Shemeji yangu hataki kuhama nyumbani akajitegemee

Shemeji yangu hataki kuhama nyumbani akajitegemee

dagaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
290
Reaction score
382
Habari wana jamvini,

Niende moja kwa moja kwenye hoja kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Mimi nimekaa na shemeji yangu toka yupo sekondari, amemaliza sekondari kamaliza chuo na ni nimemsaidia kapata kazi na analipwa milioni 2 na sasa kamaliza master.

Ila huyu shemeji yangu hataki kuhama nyumbani akajitegemee na mimi nahisi nimemchoka jamani, mpaka lifti asubuhi kazini nampa na mwacha kazini na jioni nampitia na hana aibu na kishoka mbele anakaa kwa kweli mimi nimemchoka kabisa.

Ila kumwambia ndo siwezi, na nikijaribu kumchomekea kaka ake naona ananipotezea hapa nafikiria nimwambie live shemeji kapange sababu kwakweli nahisi nimemchoka kama fadhira nimeshamfanyia.

Au nyie wanawake wenzangu mnawavumiliaga mpaka na kuozesha mnawaozesha? Hata mkate wenyewe kununua hanunui ela yake anajua mwenyewe inakoishia, mimi hata asiponunua sina shida ila shida yangu sasa ni haondoke akapange. Mimi kwa upande wangu sina hata ndugu yangu ninaye kaa nae na hajawai kukaa.

Kwakweli bwana shemeji nimekuchoka, na nyie mashemeji mlioko humu mnaokaa kwa kaka zenu siyo mnakaa kama mmefika mwisho wa reli.
 
Muite,Muulize kwanza anaplan gani na maisha yake maana huwenda ikawa ye anahic anachokifanya ni sahihi hvy bila kumwambia hawez jua,ongea nae vizur kana kwamba unampa ushaur yeye saiz ameshakuwa muda c mref atakuwa baba mwambie tu kwa upole ili ajue kwamba unafanya hvy kwa faida yake
Huwenda ikawa hapati mtu wa kumshaur

Usimchoke huyo ni ndugu wa mumeo mvumilie tu
 
Wanawake wanarojo mbaya sana au kisa si ndugu yako mbna mnakua n ubinafsi sana hauwezi jua Labda MTU ndo anajipanga aanze maisha yake vzur, ebu kua na roho nzur bc Hata kwa mwenyezi Mungu atakubariki
usilolijua ni kama ni usiku wa giza, fadhira zote izo nilizotenda bado unaona bure, miaka 9 unaenda wa 10 ninae. sasa kujipanga vip unakuta? acha niwe na roho mbaya
 
Muite,Muulize kwanza anaplan gani na maisha yake maana huwenda ikawa ye anahic anachokifanya ni sahihi hvy bila kumwambia hawez jua,ongea nae vizur kana kwamba unampa ushaur yeye saiz ameshakuwa muda c mref atakuwa baba mwambie tu kwa upole ili ajue kwamba unafanya hvy kwa faida yake
Huwenda ikawa hapati mtu wa kumshaur

Usimchoke huyo ni ndugu wa mumeo mvumilie tu
nitajaribu tena
 
Mlipie kodi ya chumba.. Mwambie unamfanyia ivyo ili awe free na wufi.. Kodi ikiisha, inayofuata atalipa mwenyewe.. Frm there utakuwa umetua mzigo.
 
Back
Top Bottom