Shemeji ulichofanya ipo siku tu

Shemeji ulichofanya ipo siku tu

Nakuambia achana Na mapenzi ya Dada yako mapenzi hayatabiriki ndugu yangu utakuwa utaona nakuhakikishia Dada yako anaweza akarudiana Na huyo shemeji yako achana nao tu wote wawili mtoto Wa kiume kumfatilia Dada yako tena ameolewa ni ujinga
 
Shemej yako mkurya anamatatizo ila familia yenu inamatatizo zaidi,nahuenda hayo ndo yaliyompelekea mkurya kumsalit dadako..!
**familia yenu haina usiri kuanzia mama mpaka kwa jarome,mpaka nikahis huenda mwandishi anamatatizo yakijinsia.
Haiwezekani mamako akitaka kununua boxer yamkwe wake mpaka aweke kikao chafamilia.
** haiwezekani ww mtoto wakiume ujue kuwa shem wako yuavaa chupi badala yaboxa,ndo maana napata shaka najinsia yako iliyompelekea dadako akwambie yachumban mwake namumewe unless uwe namatatizo yakijinsia.

##familia yenu nimbovu,haifai kuolewa au kuoa coz haina usiri wakutunza hata jambo la chupi,ndo itaweza kutunza kasoro za kitandan??#
kajifunze kwanza kuandika mkuu alafu familiaa yetu hainateam ya wadada ya kuja kuolewa as longer as ashapata mtoto anaweza akabaki hivyo hivyo sio lazima kuolewaa bwana by the way kununuliwa vitu kama hivyo lazima nijue cozwakati nikiwa naenda shoping na mama na yy alikuwa ananunuliwaa na walivyo gombana pia nilijua mengi hayo ni machache
 
Nakukanya achana Na mapenzi ya Dada yako mapenzi hayatabiriki ndugu yangu utakuwa utaona nakuhakikishia Dada yako anaweza akarudiana Na huyo shemeji yako achana nao tu wote wawili mtoto Wa kiume kumfatilia Dada yako tena ameolewa ni ujinga
sio rahisi kuacha aiseee
 
aisee kinachouma zaidi ni kutukana familiaa bora wangetukanana na mkewe sisi yasingetuhusu
Sema Shida Nyingine Uyo Jamaaa Badae Anaweza Kuja Kwa kuingia tena kupitia Huyu Dada Etu

Wanaweza Wakaanzisha vimausiano Vya chin kwa chin Had Wakarudiana tena

Mwambie Dada Etu Awe Siriaz Na Hili Swala Kama Kaamua kuacha ache Kabisa

Badae Asije Sema Hoooo Huyu Mume wangu

zile Zilikuwa tofaut Ndogo Ndogo Ivyo Siwez Muacha

Kiukwer Wanaume Wanambinu Nyingi sana Za Kuwa Atack Vimwana

So Take Care Sana
 
Mimi binafsi mambo ya huba huwa siyaingilii kwa kiasi hicho tangu nilivyotiwa aibu na dada yangu.....

Nakumbuka dada yangu alikuja nyumbani akiwa kavimba utasema amegongwa na gari huku jicho moja likiwa limejifunga kwa uvimbe...

Ile hali ilitustusha pale home kama unavyojua uchungu wa dada aujuae kaka....na damu ni nzito kuliko maji....

Vijana wa kiume tukahamaki na kujiorganize kwenda kumshikisha adabu shemeji........

Tulifanya uvamizi mkubwa na kutoa kichapo kikubwa sana...kwa shemeji tukiamini kuwa ule ndio mwisho wa yeye na dada yetu......dada yetu alitushukuru sana na kutuahidi kuwa kule hangeweza kurudi tena maana yule jamaa ni mnyama......

Baada ya mwezi kupita tukamuona dada ameanza kubadilika kumbe alikuwa tayari ameshatudiana na lile lijamaa....hakika ilikuwa ni aibu ya mwaka...

Tangu hapo nikala kiapo kuwa sitaingilia tena ugomvi wa mtu na mume wake labda wakiwa wanakaribia kuuwana....
 
Mjifunzage...

Hawa "mashemeji" wanaowaoa dada zenu wakiwa na hali ngumu mkaanza kuwaenga enga kama mayai na kujidai eti "mnawaboost" nao wawe "watu" mjini mwisho wakishatoka kimaisha yanakuwaga "mashetani watu" Most of them ni wezi wa fadhila. Washenzi kweli hawa watu.
 
Mimi binafsi mambo ya huba huwa siyaingilii kwa kiasi hicho tangu nilivyotiwa aibu na dada yangu.....

Nakumbuka dada yangu alikuja nyumbani akiwa kavimba utasema amegongwa na gari huku jicho moja likiwa limejifunga kwa uvimbe...

Ile hali ilitustusha pale home kama unavyojua uchungu wa dada aujuae kaka....na damu ni nzito kuliko maji....

Vijana wa kiume tukahamaki na kujiorganize kwenda kumshikisha adabu shemeji........

Tulifanya uvamizi mkubwa na kutoa kichapo kikubwa sana...kwa shemeji tukiamini kuwa ule ndio mwisho wa yeye na dada yetu......dada yetu alitushukuru sana na kutuahidi kuwa kule hangeweza kurudi tena maana yule jamaa ni mnyama......

Baada ya mwezi kupita tukamuona dada ameanza kubadilika kumbe alikuwa tayari ameshatudiana na lile lijamaa....hakika ilikuwa ni aibu ya mwaka...

Tangu hapo nikala kiapo kuwa sitaingilia tena ugomvi wa mtu na mume wake labda wakiwa wanakaribia kuuwana....
Haya mambo achaga tu mzee mwenzangu..

Mambo ya watu waliokwisha kulala masiku kadhaa na suti zao natural huwa wanaachana kimwili tu nyoyo haziachani.
 
Habari wanaJF,

Naanza week kwa machungu makubwa na kwa hasira isiyokuwa na wa kunituliza.

Kwako shemeji Mkurya,

Naandika kwakuwa najua unaingiaga JF 24/7. Nachotaka kukuambia ni kuwa Mungu yupo kwa ulichomfanyia dada angu. Nataka nikupe taarifa tu kuwa alopewa kapewa na kama kikitoka kimoja huwa vinarudi zaidi ya kumi.

Baada ya kumuoaa dada angu ukakaribishwa home ukawa unalelewa zaidi ya mimi mdogo wa mtu. Familia yetu ilikutunza kama mtoto mchanga mpaka vocha ukawa unanunuliwa ila shemeji shukrani huna, ulijivika ngozi ya kondoo dada angu kakuogesha ukatakata na sasa una shine mjini umejisahau.

Wewe wa kumletea dada angu mke mwingine ndani wakati nyumba ni ya dada angu na kila kitu ni cha kwake? Yaani aiseee ulichokifanya kimeumiza saana familiaaa yetu.

Umesahau baba na mama ndo walokulipia ada yako ya masters baada ya kujifanya wewe ni mtu wa shida sana? Umesahau mama alikununuliaa kila kitu ili uonekane na wewe mwanaume wa mjini? Daah shemeji hakika umefika mjini nakuaandikia kwa kuwa najuaa ujumbe utakufikiaa.

Kupata kazi usidhani ndo umeyapatiaa maisha na kuleta jeuri. Kumbuka ulikuwa unanunuliwaa mpka boxer manake ulikuwa hujui boxer ni nini zaidi ya kuvaaa machupi mtu mzima? Majibu yako na matusi yameisikitisha familiaa na tulichoamua ni kuwa dada angu hatorudi tena kwako na sisi hatutaki kukuona tena na mwanao hutakaa umuone tena wala mkeo hutakaa umsikie tena. Jiandae kwa talaka ya kanisani.

Mwanaume gani wewe ndoa haina miaka 3 ushaingiza mke mwingine ndani? Kwanza tulikukataaa familiaa nzimaa ulivyokuja kama msukule ila dada angu na kiherehere chake akakung'ang'aniaaa na kujifanya kakupenda wewe tu.

Sasa hatma yako imefika, hatukutaki home wala hatutaki kukusikiaa from now onwards, usije niuliaa dada angu akati tupo wawili tu kama macho, ila kumbuka shida hazina mwisho kila kitu chetu twaja chukuaaa shemeji usiyejielewaaa.

From your brother inlaw,

Jerome j.k
duh
 
Kumsaidia huyo jamaa mchukulie tuu kama mlitoa sadaka.Wanaume wa hivyo mwishowe ni majanga.Tena mshukuru Mungu dada yako yupo hai labda wanaweza kurudiana.Vinginevyo angeshamuua kabisa ulete uzi wa simanzi humu.Cha msingi wakati jamaa analetwa mama ndo alitakiwa ashikilie msimamo kuwa mwanaume asiyetokwa jasho ni marufuku kumuoa binti yake full stop.Nakushauri usifuatilie tena huo uhusiano najua unaumia ila ndo hivyo.Pale mwanzoni ndo mlikosea.Hakuna mwanaume anayenyekea mwanamke,wakwe na shemeji kwa maisha yake yote.Hufanya hivyo kwa kitambo tuu na kwa sababu maalum huyo shemeji yako kitambo kilishapita na sababu ya kukosa kipato ilishaisha.Sasa anataka asimame kama mwanaume anyenyekewe na yeye .Na ukweli uko wazi mwanamke akikuhudumia sana kwa kiasi alichofanya sister ako unyenyekevu kwa mume ni 0.Na matokeo yake ndo hayo tena kwa mkurya ndo mlibugi kabisaaa.Ila poleni kwa yote aisee kama nakuona vile ulivyo na machungu.
 
kilichokea sio mamabo yake mkuu mwanaume kucheat ni jambo la kawaida huo ndio uanaume ilaa kusahau yote na kutukana wazazi wangu hiyo ndo imeumiza saana familiaa bora angemtukana mkewe kwa sababu hayatuhusu ila katukana


kwahili lazima niiingilie kwa sababu kaitukana familiaa yetu ilhali kalelewaa kama mtoto mchanga and by the way my sister kasha moove on na hamna kurudi nyuma kamwe tupo wawili kama macho mkuu na wazazi wetu hawtarajii na hwawezi tena kuzaa kwa sasa sa kwann aje kuleta mabo ya kijinga
Jiangalie sana ndugu mwanamke siyo mtu wa kumuamini sana,hata mm ilinitokea hiyo tena mm kwao na mwanamke walinichukia woteee anzia mashemeji,wakwe zangu na ndugu wote upande wa mke wang,nilitengana na mke wangu ikabidi niwe naenda kumusalimia mwanangu na kutoa chochote,ck moja nilipoenda kumsalimia mwanangu walinifanyia fujo walinipiga sana,anzia baba mkwe mama mkwe mashemeji woote walinichangia kunipiga,,niliamua kuondoka kbsa mkoani kwetu baada ya muda mke wangu akaomba radhi tumeludiana,sasa aibu iko kwa hao walionidhalilisha kwa kunipiga utadhan hawanijuw sa hizi hata kwangu hawana hamu ya kuja,jifunze ndugu yangu mapenzi ni mapana saana hayasomeki kwa kusoma neno mapenzi tu,kuna siku tu wataludiana maana hakuna kabuli la mapenzi
 
Ila mi niliwahi kuwaambia wadogo zangu, yani siku ukiwa na boyfriend sijui akanyanyua mkono kukupiga..walai kama unampenda sanaaaa basi hakikisha sifahamu la sivyo sitojali ni baunsa kiasi gani ila nita deal na yeye sawia!!!

Somehow nakuelewa..ila ndo maisha...think positively, kila jambo lina jema lake! (ingawa ni ngumu kukubali)
yaani mkuu upo kwenye maind yangu mana niliapa mtu akinyanyua mkono japo kofi tu juu ya dada yangu tutaenda wote segerea manyinyaa!!
 
Aiseee mie sijaumbwa na huo uoga kabisa ukinikosea nakwambia live lakini haya mambo yakumuandikia ujumbe ilihali una uwezo wa kumwambia live.Kama mtu mlimsaidia kihivyo hana fadhila na haukupaswa kumficha ficha wewe mwanaume unaongea nae kiume unamwambia ya moyoni ila hizi mambo tuachie watoto wa kike japo mie pia nisingeweza kumuandikia ujumbe ningemwambia live bila chenga
Wee utakua mchoyo tu ulitaka tusiongeze uzoefu au unazani ameshindwa kumwambia?
Na huenda niutunzi tu mana haya mambo yapo
 
kwa hili ni la familiaaa sio lake na mkewe yaan alikuwa kama mtoto home na sio shemeji ilaamkapata kazi kaitukana saan familiaa while kosa lake mwanaume unashindwa kujizuiaa ndio basi kcheat ndo mpaka mimba jaman??
Jerry
Kama nakufahamu hivi,unakaa tangi bovu?
 
Kuwa na akiba ya maneno. Huyo ni dada yako mengine hawezi kukwambia. We unaweza kuona ndo mwisho lakini wakarudiana. Tumeona mengi. Kwahiyo nakushauri uwe mpole we ni kaka mtu na vigumu kumsemea dadako. Dadako akisema haya unayosema angalau tunaweza kuamini ingawa napo.wengi baadae hubadilisha maamuzi. Haya mambo ya mahusiano yako complicated usiyachukulie kwa hasira. Ikitokea dada akarudi kwake we utaishiwa la kusema. Mkianza maneno anaweza.kukwambia unamgombea dada yako. Hivyo nafikiri hili jukumu muachie dada yako ndiye mtendwa.
Nikiunga mkono hoja nna tukio mkwe wangu ananyanyasika mpka huruma mwisho kaachwa ndugu wote wakashukuru baada ya mda wanaibana kwa siri watu tumebaki midomo waziiii hahahaa mapenzi ni nouma.
 
Kule kwetu Mara,mwanamke analazimishwa tu kuwa na mke mwenza. Jamaa hajamwacha dadako bali kamwongezea msaidizi
 
Huyu jamaa kashusha heshima ya kiume.......lakini machozi ya mwenye haki ni nuksi kweliekweli,yatamtokea kwenye kiini chake.
 
Aiseee mie sijaumbwa na huo uoga kabisa ukinikosea nakwambia live lakini haya mambo yakumuandikia ujumbe ilihali una uwezo wa kumwambia live.Kama mtu mlimsaidia kihivyo hana fadhila na haukupaswa kumficha ficha wewe mwanaume unaongea nae kiume unamwambia ya moyoni ila hizi mambo tuachie watoto wa kike japo mie pia nisingeweza kumuandikia ujumbe ningemwambia live bila chenga
dogo jerry muoga.....na anaongea kama dem......bado kavulana.....hayo mambo ya wakubwa we tulia utayakuta...
 
Back
Top Bottom