Sheikh Yahya Hussein afariki Dunia

Sheikh Yahya Hussein afariki Dunia

Huyu mzee nitamkumbuka kwa umaarufu wake, wenye umri kama mimi watakumbuka enzi zileee tukikusanyika nyumbani kwake na hata kule sabasaba tukiangalia mpira ktk video/TV. Huyu mzee ni miongoni mwa watu waliochangamka zamani.
 
Wewe wasema, no comprimise na wachawi na washirikina wanaojaza hofu wananchi. kifo cha huyu pepo mchafu ni GREAT RELIEF kwa Taifa.

Well, tutasema, kuwaza, na hata kuongea mengi. Kwamba Marehemu muda huu yuko wapi, mie sijui; au labda yuko kwenye ile mito itiririkayo vilevi akistarehe na wale mabikira, pia mie sijui; ila neno moja najua nalo litasimama milele:

"Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU AMBAO HAKUNA ATAKAYEMWONA MUNGU ASIPOKUWA NAO".

Na huo utakatifu hupatikana katika YESU KRISTO peke yake. Na tena, kisasi na hukumu ni vya Bwana MUNGU wetu.

Marehemu Sheikh Yahya apumzike kwa amani - AMINA.
 
dah kaaz kwel kwel hope ata meet Nyerere na kumegea data za huku!
 
Shekh mkuu na mtabiri Shekh Yahya Hussein amefariki dunia leo saa nne
chanzo ITV
 
Duh! Poleni Watanzania wote Mpendao Amani, Mshikamano na Umoja. Sheikh Yahya atakumbukwa sana kwa kutokuwa muumini wa UDINI.
 
Duh! Poleni Watanzania wote Mpendao Amani, Mshikamano na Umoja. Sheikh Yahya atakumbukwa sana kwa kutokuwa muumini wa UDINI.

Alikuwa anazitaka pesa za watu wa dini zote, sasa angekuwa mdini wale wateja wa upande wa pili angewakosa.
 
Uuwiwiwiwiiiiii ..... Rais atalindwa na nani?.......
 
huyu mzee si yuko safari huyuau karudi maana mlinzi wake kafa
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KUFUATIA KIFO CHA SHEIKH YAHYA HUSSEIN

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Sheikh Yahya Hussein kufuatia kifo cha Mnajimu Mkuu huyo kilichotokea asubuhi ya leo tarehe 20 Mei, 2011, katika Hospitali ya Mount Ukombozi iliyoko Morocco Jijini Dar es Salaam.


Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Sheikh Yahya Hussein ambaye enzi za uhai wake alijipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kutokana na kipaji chake katika masuala ya unajimu wa nyota ambao ulimpatia sifa kubwa, amesema Rais Kikwete katika rambirambi zake.


Ameongeza: Naomba, kama familia, mpokee salamu zangu za pole kwa kuondokewa na kiongozi muhimu na tegemeo kubwa la familia. Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya Marehemu. Amina.


Amesema Rais Kikwete katika salamu zake: Naelewa fika machungu mliyonayo katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wenu. Najua alikuwa mzazi, alikuwa baba, alikuwa babu, alikuwa mlezi na tegemeo kubwa la familia. Najua ameacha pengo kubwa ambalo litakuwa gumu kuzibika. Najua mko katika kipindi kigumu na cha majaribio. Hivyo nawaombeni muwe na moyo wa uvumilivu na subira. Yote ni mapenzi ya Mola. Napenda kuwahakikishieni kuwa niko nanyi katika kipindi hiki cha maombolezo ya msiba wa mpendwa wenu.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

20 Mei, 2011

Mkuu rekebisha heading. Hawezi kutoa rambimbi kwa marehemu.
 
Na leo ndio nimepata siri kwamba huyu Sheikh ubwabwa kumbe alizaliwa Bagamoyo.
 
kumbe kila kitu kinamfikia sio?ingekuwa taarifa ya umeme kukatika au watu kukpigika hataki kujibi anajifanya hajasikia kumbe anapata taarifa zote wajameni
 
People's pawaaaaaaaaaaaaaa, Sauti ya Slaa ni sauti ya watu, na sauti ya watu ni sauti ya Mungu, hivyo basi, Sauti ya Slaa ni sauti ya Mungu. Ole wake anaepingana na sauti ya Mungu kwani hayatampata mema. Shekhe huyu alipingana na sauti ya Mungu kwa kusema yeyote atakayesimama kumpinga Kikwete atakufa. Sasa hatima yake kama mpinga sauti ya watu (which = sauti ya Mungu) imefika. Tutoeni tu salam za rambirambi
 
Maskini hakuweza kujua au kutabiri kifo chake....rip all the same late Sheikh Yahya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom