Shemeji yangu hataki kuhama nyumbani akajitegemee

Shemeji yangu hataki kuhama nyumbani akajitegemee

Noma sana, Nimeanza kujitengemea nikiwa na miaka 10 nipo fikisha miaka 20 nimerudi mikononi salama ya Mama yangu...... Ahahah
 
Yan kusema tu shemeji kuna chumba kizuri kwa jirani nimesikia wanakodisha apo nimekishika kwa ajili yako, unashindwa kumwambiaa
 
Hata hivyo umejitahidi kuka nae miaka 9,wanawake na msaada walio wengi ni kama mashariki na magharibu,wanavumiliaga tuu
 
Wanawake wanarojo mbaya sana au kisa si ndugu yako mbna mnakua n ubinafsi sana hauwezi jua Labda MTU ndo anajipanga aanze maisha yake vzur, ebu kua na roho nzur bc Hata kwa mwenyezi Mungu atakubariki

SAA nyingine mnalaumu wanawake acha mama wa watu alalamike kama yupo na mabinti nyumbani lazima awe na wasi wasi. Kuna vitu vingine hatuwezi elewa dunia ya sasa kuishi Na ndugu wa kiume ni risk heri uchukue simba wa porini ukae nae. Hata mama ako wewe kuna vitu alivifanya ili akulinde. Na kama mtoa mada angekuwa na roho mbaya huyo Shemeji asinge maliza hata Mwaka. Binadamu kuna kipindi tu inafika unachoka anataka happy time na ur own family. Mtoa mada sijui unaishije na Mme wako ila kama hakusikii tafuta rafiki labda wa Shemeji yao ajaribu kuku advice akapange au kama ana girlfriend amshauri.
 
Mwone ,,labda wewe ndo kila kitu hapo .

Yaaan Mimi niwe boss Wa nyumba ,, kila kitu nikitoe Mimi ,,hakuna kinachopungua ndani ,,, alafu eti ooohhhh Muondoe Dogo wako baby ujue keshapata kazi oohhhh analipwa 2 M ,,kwan nn umepungukiwa ??????? Yaaaan kufura kwako ndo shidah [emoji57] [emoji57] .

Utakua mchaga wewe au mnyakyusa. ... Kama nimimi daaahhh nahisi wewe ndo nahisi utakua umechoka kukaaa kwaiyo nilazima utaondoka wewe kwanza .

Mimi napenda kukaaa nawatu napenda nyumba yenye vicheko ,sio ulete mambo ya baby sasa nyumba niyetu wawili tuuu[emoji23] [emoji57] [emoji108] .alafu unakuta nyumba inavyumba sita,,,, ivo vingine unataka ufugie majini ???
yaani kama nina uwezo na bangalow la kutosha,dogo kuondoka kwangu ni mpaka siku akiamua yeye,wanawake ni selfish sana,hawafikiriagi kesho na yeye anaweza kwama
 
Shemeji umekuja kunitangaza humu duh leo nahama usijali!!!
Kweli, dogo hama kwa kakako . umeshakuwa mtu mzima na kaz unayo bado tu unambana shemejio. Mwache shemejio afanye mambo yake kwa kakako. Wewe ndo unamzuia kujimwaga na mmewe. Au kakako anakumega??!!
 
tuanzie hapa, Je wewe ndo unayetoa matumizi yote ya familia?
 
Hata kama ujumbe ni fix....

Ila umefika.
 
Nashindwa kuelewa kwanini watu wengi mnamponda mleta mada. Au na nyinyi ndo hao hao?


Inakuwaje mwanaume mzima unakaa kwa kaka yako unapokea mshahara,tena wa kutosha,lakini hata chumvi huchangii?? Ina maana hata akitaka kuoa ataleta mke wake humo humo? Labda kama ndo kaanza kazi mwezi uliopita basi anahitaji muda wa kujipanga kama sivyo anakosea sana.



Na huyo kaka mtu nae zombi kama mdogo wake labda kama we mleta mada ulishaanza kumkataa shemejio kabla hata hajaletwa maana kama ni hivyo huyo mumeo hatokusikiliza kamwe sababu atajua bado una chuki na mdogo wake.
 
Acha roho mbaya huyo ni kama mtoto wenu huwezi jua huko baadae atakusaidia vp ww binafsi au familia yako au watoto wako
 
Hii roho mbaya kwa brother ake ahame vp kwani nyumba imejaa
 
Hara ukilipwa milioni mia, huwezi kutatua changamoto zote kwa siku moja!
Lakini kusubiri mpaka amalize changamoto zote ndio ahame si hatahama kamwe? Swali la kizushi, hivi mtu anatakiwa ajistukie na kuhama kwa 'watu' wakati gani? Maana hakuna ajabu kuishi kwa madada/makaka/ndugu wengi tumepitia huko.
 
Wanawake wanarojo mbaya sana au kisa si ndugu yako mbna mnakua n ubinafsi sana hauwezi jua Labda MTU ndo anajipanga aanze maisha yake vzur, ebu kua na roho nzur bc Hata kwa mwenyezi Mungu atakubariki

Acha unafiki,

Mtu mzima akae kwa mtu hadi apate kazi, ahudumiwe kama mtoto?? Anajipanga na nini? Kwamba asijiongeze akachangia chochote wakati analipwa ili ale za wenzie????

Huyo ni mariooooooo girlfriend wake ana mzigo. Mwanaume akipata kazi na bado hajishtukii kuwa tegemezi ni hewa sana.
 
Hapo dawa ni ndogo kila ukipika weka chumvi nyingii visa kibao ataondoka ila ukizubaa utaondoka wewe kumbuka hao ni ndugu
 
Kwa nini mmeo anakupuuza ishu nyeti kama hij?? Anza na yeye, ye ndo tatizo.
 
Back
Top Bottom