Africa lakini kamwe hawawezi hata kufikiria hata siku moja kuwavamia polisi au kupambana nao.

IGP atoke huko mafichoni aongee na IGP mwenzake wa South Africa tuwapeleke vijana wetu training kule, na wale vijana wenye maumbo six park na ya kimazoezi sasa waondolewe FFU na waletwe kwenye vikosi vya anti robbery.

Huwa sielewi eti wale vijana wenye maumbo shupavu ati wanapelekwa FFU kula kulala kusubiri kuwapiga mitana na virungu raia wema wanaondamana kudai haki zao.

Mwigulu Nchemba soma ushauri huu, nenda pale FFU piga king'ora cha parade uone mijibaba ilijoza kimazoezi itakayofika pale halafu fananisha na kikosi chako cha Anti robbery utagunduwa wazi sisi tuna matatizo kichwani.

Mimi si mtaalam wa mambo ya ulinzi lakini ni muda muhafaka sasa wa kuwa na kikosi maalum na siyo kikosi kazi, kikosi hiki kiundwe na FFU pamoja na JWTZ na kiitwe Cobra, hakuna jambazi tena atakayetamani kukutana na Cobra.
Thanks kwa mchango huu, very objective
Paskali
Update 3.
Huu ni mchango very objective
Mkuu Paskali, tukio hili kwa kweli linaumiza sana. Na linaumiza na kuleta hofu kubwa; kwamba kama askari wetu ambao ndio tunawaamini kuwa wanaweza kutulinda wanapukutishwa kirahisirahisi kiasi hicho, usalama wetu sisi raia uko katika mazingira gani? Ni tukio baya lakini linalotaka tafakuri huru isiyoathiriwa na ubaya wa tukio lenyewe. Kwanza, kuruhusu polisi wawe licenced to kill officially itakuwa ni wazo lililoathiriwa na ubaya wa tukio lakini lisilotatua tatizo la msingi. Kuruhusu polisi kuua hapo hapo ni kuongeza tatizo badala ya kulitatua. Vifo hata vya wasio na hatia vitaongezeka. Na haiwezi kushangaza "majambazi hewa" wakawa wengi kuliko majambazi halisi!

Ni mtazamo wangu kwamba tatizo hili tunaliona sasa-la askari kuuawa kwa namna inavyotokea huko mkoani Pwani, uhusiano baina ya polisi na raia unahusika positively or negatively. Ni bahati mbaya kwamba wakati kuna viongozi wa kisiasa wanaoamini katika kuwepo kwa uhusiano mzuri baina ya askari polisi na raia, bado viongozi wengine kauli na matendo yao ni tangazo kwamba hawataki kabisa polisi wawe na uhusiano mzuri na raia. Hii inakata mtiririko wa polisi kupata taarifa za criminals.

Pili, polisi wasio waadilifu wamekuwa wakishirikiana na raia wasio waadilifu kufanya matukio ya kijinai-wao huwa wanaita "ni kutafuta pesa". Kuna wakati hawa watu hugeukana, na wanapogeukana haya ndio hutokea. Sisemi kwenye tukio hili kuna mazingira haya, bali najaribu kuonyesha mazingira yanayosababisha wakati mwingine kuwepo kwa matukio kama haya.

Tatu, polisi wengi wanachoweka mbele kwenye akili yao ni pesa, yapo matukio ya kuuawa kwao yanayosababishwa na wao kudhani kwamba kila mtu kwao anaweza kuwa "deal". Tukio la askari polisi kuuawa katika kituo cha polisi Stakishari linaingia kweye mfano huu. Baada ya tukio la Stakishari polisi walionekana kushtuka lakini ile hali ya kudhani kila mtu kwao ni "deal" imewarudia tena, unaweza kuona kupitia matukio mbalimbali ya ukamataji "yasiyo rasmi".

Sitaki kuharakisha kuhusisha matukio hayo na ugaidi. Lakini ushauri wangu kwa polisi au serikali yenyewe kwa ujumla, kiwepo kitengo maalum cha kuchunguza mienendo ya askari kuanzia wa vyeo vya juu hadi chini. Kuna mitandao ndani ya polisi ambayo kazi yake ni kupora mali za criminals na mwisho wa siku huibua hasira kwa criminals hao, kushirikiana na criminals kufanya matukio ya kijinai na mwisho wa siku hudhulumiana na baadaye kuwepo matukio ya kulipiza visasi; nakadhalika. Na mwisho, angalau kwa sasa, nashauri viongozi wetu wahubiri uhusiano wa polisi na raia badala ya kuhubiri chuki baina yao!
RIP askari wetu..
Thanks for this.
Paskali
 
Kiukweli nimeumia sana baada ya kupata taarifa hii ya mauaji ya kutisha.Mimi nipo Lindi kwa habari zilizozagaa miongoni mwa polisi aliyeuawa ni ndugu yetu si watumbo moja bali anatokea hapa Lindi. Nimeumia,tumesikitika kwani polisi ni ndugu zetu,watoto wetu ifike wakati serikali ikomeshe haya mauaji imetosha.Ikibidi hata wapelelezi huru kutoka mataifa makubwa waje watupelelezee maana tunaumia jamani ndugu zetu hawaaa.
 
Kisifanyike chochote juzi kuna Wabunge wameomba hilo swala lijadiliwe bungeni kuna wanawake jenista mhagama na mwenzie bila hata aibu wanasema ni uchochezi!
Yakasikika makofi ya Wabunge wa ccm waaaa...waaaa....waaaa....
Acha tuendelee hivi hivi
 
Matukio yanayotokea huko Pwani ni asilimia 100 ugaidi. Kitu cha kushangazaa ni hawa magaidi kuua na kuchukua silaha je wanamipango gani na hiyo silaha. Serikali isichukulie suala hili mzaha ama ujambazi wa kawaida kwani tunatakiwa tujifunze kutoka Nigeria jinsi Boko Haram ilivyoanzishwa. Mkoa wa pwani unapakana na bahari ya hindi na mnavyoelewa kuna tatizo la magaidi Kenya na Somalia je serikali inatathimini vipi watanzania wangapi wamejaribu ama wamejiunga na vikundi hivyo vya kigaidi na kurudi hapa nchini. Leo hii tunaona nchi za ulaya kuna vijana waliokuwa wamejiunga na Islamic State huko Syria wamerudi ulaya na kuanza kufanya ugaidi. Tuangalie suala la uchumi pia sasa hivi sisi na majirani zetu tuko kwenye vita vya kiuchumi katika ujenzi wa bomba la mafuta, reli na utalii majirani zetu wameonekana sio salama na Tanzania imeonekana ni nchi salama kunauwezekano wa hawa majirani zetu wakatumia watu wabaya ili Tanzania isionekane nchi salama,
Serikali ilichukulie hili suala very very serious kabla halijawa out of control.
 
Kweli vifo vya askari wetu ni jambo linalomsikitisha kila raia mpenda amani, lakini kikubwa ninachokiona hapa na hasa hii awamu ya tano ni kiongozi mkuu kutopenda ushirikiano ulikuwa unasaidia kupatikana taarifa kati ya police na raia. Tumeona rais aliyotumia nguvu nyingi kuzuia police jamii wakati hilo liliwekwa kwa ajili ya kupunguza uhalifu kama huo
 
Dereva wetu mzuri yuko anaendesha Roli hivyo ata tukisema hawezi sikia. Yeye anafanya anavyoona inafaa ilimradi atufikishe 2020, tukiwa vilema, viwete, viziwi au marehemu hiyo ni bahati mbaya kwake maana anajinasibu kuwa yeye dereva mzuri ambaye hajawahi tokea kwenye huu ulimwengu.
 
In my point of view this is neither cospiracy nor robbery but it seems to be the FEELING of dehumainsation and oppression thats being conducted by the governing THEATRE...thus, this has the scence of RETALIATION ON THE MOTION and easist target is armed servicemen(women) that exactly giving us "tanzanian" hard time thinking of our "SAFETY" while armed men are dying accassionaly what about we the normads of life? Can we be spared our safety?
 
Mkiona jambazi ana bunduki umuwahi uchukue bunduki hiyo kauli inawaponza sana sasa jambazi gani atakubali mtaji wake uondoke kirahisi rahisi

Kuna ile alisema majambazi walazwe chini badala ya kusema wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo husika.

Sasa naona majambazi wameamua ku-retaliate..ndo wanawalaza askari chini sasa. Inabidi kwa kweli kiongozi wa nchi apime kauli zake maana........
 
Wanabodi,
Taifa bado liko kwenye shock ya nini haswa kilichotokea kwa askari wetu?.

Mauaji haya ya Polisi Wetu ni Ujambazi tuu, ni Ugaidi au Retaliation?. Wakati vyombo vya uchunguzi vikiendelea na kazi yake, Sisi Watanzania kama taifa lazima tujiulize, Nini Kifanyike Kukomesha Hali Hii?,

Kwanza nikiri nimesikitishwa na vifo hivi vya vijana wetu askari polisi kushambuliwa na kuuwawa na majambazi wenye silaha.

Swali ni jee huu ni ujambazi tuu wa kawaida, uvamizi kwa lengo la kuiba silaha, ni ugaidi, ambush au nini haswa?.

Hili kuwaweka polisi wetu kwenye risk na kuwa an easy target, kwa majambazi wanaotumia silaha, niliwahi kulizungumza hapa kwa kirefuhttps://www.jamiiforums.com/threads/hili-la-polisi-kuruhusiwa-kuwanyanganya-silaha-majambazi-na-kupandishwa-vyeo-limekaaje.1071133/page-5

Kwa tukio kama la jana,jee mnadhani huu sasa ni wakati muafaka wa kuzibadili sheria zetu za jeshi la polisi ili kuwalinda polisi wetu wawe licenced to kill officially na serikali itangaze rasmi kuwa ujambazi wa kutumia silaha adhabu yake ni kifo cha papo kwa papo, no prosecution no kesi, bali ni hukumu ya kifo there and then ili kuwaogofya kabisa majambazi wote wanaotumia silaha wasithubutu?!.

Kama ni ugaidi au retaliation, tufanye nini?.

Natoa pole kwa rais wetu wa JMT, waziri wa Mambo ya Ndani, IGP na familia za askari hao!

RIP Askari Wetu.
Nini Kifanyike? .
Ijumaa Kuu Chungu!.
Paskali

Nionavyo mimi ni makundi ya maharifu yanakusanya silaha.

Halfu kitu kingine kule yanakotokea haya ni kule kule kwenye pwani isiyokuwa na ulinzii. Ulinzi uimarishwe katika njia chocho za bahari.

Ninaomba JWTZ wafanye operation maalumu katika misitu iliyokatika maeneo hayo. Kunaweza kuwa na kambi maalumu ya uahrifu.

Tatu viongozi wa dini ya kiisilam, wale wanaowaza mema, wakae na wajadili namna ya kukomesha mitazazmo mibovu ya baadhi ya watu walio nao juu ya maisha. Bila shaka wanafahamu haya ni kwa nini yanatokea kwa kuwa eneo yanakotokea haya ni kule kwenye wingi wa wafuasi wao ambao wameshindwa maisha. Wanatakiwa wawape elimu sahihi namna wataboresha maisha yao badala ya kutafuta njia za kiharamia au kutaka kuharibu nchi ili wakose wote. Hii ni roho ya shetani yule mwenye wivu.

Nne jeshi la polisi lirudi katika misingi ya kutenda haki. Waacha uharamia wa kudhulumu na kuonea raia. Polisi waache unyanganyi wa mali na haki za raia ili jamii iwaone kuwa ni sehemu yake na iwape ushirikiano. Polisi wamejitenga na wananchi ki malengo na ndiyo sababu wananchi wako kimya hata wanapoona mipango miovu inatokea. Ninasema hivi kwa sababu, bila shaka hata katika tukio hili kulikuwa na watu karibu. Hao jambazi hakutoka hewani na hakuyeyeyuka baada ya ushetani wake. Watu walimwona akiingia na alikoelelkea wanajua. Jeshi la polisi linahitaji kuhamasisha umoja kati yake na raia ili raia walisaidie kuzuia matukio ya kishetani kama haya.

Tano serikali iache kuwatumia polisi vibaya. Inawajengea chuki dhidi ya wananchi. Wanachi wanaoan polisi ni watesi wao na si wasaidizi n ahivyo kujitenga nao mbali. Viongozi wa ccm na serikali wawekeane mikakati ya kudhibiti matumizi ya jeshi la polisi yasiyo halali. Yanalidhalilisha jeshi letu na kuliweka katika wakati mgumu sana wa kutengwa na umma.

Serikali itambue kwamba hii ni karne nyingine. Budget za serikali ziangalie suala la technolojia ya ulinzi na usalama ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu. Ikiwa tetemeko lilitokea Bukoba na hapakuwa na hata kipimo cha kutambua kabla hatua stahiki zikachukuliwa, na bado serikali ikasema haikuleta tetemeko, niina mashaka na uwepo wa technolojia ya ulizini wa mipaka yetu hasa katika bahari na sehemu zisizokaliwa na watu. Kuliko kutumia nguvu kubwa kudhibiti wapinzani, ninaomba serikali iwekeze kweney technolojia surveillance ndani na nje ya mipaka yetu. Polisi wanaoonyesha uharamia kama kunyang'anya mali za mahabusu kwa nguvu, kutetea uharlfu ndani ya jeshi, kuonea na kusingizia raia, wanatakiwa kuondolewa kwenye kikosi hivi kwa sababu hawa ini hatari kwa jeshi lenyewe. Wanaweza kuuza taarifa hata mipango ya dani ya jeshi kwa maslahi ya 1000,000. Ondoeni maharamia kati ya polisi, sukeni jeshi letu upya, kisha liwezeshwe kwa technolojia inayoona na kutoa taarifa ya matukio hasa katika maeneo yenye wasialam wengi kama huko pwani na mkuranga.

Watanzania ninaomba sana tuendelee kuishauri serikali japo inakataa kushauriwa. Hii la kukataa ushauri wa wanaoongozwa tulichukue kama tatizo linalohitaji tiba kama maradhi lakini hatwezi kujenga taifa pasipo kushauriana na kusikilizana. Ccm ninyi ndio wenye viburi, ninaomba muwe wa kwanza kujirekebisha. Tambueni bila taifa lenye amani ccm haipo.

Viongozi acheni kujenga matabaka miongoni mwa wananchi. Acheni kuwadharau watanzania na kuwabagua, huku mkifanya kebehi za wazi kwa viburi. Migawanyikio mnayoijenga ndiyo inayoondoka mishkikamano na mioyo ya uzalendo . Bila kuwa na umoja na uzalendo, hakuna suluhu rahisi ya matatkzo yanayoinuka.

NINAOMBA NISIITWE MCHOCHEZI MAANA SERIKALI INADHANI IKIWAUNGA WATU VINYWA NDIYO INASHINDA, KUMBE INAJENGA ROHO MBAYA ZA KIKATILI NA MTAWANYIKO UANOANZA KULIGHARIMU TAIFA KWA KASI HII YA AJBU.
 
HII KIPANDE YA KUTOKA TEMEKE MWISHO KUELEKEA RUFIJI IFANYIWE OPERATION MAALUM KWA MSAADA WA JESHI NA KWA MSAADA WA RAIA WEMA NA JWTZ./ DEPLOYMENT YA TISS IPELEKWE HARAKA KWANZA KABLA YA OPERATION KUANZA.
•nadhani hapa ndipo pahala tiss wanapaswa kufanyia kazi na si kazi hizo zingine ....!/
 
Back
Top Bottom