Habari zenu
Nimefanya kazi ya uganga kwa miaka mingi, kazi hii imenipa kula, nimejenga nyumba tatu, Dar 2 na Mwanza moja, ila sina amani ya roho, na sipati hela kama zamani nimekuwa natamani kuiacha na kuwa mtu mwema bila mafanikio.
Wateja wangu wengi ni akina mama, wanaokuja kutaka ndoa, watoto na kuwadhibiti waume zao, sina ujuzi wowote wa dawa wala uganga Bali tuna mtandao wetu Wa waganga feki ambapo tunapeana mbinu mbalimbali na kushirikiana
Mfano ni mama mmoja aliyefiwa na mumewe na kuachiwa Mali, alikuja kwangu kwamba nyumba yake ina mauzauza, nikafanya ramli ya uongo na kumwambia ni shemeji zake upande wa marehemu mumewe ndio wanamchezea, akaingia kingi, kila pesa anayopata akawa analeta na nikatembea nae, mwisho nikamuomba alete hati ya nyumba niifanyie zindiko, akaleta, tukaenda kwake nikiwa na wenzangu, tukajifanya tunaizindika, nilikuwa nimeshawabonyeza wenzangu, wakamwambia mama huwezi kuishi humu tena utakufa, akaenda kupanga yeye na wanawe wadogo wa shule ya msingi.
Tukaiuza nyumba tukatokomea, baadae alipata matatizo ya moyo akafa, kwa kawaida huwa hatukai sehemu moja, tukahama eneo, hata hivyo roho inaniuma hadi leo, maana wanawe wameteseka sana.
Kuna Dada mmoja nilipewa namba yake kupitia mtu flani, nilikuwa namuwinda siku nyingi sana maana ana hela sana, anafanya shirika kubwa, nilipopata namba, nikatafuta line nikamtumia sms ya kutisha sana, kwamba mimi ni fundi wa kiroho, kuna mtu kaja kushtaki kwangu kwamba umemkosea nikataja na kosa lenyewe, na anataka nikuondoe duniani, na hapa nipo kwenye maandalizi ya mwisho kabisa ya kuchanganya dawa ili nikamilishe hiyo kazi, sasa nikaone ni vyema nikusikilize na wewe upande wako unajiteteaje, wana Jf niligundua mwanaadam anaogopa sana kifo, huyu Dada alibabaika akaniomba nisifanye hivyo, yupo tayari kwa lolote.
Kwa kweli nilikula sana hela za huyu Dada, na akawa kama bibi yangu, tunalala mahotelini akisingizia yupo semina, mwisho nikakimbia na hela ya maana.
Baadae nikapata dawa flani kwa wenzangu ambayo ukiwa unaongea na mtu unampumbaza anaweza kukupa chochote alichonacho mkononi au kukufuata nyumbani hati au kadi ya Gari akishakupa ndo anazinduka na kuanza kupiga kelele katapeliwa.
Kwa sasa nimehamia Mkoani, azma ya kuwaandikia ninyi nikuwajulisha kuwa nataka kuacha kazi hii, nimepata msichana Mwanza nilikohamishia makazi yangu na nimejenga Nyasaka, huyu msichana nimempenda na ningependa kumuoa, ingawa hajui kama nafanya kazi hizi, maana nafanyia kazi hizi sehemu fulani nimekodi Chumba, huyu binti hapafahamu, ila nyumbani anapajua ninapoishi.
Nataka kuacha niwe mtu mwema, najua dini inakataza mambo Haya, lakini kila nikitaka kuacha najikuta nashindwa kwamba ntaishije, naweza kuacha kwa mwezi au zaidi lakini baadae narudia tena.
Wakati wa nyuma nilipata hela sana ila sikufanya cha maana, zaidi ya wanawake na starehe.
Sasa hivi napata wateja wa kawaida hela ya kula tu.
Nilikua nataraji nikipiga hela nyingi ndo niache niamie kwingine
Nahitaji kuacha