Shemeji yangu hataki kuhama nyumbani akajitegemee

Shemeji yangu hataki kuhama nyumbani akajitegemee

Kama ana kazi akapange.
Ila aambiwe na kaka yake ole wako ulianzishe wewe utanuka kama samadi kwenye familia nzima.
 
Habari wana jamvini,

Niende moja kwa moja kwenye hoja kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Mimi nimekaa na shemeji yangu toka yupo sekondari, amemaliza sekondari kamaliza chuo na ni nimemsaidia kapata kazi na analipwa milioni 2 na sasa kamaliza master.

Ila huyu shemeji yangu hataki kuhama nyumbani akajitegemee na mimi nahisi nimemchoka jamani, mpaka lifti asubuhi kazini nampa na mwacha kazini na jioni nampitia na hana aibu na kishoka mbele anakaa kwa kweli mimi nimemchoka kabisa.

Ila kumwambia ndo siwezi, na nikijaribu kumchomekea kaka ake naona ananipotezea hapa nafikiria nimwambie live shemeji kapange sababu kwakweli nahisi nimemchoka kama fadhira nimeshamfanyia.

Au nyie wanawake wenzangu mnawavumiliaga mpaka na kuozesha mnawaozesha? Hata mkate wenyewe kununua hanunui ela yake anajua mwenyewe inakoishia, mimi hata asiponunua sina shida ila shida yangu sasa ni haondoke akapange. Mimi kwa upande wangu sina hata ndugu yangu ninaye kaa nae na hajawai kukaa.

Kwakweli bwana shemeji nimekuchoka, na nyie mashemeji mlioko humu mnaokaa kwa kaka zenu siyo mnakaa kama mmefika mwisho wa reli.
Wote wanaojibu huu Uzi ni wanawake,coz amesema au nyie wanawake wenzangu mnasemaje.
Haya Dada ngoja waje akina miss natafuta
 
Umemchoka we mwenyewe kwako unaweza kuta hiyo nyumba mnayoishi hata senti hukuchangia kama unaona umeshindwa kabisa ondoka waache usitake watu wavunje undugu wao kwa mtu walokutana na wewe ukubwani yani wanawake sijui tupoje hivi kama mdogo wako kweli ungeongea hayo
 
ROHO MBAYA HIYO, HLO GARI KANUNUA KAKA YAKE, NYUMBA YA KAKA YAKE, CHAKULA CHA KAKA YAKE. KAKA YAKE HAJAMCHOKA KWANIN WEWE UMCHOKE? ADA KAMLIPIA KAKA YAKE. HALAFU HUELEWEK, TATZO NI WEWE HAKUNA NDUGU ANAYEKAA HAPO? AU KWA SABABU HANUNUI KTU? AU KWA SABABU UMRI WAKE UMEKWENDA? NAKUSHAURI, UWE NA STRONG REASON, VINGNEVYO UTAONEKANA UNA ROHO MBYA NA UCHOYO. HUYO IKFKA TAREHE ZA KUHAMA ATAHAMA MWENYEWE BILA SHURUTI.. ILA KAMA UNAONA ANAFAIDI SANA, BAS MWITE NDUGU YAKO NA WEWE AJE KUKAA.
 
Back
Top Bottom