I hope mko salama ndugu zangu
Nisiwachoshe nanyooka mazima
Yapata wiki ya tatu sasa kila nikishika simu ya mke wangu nakuta charts zake na mtu anayedai ni ndugu yake.
Nimehoji mara kadhaa na amekuwa akisisitiza ni ndugu yake,leo asubuhi ameamka akaenda kufanya usafi nje huku nikibakia kitandani ukizingatia leo ni weekend.
Mara simu yake ikapigiwa ile napokea jamaa akakata huku mpigaji akiwa ni yuleyule anayedaiwa kuwa ndugu.
Alipokata nikazama kwenye text nikakuta chating kama kawaida tena wife anajaribu kumlalamikia jamaa mbn anamdanganya kila siku anamtumia hela na hatumi.
Nikamsubiri wife alipokuja nikamuuliza huyu unayemwomba hela kila siku ni nani?hakujibu na mm nikamuacha nikampa simu yake na nikamwambia nmechoka na hii tabia sasa kama hutaki kunielewa subiri vitendo.
Wife akajibu"siwezi kusubiri vitendo bora nisepe tu"na nikamwambia kumbe nia yako ni kusepa basi umechelewa.Ile namaliza kuongea hivyo akachukua begi akaweka nguo zake baadhi akabeba ameondoka ameniacha ndani namuangalia huku akitokomea.
Sasa wadau nichukue hatua gani za awali?Naombeni ushauri najua humu wengi tu ambao wamo kwenye ndoa na kuna wali na uzoefu wa muda mrefu hata kama haupo kwenye ndoa lkn pengine umekumbana na changamoto za mahusiano kwa namna moja au nyingine.
I hope nitapata ushauri utakaonisaidia by any means.