Wakuu zangu,
Ifikie wakati tuwe na heshima na hizi dini zetu pamoja na kutambua ukubwa wa elimu kwani Sheikh Yahya ni mnajimu (Astronomy) ambaye huzungumzia vitu ambavyo dini zote na sayansi zinavikubali kuwa elimu hiyo ipo..
Ameitumia vibaya elimu hiyo ni swlaa jingine kabisa kuliko kuingiza habari za kumlinganisha Sheikh Yahya na Yesu.. Kwanza ni ukosefu wa imani na kumdharau Yesu mwenyewe kwani Utabiri sii kitu cha ajabu na wamefanya watu wengi sana hata kabla ya Yesu mwenyewe kuzaliwa.
Majini yapo, aidha tuamini au tusiamini lakini yapo na tunashindwa kuelewa kwa sababu sisi sote hatuna elimu hiyo.
Sheikh Yahya ni binadamu na tumwombee uhai na afya nzuri kama binadamu wengine kwani hakuna sehemu hata moja amedai Unabii au yeye kuwa sawa au zaidi ya Yesu. Sisi ndio tunamfananisha hivyo kubeba madhambi yote.