Sheikh Yahya Hussein afariki Dunia

r.i.p sheikh yahya .....inna illalah rajuun....


pole sana JK na wengine wote ...

Mwenyezi Mungu anasema ni bora kumtumainia yeye kuliko mwana adam..!!!
 
Ndugu wa Jamii,

Poleni sana kwa Msiba wa Mnajimu Mkuu wa Tanzania na Afrika Mashariki,

R.I.P sheikh Yahaya Hussein,

Watanzania tusiwe na tabia ya kufurahia mtu akifa,vitabu vitakatifu vinatufundisha kulia na kuomboleza,na wafiwa,tuachane na tabia/siasa za chuki,sisi watanzania ni wamoja na wapenda amani.
 
lol hiki kigagula kaaga?? hakutabiri?

Yahya Mtabiri????!! Mweeeh!!!

RIP Shekh Yahaya Poleni CCM

Pole sana Jakaya Kikwete na wafiwa kama habari hizi zinaukweli!

alikuwa anaweka usiku sana kwenye maendeleo ya nchi.....akavune alichokipanda kudadadeki....

sasa hivi shehe yahaya yuko na mabikira 80 anajivinjari nao....

Mkuu kupata bikira lazima ujilipue kwa bomu au kujiua huku ukiua wengine

huo ni utabiri au yameshatokea! tatizo litakuwa kubwa zaidi kwa wale wanaolindwa na yeye! namanisha wale waliopewa ulinzi na yeye!

Nina uhakika maandalizi ya kupata mlinzi mbadala yameshafanyika. He was a stateman, teheh tehe heh teheh haaaahaa ha

The info is true!

Mzee Yahya in no more, wamepeleka mwili wake Lugalo muda si mrefu.

Poleni wafiwa wote!


Hapo kwenye red, was he black amiri jeshi mkuu mpaka mwili upelekwe Lugalo hosp na si muhimbili?

angekuwa mnajimu huyo ni mwanamke angepewa watu gani? kwahiyo hata watu wakifa Uzinzi unaendelea tu!.
Imani zingine…..

Tatizoina bidi wakazi wa dar wakae vizuri maana yale majini yake hayana pa kwenda

Yatawaendea wateja wake tu, mnaopenda kwenda magogoni kazi kwenu…maana kule aliyaweka yeye kumlinda mkulu

ha ninashaka na khabari hizi!mbona sijaskia wimbo wa taifa?

Cd zimegoma, ulinzi aliouweka nao umetoweka.

pumzika kwa amani mzee Sheikh yahya, u will be remembered by many people.
For good or for worse?

Ni kweli sheh wa ukweli wa ccm kafariki R.I.P
duuuuuh

Huu ni msiba wa kitaifa ; itabidi Jakaya Kikwete arudi haraka toka Namibia asimamie mazishi ya kamanda!!!
Atangaze pia mapumziko ya kitaifa angalau siku mbili, bendera zote zipepee nusu mlingoti kwa majuma mawili
 
Kweli huyu alikuwa mnajimu, maana alitabiri kifo chake: alitabiri kuwa mwaka huu mtu maarufu atafariki- nadhani ndo utabiri umetimia.
 
kumbe hata yeye amekufa,nlidhani anatabiria wengine kufa kana kwamba yeye hataonja umauti.
Rest in pieces sheikh
 
Atakaye pingana na Jakaya Kikwete ndani ya ccm kwenye kinyan'ganyiro cha uchaguzi atafariki dunia-sheik yahaya
 
I just heard kwenye redio SHEIKH YAHYA AMEFARIKI...
 

ebu jikumbushe
 
Mods,
Unganisheni threads za tukio hili iwepo moja, zatuchanganya na repeated threads.
 
Habari


Sheikh Yahya:Naendelea kutoa 'ulinzi' kwa Kikwete

Mwandishi Wetu​
Septemba 15, 2010
Asema hahitaji ruksa ya CCM, serikali
LICHA ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kumkana, Mnajimu maarufu nchini, Sheikh Yahya Hussein, ameibuka na kusema kwamba hahitaji kibali katika kumwekea "ulinzi wa majini" mtu anayempenda - Rais Jakaya Kikwete.
Akizungumzia kauli za viongozi wa CCM na Serikali kwamba hawatambui "ulinzi wa majini" aliosema atautoa kwa Kikwete, Sheikh Yahya, amesema: "Sihitaji kibali cha yeyote kumuwekea rais wangu ulinzi wa majini."
Sheikh Yahya, ambaye amekuwa akitoa kauli tata kuhusiana na Kikwete hata kabla ya kampeni kuanza, alisema, jana, jijini, kuwa anachozungumzia yeye si uchawi wala ushirikina; bali ni mambo ambayo yapo na hayakwepeki.
"Kila mtu anazaliwa na jini. Hata Slaa (Dk.Willibrod Slaa, Mgombea urais wa CHADEMA) ana jini anaitwa Subiani. Nakwambia sihitaji kumshirikisha mtu katika hili," alisema Sheikh Yahya Hussein na kumkabidhi simu mwanae aliyejitambulisha kwa jina la Hassan, ambaye naye alisema;
"Sheikh alisema binafsi hahitaji kumshirikisha mtu katika hili. Serikali iendelee na ulinzi wake na yeye atatoa ulinzi wake. Mbona hao walinzi walikuwapo lakini akaanguka? Matatizo yale si ya kiafya. Sheikh anafanya kwa kuwa anampenda na hutasikia tena anaanguka."
Awali Sheikh Yahya alinukuliwa katika taarifa yake akisema kwamba atatoa ulinzi usioonekana kwa macho kumkinga Rais Kikwete ili mtu yeyote asijaribu kumfanyia ‘mchezo' wowote kama ilivyotokea Jangwani.

Sheikh Yahya alisema katika taarifa hiyo ya kuwa amefikia hatua hiyo kutokana na uchungu alionao kwa nchi na kwa Rais Kikwete anayempenda.

Kufuatia kauli hiyo, Dk. Slaa alikemea kauli hiyo na kusema: "Nchi haiwezi kuongozwa na uchawi. Haiongozwi na imani za watu, kila mtu ana imani yake, lakini tusifike mahali tukaongoza nchi kwa uchawi."

Alimtaka Rais Jakaya Kikwete kumkemea Sheikh Yahya kwa kauli hiyo iliyotolewa juzi Dar es Salaam, la sivyo wananchi wataamini mnajimu huyo anatumiwa na CCM kuleta hofu katika jamii.

Dk. Slaa aliwakumbusha wananchi kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, Sheikh Yahya alisema mtu yeyote atakayegombea urais na Kikwete atakufa na kuongeza: "Sisi wengine ni majabali, hatuogopi kufa kwa ushirikina."
Tayari serikali imesema haihusiki na hoja ya ‘ulinzi' usioonekana kwa Rais Kikwete, kama ilivyotangazwa na Sheikh Yahaya.
Hata hivyo, Sheikh Yahya alisema hakuwa anazungumzia uchawi wala nguvu za giza, "bali majini ambao ni viumbe kama sisi, isipokuwa wao wameumbwa kwa moto na sisi tumeumbwa kwa udongo na wametajwa katika vitabu vyote vitakatifu vya Waisalamu na Wakristo na Mwenyezi Mungu amesema tushirikiane nao".

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kampeni za CCM, Abdulrahman Kinana, alisema Rais Kikwete ni muumini wa Dini ya Kiislamu, ambaye anaamini Mungu na hivyo hahusiki kwa vyovyote na kauli ya Sheikh Yahya.
Kauli hiyo ya Sheikh Yahya imeibua mjadala mkali; huku baadhi ya wananchi wakitaka uchunguzi wa kina ufanyike kuangalia kama kuna fedha za umma zinazotumika kugharamia masuala ya ushirikina.
Baadhi ya wananachi hao, wakiwamo viongozi wa dini, wamekemea tabia ya baadhi ya viongozi kukimbilia katika imani za ushirikina baadhi wakitumia raslimali za umma katika kugharamia imani hizo.
Rais Kikwete amepata kuanguka hadharani mara tatu; mara ya mwisho ikiwa ni wakati akizindua kampeni yake ya urais, hivi karibuni, katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.
Alipata pia kukiri hadharani kwamba alimsaidia Sheikh Yahya fedha za kwenda matibabuni nje ya nchi.
 
Innallilahi waina illaihi rajiun ndio mwisho wa safari ya kila mja. Tena amefariki siku nzuri ya ijumaa. Shida ipo katika matendo yake kwakweli yalikuwa yanatusikitisha waislamu wengi inshallah mmungu amuhidi kwa yale aliyokuwa akiyafanya duniani kwani sote sie ni wanaadamu na hakuna mkamilifu duniani.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…