Dah! Wife umenivunja moyo aisee na siamin!!

Dah! Wife umenivunja moyo aisee na siamin!!

Boli linatembea

Senior Member
Joined
Dec 21, 2022
Posts
115
Reaction score
333
Salaam wakuu,
Mada hapo juu yahusika...basi bana baada ya kukaa America miaka miwili kasoro nilirud nyumbani kuona familia, ikumbukwe toka kipindi chote hicho mimi na wife tumekuwa tukiongea sana zaidi hta ya mara 8 kila siku pamoja na changamoto ya kupishana masaa, ukweli sikuwah kuhic chochote sababu wanakaa mji ambao sina ndugu na ni mbali na ndugu zangu so nikawa naona mke ninae

Basi bana ikatokea bahati kuna ndugu yangu nikamtuma akaenda kimya kimya wife akaleta vurugu sana et kwann kaja bila taarifa akamfanyia visa sana yule ndugu yangu akaondoka kumbe alimuachia namba beki tatu

Beki tatu kwa siri akaanza kufunguka kumbe na jamaa huwa anakuja usiku mara kwa mara analala,anapikiwa, anafuliwa na kupigiwa pasi na yeye alidhani huyo jamaa ndo mimi ila alistuka mbona watoto wanyonge?ndo kamwambia ndugu yangu , nikaambiwa nikapewa namba ya huyo beki tatu nikaongea nae asee ni kweli na watoto wameambiwa wamuite ankodady

Nimeenda likizo kimyakimya beki tatu akaogopa akasepa nimefikia gest nikajibana siku mbili nikiwa na huyo beki tatu nikaona nijipoze hasira kwanza.kaniambia kila kitu ni mbaya sana usiombe wadau, siku kama wiki wife hanipati kumbe nishatua kitambo, nikamvamia usk wa manane fungua mlango anatetemeka kukagua hamna kitu, cheki simu hamna kitu, nikaona usinitanie nikampiga talaka 2 kwanza nimtishe sababu alianza dharau, mbele ya mashahidi akakiri ni kweli ila hajawah kulala anamtembeleaga tu, mbaya zaidi nikamwambia muite kampigia jamaa yuko njiani mashahidi wakasema achana nae utajipa kesi hata kwa trump usirud uharibu future yako, mtoto wa kiume anasema ni kweli jamaa anakuja , nasikia akija wanalala ndani jamaa anapelekewa kila kitu sa zingine mpk sa tano asbh ndo anaondoka

Nilikaa nae ndani baada ya hizo talaka sababu sheria inatutaka tukae miez mitatu ndo nitoe uamuz kwamba zinakua tatu au mbili hizohizo, nimekula sana mzigo(ilibid) awali miez miwili kabla sijaenda nilikata matumiz hta watoto walichelewa shule wiki 4 ada haijalipwa

Huyu mwanamke anase alijua sitorud tena ameomba msamaha na naona pamoja na hayo anapambana ki ukweli hta pesa namzomtumia za ujenz amesimamia kwa 100% nimejionea, watoto wanakula, wanaenda shule, nyumba safi iko vizur, ila kwa alichokifanya nimerud huku likizo imeisha ilikua mwez tu moyo una kinyongo na naona daima itakua hivyo kifup moyo umegoma kusamehe pesa napata kwa tabu aisee imeniuma sana, nifanyeje jaman?mke anasema bado ananipenda sana na kwa vitendo nathibitisha ni kweli , nimalizie tu ya tatu au?je akija huku si yatakua hayohayo tu?na nimeondoka si jamaa ataendelea kupiga?nifanyeje? Hii ni stori ya kweli niko na depression take serious too
 
Dah pole mkuu ila kwanini unayaamini machozi ya mwanamke?? Unataka kuja kufia jela au kujiua nawewe baada ya kufanya mauaji ya huyo mwanamke au unataka kuishia Mirembe??

Hapo mlipofikia panatosha mzee mwanamke akishaanza hizo habari jua kifo chako kinakaribia..
 
two wrongs don’t make a right..
kilichofanya na wewe kulala na dada wa kazi ni nini..!? eti upunguze machungu mtseeeuuuw’..!!

mmekutana nyote ni wazinzi, ila ni vile nyani huwa haoni ………, hivyo hapo wewe wajiona msafi..!??
 
Msamehe sababu
1. Ulikosea kula tena mzigo.
2. Ulikaa naye nyumba 1 baada ya kosa.
3. Ulikubali kumsikiliza anavyo jiliza msamaha.
4. Mlee watoto wenu pamoja, watoto wanahitaji sana malezi ya wazazi wote, do it for them.
5. Hata ukioa mwingine lazima utamkumbuka tu(mazoea ni ulemavu wa akili).
Hitimisho:
Ukikaa naye usipomuacha ujue huyo maisha yako yote una kinyongo naye hata maumivu ya moyo wako yakipoa.
Hautamuamini tena maisha yake yote. Huyo amesha piga muhuri kwenye akili yako kwamba siyo mke mwema.
Kwa 90% ipo siku atarudia uzinzi wake. Kwa sasa anajuta kweli toka rohoni ila muda ukienda sana ataona kawaida tu, yeye siyo wa kwanza. Kisha atarudia kosa.
 
Back
Top Bottom